Iran yaalaani matamshi ya Trump 'ya kukosa heshima na yasiyokubalika' kwa Khamenei

Iran yaalaani matamshi ya Trump 'ya kukosa heshima na yasiyokubalika' kwa Khamenei

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amelaani siku ya Jumamosi, Juni 28, 2025, matamshi "ya kukosa heshima na yasiyokubalika" yaliyotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alidai "aliipiga Iran" na kumuepusha Kiongozi wake Mkuu Ali Khamenei "kifo cha kutisha na cha aibu.
Ikiwa Rais Trump anataka kweli kufanya makubaliano, anapaswa kuweka kando sauti yake ya dharau na isiyokubalika kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Mheshimiwa Ayatollah Khamenei, na kuacha kuwaumiza mamilioni ya wafuasi wake waaminifu," Araghchi ameandika kwenye akaunti yake ya X.

Heshima huzaa heshima"​

Watu wakubwa na wenye nguvu wa Iran, ambao wameuonyesha ulimwengu kwamba utawala wa Israeli hauna budi ila kukimbilia kwa 'Baba' ili kuepuka kuangamizwa na makombora yetu, hawathamini vitisho na matusi," Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza.

"Nia njema huzaa nia njema, na heshima huzaa heshima."

Katika ujumbe mrefu na wenye kuchukiza vibaya katika mtandao wake wa Truth social, rais wa Marekani ameikosoa Tehran siku ya Jumamosi kwa kudai ushindi katika vita vya siku 12 dhidi ya Israeli na kutangaza kuwa anasitisha kazi zote za kuondoa vikwazo dhidi ya Tehran.

Donald Trump anasema alimuokoa Kiongozi Mkuu "kutokana na kifo kibaya na cha aibu."

Donald Trump pia alimshutumu Kiongozi Muadhamu wa Iran kwa kukosa shukurani kwa kupuuza wigo wa mashambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi yake na kwa kusema kuwa Iran imeishinda Israeli na Washington "kupata pigo kubwa."

"Nilijua haswa alikojificha, na sikutaka kuruhusu Israeli au vikosi vya jeshi vya Marekani, ambavyo vilikuwa na nguvu zaidi na vikubwa zaidi ulimwenguni, vikatishe maisha yake," rais wa Marekani amebainisha katika mtandao wake wa Truth social.

"Nilimwokoa na kifo kibaya na cha aibu," alijigamba.

Marekani ilishambulia kwa mabomu vituo vitatu vya nyuklia nchini Iran usiku wa Juni 21-22, ikijiunga na mashambulizi yaliyoanzishwa na Israeli mnamo Juni 13 kwa lengo la kuzuia nchi hiyo kupata bomu la atomiki, nia ambayo Tehran imekuwa ikikanusha.
 
Khamenei ni mfu tayari , yupo ndani ya nchi yake na anajificha kwenye tunnels kama panya
 
Back
Top Bottom