Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Habari za kijasusi za Marekani kwamba Iran wameisambazia Urusi makombora ya masafa mafupi zitakazotumika katika vita na Ukraine, sasa si siri tena baada ya mbunge wa Iran na mjumbe wa kutunga sera za kiulinzi kusema ni kweli wameshaipatia Urusi silaha hizo.
Akiweka wazi hatua zao hizo,mbunge huyo amesema nchi yake imekuwa ikifanya hivyo kwanza kukwepa vikwazo vya kiuchumi vya nchi za magharibi.Wanapeleka silaha hizo kubadilishana na maharagwe pamoja na ngano kwa matumizi ya raia zake.
Kwa upande mwengine taifa hilo lenye uhasama na Israel limesema tayari wameshakipatia chama cha Hizbullah silaha yake adimu na ya kipekee ya EMP ambayo ni maalumu kwa ajili ya kupiga mifumo ya kusambazia umeme na kulenga radar zinazotumiwa na jeshi la Israel kuongozea ndege zake za kijeshi.