Iran yatoa Masharti, wakati Trump akidai kusitishwa kwa mapigano

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi, ameweka ujumbe hivi karibuni kwenye mtandao wa X akisema kwamba ikiwa Israel itaacha "uchokozi usio halali" Iran "haina nia ya kuendelea kujibu".

Araghchi alisema Israel lazima isitishe mapigano ifikapo 04:00 saa za eneo, ambayo imepita:

"Kama Iran ambavyo imerudia kusema wazi: Israel ndio ilianzisha vita dhidi ya Iran, na si kinyume chake.

"Hadi kufikia sasa hakuna "makubaliano" juu ya usitishaji vita au operesheni za kijeshi. Hata hivyo, ili mradi utawala wa Israel utasitisha uchokozi wake usio halali dhidi ya watu wa Iran kabla ya saa kumi asubuhi kwa saa za Tehran, hatuna nia ya kuendelea kumjibu.

"Uamuzi wa mwisho juu ya kusitishwa kwa operesheni zetu za kijeshi utatolewa baadaye.

Awali, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza usitishaji "kabisa" wa mapigano kati ya Israel na Iran kwenye mitandao ya kijamii.

Trump alisema usitishaji mapigano utaanza "katika takriban saa sita kutoka sasa" baada ya kila nchi "kupunguza" operesheni zao za kijeshi.

Tangazo la Trump ni njia anayotumia mara kwa mara kupunguza uhasama lakini aliongeza kwamba "ndani ya saa 24" vita vitamalizika rasmi.

Israel na Iran bado hazijathibitisha kufikiwa kwa usitishaji mapigano.
 
Ndio unaamika usingizini wakati vita ishaisha kitambo, si usome tu news kuliko kuanzisha nyuzi za habari zilizokwisha changiwa hadi ikatosha.
 
Vita vimeisha na Iran tayar wameshafanya sherehe ya kushangilia Ushindi dhidi ya Adui wao Israel
 
Labda ushindi wa kupiga majengo matupu huko😂😂 wakati huo moyoni wanavuja damu na kulia kilio kichungu cha kupigwa na kanchi kama mkoa wa Dar es salaam wakati waliwaaminisha kobazi wenzie kwamba wao ndio taifa lenye nguvu middle east 😂😂 huku wakiwa na msiba mzito wa wakuu wao wa jeshi na wanasayansi wa nyuklia huku wakiwa hawana tena vinu vya nyuklia walivyo vijenga makumi ya miaka kwa mbwembwe na bashasha mpaka kina Amina ndala ndefu wa uwanja wa fisi,kwa bonyokwa, river side,kitambaa cheupe wanajua jamaa wana nyuklia tayari kumbe puto tu ndani ushuzi mtupu na tumekuja kujua baada ya kupigwa sindano ndio ikawa mwisho wa mbwembwe za miaka kenda huko 😂😂
 
Back
Top Bottom