Iran Yatangaza Maofisa Wake Wawili Kuuawa na Mashambulizi ya Israel

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Juzi Iran iliishambulia Israel ikidai ni kutokana na kitendo cha Israel kuendelea Kuwashambulia Hezbollah huko Lebanon.

Baada ya shambulio la Iran nchini Israel, Rais Trump alimsihi Netanyahu asijibu mashambulizi ili mazungumzo ya kumaliza vita yasiharibike. Lakini Israel iliishambulia Iran, ndani ya mji mkuu wa Tehran, ikiteketeza majengo pamoja na kiwanda cha kemikali za kutengenezea makombora.

Baadaye Iran ikatangaza kusimamisha mashambulizi dhidi ya Israel, lakini ikatoa angalizo kuwa inaweza kuishambulia Israel kama Israel itaendelea kuwashambulia Hezbollah huko Lebanon.

Israel nayo ikatangaza kusimamisha mashambulizi nchini Iran, lakini ikasema kuwa hakuna wa kuizuia isiwashambulie Hezbollah, na kwamba kama Iran itaishambulia, basi itayajibu mashambulizi hayo kwa nguvu zaidi ya ilivyofanya hapo jana.

Israel kama ilivyotamka, imewashambulia Hezbollah usiku wa jana na mchana wa leo.

Na mchana huu, Iran imetangaza kuwa zaidi ya uharibifu wa kiwanda cha kemikali na majengo, lakini Israel iliwaua pia maofisa wake wawili wa jeshi la Iran waliokuwa wakipambana kujaribu kuzuia mabomu ya Israel.

Televisheni ya taifa ya Iran ikaripoti kuwa wanajeshi wawili wa kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la nchi hiyo waliuawa katika mashambulizi ya Israel yaliyofanyika jana.

Soma Pia: Kundi la Hezbollah ladaiwa kuanza mashambulizi dhidi ya kambi za jeshi la Israel baada ya Iran kusitisha mapigano

“Mashujaa hawa wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi walipata shahada wakiwa wanatekeleza jukumu lao la kulinda anga ya taifa dhidi ya uchokozi wa jana wa utawala wa Kizayuni,” televisheni hiyo ya taifa ilisema.

JAMBO LA KUJIULIZA:
Kwa nini Iran isiachane na hao Hezbollah ambao hata Serikali ya Lebanon imetamka kuwa haiwataki?
==============
Iranian state television says at least two members of the army’s air defense force were killed in Israeli strikes yesterday.

“These esteemed martyrs of the Army Air Defense Force attained martyrdom while carrying out their mission of defending the country’s skies during yesterday’s aggression by the Zionist regime,” state television says.
 
bado wanaendelea kuua wa ayatollah? Kwani wamebaki wangapi? Ila Iran...wakati siungi mkono kuuwawa kwa hao wanaowaita mashahidi, nawashangaa kuruhusu kula TIGO 🤣 🤣 🤣 🤣 . I mean hawa mashia hawa🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ukiona Iran imekiri watu 2 ukweli ni 200 ndiyo waliouwawa!!!
 
Na hili ndio lilikuwa swali langu,
Vipi Israel hakuna aliyekufa au hata kujeruhiwa?

Hakuna aliyeuawa wala kuumia. Hata wanahabari waliopo Telaviv walisema kuwa walisikia ving'ora vilivyoashiria ujio wa mabomu, lakini makombora ya ulinzi wa anga yaliyadungua yakiwa angani kabla ya kuingia maeneo ya makazi. Na mawili yaliingiliwa mifumo yake, yakaenda kudondokea porini jangwani.
 
Kama kweli wamekufa je? Au mtasema ni AI
 
Bibi anapenda kujiamulia mambo, wazayuni hawajawai kulala nadeni
 
bado wanaendelea kuua wa ayatollah? Kwani wamebaki wangapi? Ila Iran...wakati siungi mkono kuuwawa kwa hao wanaowaita mashahidi, nawashangaa kuruhusu kula TIGO 🤣 🤣 🤣 🤣 . I mean hawa mashia hawa🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hayanaga akili hayo magaidi
 
bado wanaendelea kuua wa ayatollah? Kwani wamebaki wangapi? Ila Iran...wakati siungi mkono kuuwawa kwa hao wanaowaita mashahidi, nawashangaa kuruhusu kula TIGO 🤣 🤣 🤣 🤣 . I mean hawa mashia hawa🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Wameruhusu wapi na lini? Hao Israel ndio wamehalalisha ndoa za jinsia moja na kula jicho mwanamke sio kosa la jinai.
 
Hakuna aliyeuawa wala kuumia. Hata wanahabari waliopo Telaviv walisema kuwa walisikia ving'ora vilivyoashiria ujio wa mabomu, lakini makombora ya ulinzi wa anga yaliyadungua yakiwa angani kabla ya kuingia maeneo ya makazi. Na mawili yaliingiliwa mifumo yake, yakaenda kudondokea porini jangwani.
Taarifa umeitoa wapi? Media censorship ni kubwa Israel hata yule muingereza alivyorekodi kombora la Iran alikamatwa. Na so far Israel imeua waandishi wa habari sio chini ya 200 tokea vita imeanza sababu tu walikua na kiherehere cha kuripoti uharibifu na vifo.
 
Ulivyo mjinga na mpumbavu umeona uingize Ushoga wako ili kuficha tu kuuwawa kwa Askari wa Iran na majeshi ya Israel!!!!

Na Kama Magaidi wa Iran Wametangaza Askari wao 2 wameuwawa walivyo waongo basi wewe ongeza zero mbili ili isomeke 200. Maana kwa kipondo hicho hawawezi kufa Askari wawili tu!!!

Na wewe Uache kujifariji kwa kuleta maneno ya Ushoga ili tu kuficha kipondo alichopigwa kutoka kwa wana wa Israel
 
Back
Top Bottom