kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Katika hali isiyo ya kawaida na isiyotarajiwa Iran imepandisha bendera nyekundu ikiashiria ishara ya vita kuu.
Kikosi cha mapinduzi ya kiislam kimeapa kulipa kisasi na kutoa jibu kali kwa Marekani. Tujiandae kushuhudia moto ukiwaka.
Taarifa zaidi;
Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran imepandisha bendera nyekundu juu ya Jumba Takatifu la Msikiti wa Jamkaran, huko Qom. Taarifa zinaeleza kuwa kupandishwa kwa bendera ya rangi nyekundu kunatoa ishara kuwa kuna vita kubwa inakuja au inaendelea.
Aidha, Ripoti hadi sasa zinaonyesha kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Iran kuipandisha bendera hiyo katika jumba hilo takatifu.
Zaidi ya hayo, inaelezwa kuwa bendela hiyo sio ya maombolezo wala ukumbusho wa tukio lolote isipokuwa ni bendera inayotumiwa na Iran kuhamasisha jamii yake yote kuelekea katika pambano ambalo hawajawahi kuliona. Sambamba na hilo, inaelezwa kuwa bendera hii nyekundu iliyopandishwa haikuwahi kutumika hata wakati wa vita vya Iran na Iraqi.
Bendera Nyekundu ya Hussein iliyoinuliwa juu ya msikiti unaashiria nguvu ya kivita kama ile ya Karbala na rangi ya damu ambayo inaweza kumwaga hivi karibuni kama kisasi cha kuuawa kwa Jenerali Qassem Soleimani, ambaye kwa sasa amekuwa wanamuita Shahid Soleimanii.
Iran ililiambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu, Antonio Guterres Ijumaa kwamba ina haki yake ya kujilinda chini ya sheria za kimataifa baada ya Marekani kumuua Qassem Soleimani, kamanda wa juu wa Kikosi cha Walinzi cha Udhibiti wa Mapinduzi cha Iran.
===
IRGC yaahidi hatua kali ya kulipiza kisasi baada ya kuuawa shahidi Soleimani
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassem Suleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na mashahidi wengine katika jinai ya Marekani Ijumaa asubuhi mjini Baghdad na kusisitiza kuhusu kulipiza kisasi kufuatia jinai hiyo.
Katika taarifa siku ya Ijumaa, IRGC imelaani hujuma ya angani ya vikosi vamizi na vya kigaidi vya Marekani ambayo imelenga gari lililokuwa limembeba Meja Jenerali Soleimani, wenzake na makamanda wa Harakati ya Al Hashd al Shaabi ya Iraq akiwemo mpigana jihadi mkubwa, Abu Mahdi al Muhandes ambaye alikuwa akitekeleza mpango wa kukabiliana na njama mpya ya Marekani ya kuhuisha ISIS na makundi mengine ya magaidi wakufurishaji sambamba na kuvuruga tena usalama wa Iraq.BTaarifa hiyo imesema waliouawa shahidi wamepata fahari kubwa.
IRGC imesisitiza kuhusu kuendeleza njia ya mashahidi na kuongeza kuwa, Meja Jenerali Suleimani hakuwa tu shakhsia bali alikuwa ni fikra kamili na kuanzia sasa maadui wataweza kushuhudia upeo mkubwa zaidi wa fikra hizo katika maeneo ambayo wameeneza satwa yao kinyume cha sheria duniani.
Taarifa hiyo aidha imesisitiza kuwa Meja Jenerali Suleimani na wengine ambao wamelelewa katika fikra za Utawala wa Faqihi na Mapambano ya Kiislamu, wamefungua ukurasa mpya katika mapambano na muqawama dhidi ya Wazayuni na katika kukabiliana na magaidi pamoja na Wamarekani wavamizi katika eneo.
Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi mapema jana Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ametoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani.
Sent using Jamii Forums mobile app