Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

It's time all Sunni Arab states united against their common enemy, the Shia terrorist state and the head of the 🐍 @khamenei_ir IRGC regime to help Israel get the job done to dismantle and replace the regime to enable peace to prevail in the middle east...
Wakati unaandika huu utumbo kuna nchi za kisunni kama Qatar na Oman zimeikaribisha Iran na zimekubaliana nayo kufanya biashara.
 
Iran anajua kuwa kwenye vita na USA Shah watarudi madarakani
Iran sio nyepesi kama unavyodhani.
Kama ingekua nyepesi ingeshavunjwa utawala wake miaka ile ya 1980s ikiwa bado nchi dhaifu.
Ila sasa ishakita mizizi no way unaweza iangusha Iran.
Hao USA wenyewe wanajua sio rahisi ndio maana kila siku wanaishia kutishia tu.
Unaizungumzia nchi iliyopigana vita miaka nane consecutively.
 
Kwa bahati mbaya sana viongozi wa nchi nyingi za Waarabu ni wale tunaowaita wanafiki na wamewekwa kwenye mamlaka yao na USA ikisapotiwa na Israel. Yani hapo Jordan, Saudi, Misri, UAE etc zote viongozi wao ni vibaraka wa USA na Israel na ndio maana huoni hata wakikemea dhuluma ya Israel dhidi ya Palestina.

Hawa viongozi wao wanachojali ni maslahi yao tu hawajali chochote wala hawapo hapo kuwatetea wanaoonewa, infact wenyewe wanawaonea wananchi wao na katika hizo nchi hakuna demokrasia na hakuna uchaguzi. Lakini kamwe huwezi kusikia USA au UN wanasema hao viongozi kuwa ni madikteta. Kwa dunia ya leo Dikteta ni kiongozi ambaye hataki kufata masharti ya USA mfano Saddam na Gadafi au Mugabe lakini wanaotii kamwe sio madikteta.

Hawa viongozi waliowekwa na USA na Israel wanahakikisha wanalinda maslahi ya waliowaweka vinginevyo wanapinduliwa, na wote wanalindwa na USA na Israel. Na hawataweza kwenda kinyume na makubaliano yao na mabwana zao otherwise watakuwa eliminated. Hawa wameuza ubinadamu wao kwa mali na vyeo

Kwa hivyo ni ngumu sana hawa viongozi kubadilika labda kama yatatokea mageuzi kwenye nchi zao waondolewe madarakani. Na sisi tunaombea hilo na ninaamini ipo siku wataondoka na kupatikana viongozi wema na hapo ndio utakuwa mwisho wa Israhell.
 
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.

Iran imechukua msimamo mkali dhidi ya majirani zake baada ya kutoa onyo kali kuhusu ushirikiano wowote na Israel kwa ajili ya operesheni za kijeshi.

Msimamo huu mkali ni sehemu ya mkakati wa Iran kuzuia nchi za kiarabu kushirikiana Israel. Maafisa wa Iran wamesisitiza umuhimu wa "umoja wa kikanda" kukabiliana na kile wanachokiona kama tishio kutoka Israel, huku wakieleza pia umuhimu wa kudumisha utulivu huko Mashariki ya Kati

Soma pia: Israel kuishambulia Iran leo usiku, Marekani yaja juu

Onyo hilo halihusishi tu matumizi ya anga, lakini pia Iran inafuatilia kwa karibu uwezekano wa ushirikiano wa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Gulf

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, msimamo wa Iran uliwekwa wazi wakati wa mkutano wa hivi karibuni huko Doha.

Ujumbe ulikuwa wazi: taifa lolote la Gulf States litakaloruhusu anga yake au vituo vyake vya kijeshi kutumika kwa operesheni dhidi ya Iran litakabiliwa na kisasi.

Tehran inachukulia vitendo hivyo kama uamuzi wa pamoja wa mataifa yote ya Gulf, jambo ambalo linaweza kupanua wigo wa majibu yake.

Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .

Yaani yeye iran ametumia anga la saudia iraq, jordan, misri kuishambulia israel na mabalstic yake halafu israel asitumie anga yeyote huu ni upuuzi?
 
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.

Iran imechukua msimamo mkali dhidi ya majirani zake baada ya kutoa onyo kali kuhusu ushirikiano wowote na Israel kwa ajili ya operesheni za kijeshi.

