Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Iran ni Washia wanalengo za kuzifanya nchi zote za Middle East maskini na failed states Kama Yemen, Syria, Iraq na Lebanon
Kama ni Shia hawa Sunni kwa nini wasingefanya kama anachokifanya Shia ili kuleta huo mustakabali mzuri unaouona wewe?
 
Hana uwezo wa kuwapangia watu cha kufanya kama ambavyo yeye hataki kupangiwa.
 
Kama ni Shia hawa Sunni kwa nini wasingefanya kama anachokifanya Shia ili kuleta huo mustakabali mzuri unaouona wewe?
Lengo kuu la Mapinduzi ya Iran ni kuyahamishia kwenye nchi zote zenye Ufalme.

Baada ya kuhamisha ni kuzifanya hizo Nchi ziongozwe na Washia wenzao.

Saudia, UAE, Oman, Jordan na mataifa mengine ya Kisunni hayawezi kufanya jambo litakalo ipa nguvu Iran ambayo imeapa kuziangusha.

Saudi Arabia Iko tayari kuwasaidia Wapalestina ila sio kupitia Hamas.

Hezbollah mnayoisifia nchini Saudia inatambulika kama Kundi la Kigaidi, sababu Moja wapo ni matukio kadhaa waliyofanya dhidi ya Saudia.

Hezbollah Ndio ilikuwa inatoa Mafunzo kwa Wahouthi namna ya Kurusha Drones zilizokuwa zinalipua Matank ya Mafuta Saudi Arabia na Mashambulizi mengine, Nchi zote za Kiarabu zilikaa zikaifuta Syria kwenye umoja wa Kiarabu na kumtaka Assad aache kuua Wasyria wenzake badala yake wakae mezani, Hezbollah Ndio Waarabu pekee yao walio kataa na kuendelea kuua Wasyria na kunyang'anya Maeneo ya Wasunni huko Syria.
 
Wakati unaandika huu utumbo kuna nchi za kisunni kama Qatar na Oman zimeikaribisha Iran na zimekubaliana nayo kufanya biashara.
Unajua Saudi Arabia kuna propaganda inazieneza kwa kutumia madhheb ya Salafi kuhusu Iran na kinachoendelea ME.

Baada ya Iraq kuparaganyika Saudi Arabia anataka ukiranja mkuu wa waarabu wote hapo ME.

Tatizo la Saudi Arabia hana nguvu ya kijeshi, basi angalau ingelikuwa kwenye diplomasia kama Qatar inavyopambana kuweka mambo sawa Saudi Arabia yeye hashighuliki kabisa. Angalau angelikuwa anaongea ingeliwajaza nguvu wenzake.

Hii hatua kaichukua Iran kwa Saudi Arabia kwake hii ni bahati mbaya na anaona jinsi waarabu wengineo wanashawishika na ushawishi wa Iran kitu ambacho kwake ni hatari anaona anapoteza ukaka mkuu kwa waarabu wenzake.

Vurugu zote zinazotokea ni hapo ME Saudi Arabia na Uran ni kugombea ukiranja mkuu hapo ME.
 
Hamas ni Sunni au Shia ?
 
Kiongozi, mimi najua kinachoendelea ME kuliko wewe.

Mimi ni sunni na nina ndugu Yemen ambao ni sunni.

Najua kilichotokea Yemen kwa undani kuliko wewe.

Najua kinachoendelea Syria kuliko wewe. Sheikh Muhammad Al Hudaa Al Yaaqoubi msimamo wa kwanza alidhani kama wewe ambaye ni Sunni. Baadaye alibadilisha msimamo wake.

Sheikh Said Ramadhan Al Bouti ni mwanawazuoni mkubwa sana wa kisunni. Kauliwa na hao hao Isis ambao Saudi Arabia alikuwa aki fund operation zao kisa Sheikh Al Bouti aligundua hila zao na kuwa pamoja na Bashar Al Assad.

Tena aliuliwa ndani ya msikiti na bomu la kutegwa. Alikufa yeye pamoja na mjuu wake na watu wengine 42 na 84 wakiwa maeruhi.

Katika haya uliyoandika huwezi kuniongopea hata nukta.

Saudi Arabia walishaiuza Palestina kitambo na miaka ya nyuma kama siyo 2003 au 2005 mwakilishi wa Saudi Arabia alizomewa na wapelestina na wengine kumtaka aondoke. Mohammad Bin Suleyman alivyokuwa crown prince aliwataka wa Palestina wakubaliana na matakwa ya Israel kabla hata hii vita yao ya oktoba kuanza.

Sijisikii kuandika sana naishia hapa!
 
Tatizo ni Iran au Saudia ?

Unataka Saudia awasaidie Palestine kupitia nini ? Kama tu kashindwa kuungana na Sunni wenzake kuwasaidia Wapalestina kitu ambacho hata Shia kamshinda.

Hivi unafahamu kuwa Saudia ipo katika mchakato wa kufanya normalisation na Israel ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…