Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Hakuna ulazima wa Kuisaidia Palestina, hili lazima kila mtu alijue... Kama Wapalestina wanataka Msaada wa mtu lazima wasikilize Masharti ya mtu wanayemuomba msaada.

Hili jambo Watu wengi mnaliruka sana
 
Kituo kinachofuata baada ya Beirut ni Tehran
Nyonzo bin mvule njoo umuone mlokole uliyesema anatokea kanisa la mabati lenye viti vya bar anavyobwabwaja huku.

Yaani nyie watu mmeaminishwa ujinga vibaya sana. Israel huyu huyu aliyetwangwa mara mbili ndani ya ardhi yake ndiyo awe na uwezo wa kuishambulia Iran?

Iran ndiye mbabe wa kweli mashariki ya kati achana na fiksi za wachungaji uchwara. Fungua ubongo.
 
naunga mkono hili onyo...haswa hao saudia wakijikoroga tu warudishwe kwenye jangwa km zamani
 

Walishakaririshwa hawa watu, daima wako upande wa wasio waislamu, isipokua baadhi wenye kujitambua, hata Qur'an imeshawazungumzia hawa watu, hawatakua radhi nasi mayahudi na Manaswara mpaka tufuate mila zao
 
Kituo kinachofuata baada ya Beir Tehran
Dah! hao watu noma sana, labda ukiandika watakusoma wakiwa wenyewe majumbani mwao. Iakini ukikutana nao mahala hawasikilizi hoja wala kioja wanaongea wao tu huku wamefumba macho.hawajali kama unawaelewa au la!(wanatumia ile mbinu ya ukitaka kumuua Nyani usimuangalie usoni.
 
Vipi mkuu tukalime viazi? Haya mambo waachie waajemi, wale wanatengeneza nucleur, wewe hata njiti ya kiberiti huwezi halafu unawasema! Are you serious?
Haha,
Ninaowasema ni hawa chawa wa waajemi wa humu jF waliojichimbia huko Buza kwa Mpalange badala ya kwenda front wakalipuliwe
 
Iran anatafuta mtu wa kufanya naye, anajua kilichoko mbele yake siyo kizuri, mbele haoni mwanga anaona giza, ametengeneza mazingira zaidi ya Sadamu Huseni, USA na Israel hawezi kuacha adui atamalaki na kutishia maslahi ya USA na kulifuta taifa la Israel,
 
Kama sikosei Saudia,Jordan,Bahran,Kuwait,Oman,Falme za Kiarabu,baadhi ya hizo zina mikataba ya Ulinzi na US nyingine na Israel(Azerbaijan)
Baadhi ya hizo zina Military Bases za US.
Sijui itakuwaje!
Iran isipoangalia inatafutwa kwa mfano wa sababu zile zile zilizotumika kuipiga Iraq (Saddam)!
 
Mkuu kwani kwa sasahivi wapalestina wanataka nini na terms zao zipoje
 
Hii kuna clip moja ya historia nilicheki wanasema saddam walimuongopea ili aingie kingi


View: https://youtu.be/hxW_Oe-76no?si=rgpRD6kk0j3h8TRH
 
Hawa watu ni tatizo sijui kww nini mtu akishaasoma biblia aya 2 basi ruksa kufungua kanisa
Kwa bahati mbaya sana vibali vya kufungua makanisa hivitolewi na masjid yoyote.
 
Iran na Saudi Arabia kwa sasa wamerudisha uhusiano uliokuwa umelega lega kwa zaidi ya miaka 20 na ubalozi umerejeshwa kwa nchi zote 2
Kwa taarifa yako uelewe kwamba Israel ni muhimu kwa Saudi Arabia kuliko Iran na Saudi Arabia anaelewa kwamba Wairan ni makafiri tu.
 
Kwa taarifa yako uelewe kwamba Israel ni muhimu kwa Saudi Arabia kuliko Iran na Saudi Arabia anaelewa kwamba Wairan ni makafiri tu.
Ki namna gani
 
Wakati unaandika huu utumbo kuna nchi za kisunni kama Qatar na Oman zimeikaribisha Iran na zimekubaliana nayo kufanya biashara.
Hizo ni porojo tu za masjid ubwabwa, hata siku moja wasunni hawawezi kuelewana na washia wanaoamini ni makafiri tu kama makafiri wengine.
 
Hapo ndio mwisho wa Israel na mwenyewe anajua hilo. Si umeona mpaka sasa kimya tangu apigwe kipigo kitakatifu tarehe 1 oktoba.
Soon tutasikia free Iran.

Mwanzo watu walidai Hezbula ni kiboko ya Isarel mwaka 2006 alikimbia, wakadai anawaonea Gaza. Sasa Hezbu wanaomba poo (pause) bila masharti ya kuihusisha Gaza huku mtarajiwa wa mrithi na mtarajiwa wa mrithi wa mrithi wakiungana na mrithiwa.

Yeye Iran anasema akipiga mkwara kwa nguvu zake hajui kimo cha nguvu za wengine.

Kikubwa ameyavulia nguo. Kitajulikana na uwanja wa vita utaamua, na hii inaweza ikawa jumlajumla maana mlengwa hapo ni Ayatollah.

Nakumbuka Iraq alitoa mkwara kama huo, mwisho wa siku ndio hivo tena.

Bila Urusi kuwa bize, ingekuwa ngumu kumpiga Iran, kama ilivyokuwa Syria. Sasa Urusi yupo bize na yake, yafaa sasa kulianzisha na huyu Iran.
 
Hao warabu wajinga sana wanaweza hata kwenda na wao kushambulia Iran wanacho ambiwa na US wanakubali.

Lakini na uhakika 💯 atazipiga kweli hizo nchi tatu vibaya sana wakishiriki kwa njia moja au ingine..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…