Msimamo huu mkali ni sehemu ya mkakati wa Iran kuzuia nchi za kiarabu kushirikiana Israel. Maafisa wa Iran wamesisitiza umuhimu wa "umoja wa kikanda" kukabiliana na kile wanachokiona kama tishio kutoka Israel, huku wakieleza pia umuhimu wa kudumisha utulivu huko Mashariki ya Kati

Soma pia: Israel kuishambulia Iran leo usiku, Marekani yaja juu

Onyo hilo halihusishi tu matumizi ya anga, lakini pia Iran inafuatilia kwa karibu uwezekano wa ushirikiano wa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Gulf

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, msimamo wa Iran uliwekwa wazi wakati wa mkutano wa hivi karibuni huko Doha.

Ujumbe ulikuwa wazi: taifa lolote la Gulf States litakaloruhusu anga yake au vituo vyake vya kijeshi kutumika kwa operesheni dhidi ya Iran litakabiliwa na kisasi.

Tehran inachukulia vitendo hivyo kama uamuzi wa pamoja wa mataifa yote ya Gulf, jambo ambalo linaweza kupanua wigo wa majibu yake.

Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .

Ameshajiona ndio kiranja wa wavaa kobazi wote ?
 
Wakati unaandika huu utumbo kuna nchi za kisunni kama Qatar na Oman zimeikaribisha Iran na zimekubaliana nayo kufanya biashara.
Yani itanatia aibu sana mkuu kuona jinsi graduates wa Tanzania walivyoweupe upstairs, haswa katika mambo madogo kama haya. The problem is vijana hawana utamaduni wa kujisomea. Wao wakishamaliza shule, ni mpira, umbea, na kubeti. Mtu hata anashindwa kujua simple facts!.
 
Yaani wao Iran watumie anga za wengine kurusha makombora kwenda Israel, ila Israel isitumie hizo hizo anga kulipiza? Upuuzi huo
Habari haisemi Israel kutumia anga bali inasema Marekani kutumia anga.

Tafsiri yake ni kwamba hizo Gulf states kuna kambi nyingi za kijeshi za Marekani.

Alupo Israel na Amerika yupo! Iran asisitiza ikiwa hizo nchi zikaruhusu kambi za kijeshi za Marekani zitumike kumpiginia Israel dhidi yake naye atarudisha mapigo ndani ya hizo nchi.

Ikiwa Marekani inataka kumsaidia Israel imsaidie moja kwa moja kutokea nchini kwake.
 
Sasa mbona anahangaika yeye SI anajidai ni supapawa la kiarabu akae kwa kutulia tu.
 
Yani itanatia aibu sana mkuu kuona jinsi graduates wa Tanzania walivyoweupe upstairs, haswa katika mambo madogo kama haya. The problem is vijana hawana utamaduni wa kujisomea. Wao wakishamaliza shule, ni mpira, umbea, na kubeti. Mtu hata anashindwa kujua simple facts!.
Yani wanachukulia mambo rahisi rahisi hivyo.
Hao licha ya kutofautiana madhehebu ila ni ndugu ikifika kipindi cha Hijjah wote wanakutana sehemu moja Mecca na Medina.
Sasa haiwezekani wewe wa nje uje uwaletee ugomvi wa kudumu halafu wakuangalie tu na wakutii miaka yote.
 
Taarifa zilitoka mkuu katika vyombo vya habari tofauti na hasara ilitangazwa.
Sawa Saudi Arabia hakuacha kuzalisha mafuta,ila ikubalike hasara ya billions of dollars ilipatikanika.
Na hayo mashambulizi ndio yaliyochagiza Saudi Arabia kuondoa vikosi vyake Yemeni na kukubali kukaa mezani kumaliza uhasama na Houthi.
*Unakizungumziaje kinachoendelea Baab Al mandib!?
Je Iran ikiamua kufanya hivyo na strait of Hormuz!?
Usilete general implication mkuu.
Kila mtu ameona kinachojiri red sea kwa washirika wanaomsaidia Israel.
Hasara to which levels? Iran wali declare kuwa wanahusika na hizo attack?

A perfect attack ni kumuumiza adui asiweze kuendelea na operation zake. But then saudi ndio wana uchumi mkubwa kuliko iran, probably wana jeshi bora sasa kuliko nyuma

Tunarudi pale pale iran hamna kitu atafanya ni biti tu for nothing
 
Back
Top Bottom