Iran: Wanafunzi Vyuo Vikuu na Sekondari wachachamaa kupinga udhalimu wa kidini, huku serikali ikilaumu Marekani na Israel

Iran: Wanafunzi Vyuo Vikuu na Sekondari wachachamaa kupinga udhalimu wa kidini, huku serikali ikilaumu Marekani na Israel

Aiseee huko Iran kinadada wameamua hijab zinavuliwa kama hawana akili nzuri,Death to America Leo imekua "DEATH TO THE DICTATOR"


Kuna kibibi humu sijui kinasemaje.
 
Na haka katabia wamerithishwa jamaa zetu. Wao kila kitu ni kulalamikia mataifa ya Magharibì. Ukweli ni kuwa kuna watu wengi wako kwenye hizo mambo za đini sababu tu ya sheria kali. Lakini ukitoa uhuru kwamba anayetaka kwenda ahera basi afuate haya, utaona uhalisia ulivyo kwa watu.
 
Wawa ambie tu, anayetaka kuvaa hijabu avae asiyetaka aache.

Kwanza katika Sharia za Kiislamu hakuna panapo hukumu adhabu ya kuto kuvaa hijabu.

Ni kama kuto hudhuria swala, au kufunga ramadhani au kuhiji maka au kutoa dhaka.

Na qurani yao inasema wazi hakuna kulazimishana kwenye mambo ya dini.

2: 256 - Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Kulazimisha wasichana warembo kuvaa hijabu, yaani kuwafuni sura zao nzuri na za kuvutia ni UDICTETA ULIOPITILIZA na ni dhambi kubwa sana.

Dini ya Kiislamu haitaki kabisa huo ujinga.

Wanakengeuka namna gani hawa viongozi uchwala.

Kitu usichoelewa ni kwamba, sheria hizi zinafuatwa ili na mwingine asitende dhambi hata kwa kutamani. Mimi ni mkristo. Ona wanawake wanavyoingia makanisani uchi. Ina wanavyovyaa bila hata aibu. Ni mtu gani ambaye anataka kumshika Mungu na kila uchao dhambi na ushawishi mbaya upo mlangoni?
Mimi nafurahia wanawake wa kislam wanavyojisitiri. Tatiz tuwafundishe nini maaana yake na sio kuishi kwa kukariri.
 
Kitu usichoelewa ni kwamba, sheria hizi zinafuatwa ili na mwingine asitende dhambi hata kwa kutamani. Mimi ni mkristo. Ona wanawake wanavyoingia makanisani uchi. Ina wanavyovyaa bila hata aibu. Ni mtu gani ambaye anataka kumshika Mungu na kila uchao dhambi na ushawishi mbaya upo mlangoni?
Mimi nafurahia wanawake wa kislam wanavyojisitiri. Tatiz tuwafundishe nini maaana yake na sio kuishi kwa kukariri.
Kama unamjua Mungu vizuri hizo tamaa ndo unatakiwa upambane nazo ili uzishinde. Usisingizie watu wengine kua wanakutia majaribuni. Mbona watoto watu. Mama zetu na dada zetu hatuwataman? Na tunaishi nao ndani ya nyumba zetu.
 
Sa Marehem mzazi wa mtu amepumzika kaburini kwake toka mwaka Jana wewe mpaka leo bado unateseka nae.

Hivi ndo baba ako awe anasemwa hivi mpaka leo ungejiskiaje Mbwa mkubwa wewee.
Mbona umeumia ?! . Kiongozi lazima asemwe kwa mema na mabaya pia. Kwani ndiyo kazi wanayoiomba . Kuwa kioo cha jamii.
 
Sa Marehem mzazi wa mtu amepumzika kaburini kwake toka mwaka Jana wewe mpaka leo bado unateseka nae.

Hivi ndo baba ako awe anasemwa hivi mpaka leo ungejiskiaje Mbwa mkubwa wewee.
Dikteta lazima asimangwe na kila mwenye akili timamu
 
Ayatollah anataka aambiweje kuwa hana chake tena aende Yemen na mashuka yake.
 
Yaani Iran ni nchi ya kikoloni, kidikteta kwa kificho cha dini ambapo hata angefufuka Mohamad angewashangaa kwa ukandamizaji huo!
 
Sa Marehem mzazi wa mtu amepumzika kaburini kwake toka mwaka Jana wewe mpaka leo bado unateseka nae.

Hivi ndo baba ako awe anasemwa hivi mpaka leo ungejiskiaje Mbwa mkubwa wewee.
Narukia mada: Baba yake asingeweza kufanya ukatili na unyanyasaji ule kwani Baba yake alikuwa na akili timamu.
 
Hivi kwanini waislam/waarabu wana utamaduni wa kusingizia watu wengine matatizo yao wenyewe??

Hata hapa zanzibar unakuta Vijana wanatoroka kujiunga Alshabab ila lawama zinatupwa kwa Watanganyika wanaotaka kuifitinisha Zanzibar.
 
Kitu usichoelewa ni kwamba, sheria hizi zinafuatwa ili na mwingine asitende dhambi hata kwa kutamani. Mimi ni mkristo. Ona wanawake wanavyoingia makanisani uchi. Ina wanavyovyaa bila hata aibu. Ni mtu gani ambaye anataka kumshika Mungu na kila uchao dhambi na ushawishi mbaya upo mlangoni?
Mimi nafurahia wanawake wa kislam wanavyojisitiri. Tatiz tuwafundishe nini maaana yake na sio kuishi kwa kukariri.
Okay sawa wewe hutaki kutenda dhambi...Vipi likianzishwa dhehebu ambalo wanaamini Viatu vyote ni vya shetani....Halafu waanze kukulazimisha wewe usivae viatu kwakuwa kwao wakiviona ni dhambi?
 
Kawaida dhehebu la Shia ni watu moderate, sasa hawa ma- Ayatollah wamezidisha kuminya raia matokeo ndiyo hayo vijana vyuo vya elimu ya juu Iran wana maswali mengi ambayo wazee hawawezi kuwapa majibu toshelezi:


Toka maktaba:

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1









KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)



Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.



Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi. Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...



Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...



Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.



Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.



Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq



Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.



Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.



Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.



Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.



Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.



Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.



Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi yaliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2







Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.



Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.



Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.



Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.



Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.



Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia



RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif





Source : Asadiqmedia
MK254
 
Hii tabia ya kuwalaumu watu kila siku ni uzembe wa grade A kama Magu nae kila siku mabeberu but no evidences

Waangalie kinachosemwa kama kweli kipo wajirekebishe

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
sasa Magu ameingiaje swala la Irani!! We n mpumbavu kuliko hata hiyo hoja yako
 
Back
Top Bottom