Putin walimvimbisha kichwa hivi hivi, akabeba Crimea, wakamsifia sana kwamba Putin ni mtu wa kuogopwa.wazungu huanza kutengeneza mapicha kama haya hili muda unapofika mtu ale kisago cha usawa wake , hata Gadaf walimpamba hv hv na Sadam pia walimpamba...
Putin akajiona ni kweli wanamuogopa, akataka aivamie Ukraine, akatoa mkwara mazito kwamba atakayesaidia Ukraine atakutana na mkono mzito wa Russia, alisema hivyo akiamini hakuna atakayekubali kuisaidia Ukraine, asijue ya kwamba wenzie ndo wanammezesha ndoano.
Licha ya mikwara na sifa zote ambazo walimpa, haohao wazungu bila kificho ndio wanapeleka misaada Ukraine kurefusha vita na Putin amekaa kimya hana la kuwafanya.