Irani na Israeli wana Undugu usioyumba, Makombora 300 ya Irani naona kama ni Propaganda

Irani na Israeli wana Undugu usioyumba, Makombora 300 ya Irani naona kama ni Propaganda

Acheni kuandika vitu msivyovijua, hiyo Israel iliyopo sasa pale mashariki ya kati sio Israel iliyokuwepo hapo kale ilioandikwa katika vitabu vya dini kama Biblia na Quran.

Israel iliyopo sasa ni sinagogi la shetani au khazarian Tribe.

Hao wanaojiita waisrael waliopo mashariki ya kati ni mazayuni yanayoandaa mazingira ya mpinga kristo wakishirikiana uingereza(6), marekani(6) na hao mazayuni(6) wenyewe waliopo sasa hapo mashariki ya kati.

Tafuta historia ya khazarian Tribe (Ashkenazi Jews) utaelewa hasa chanzo chao na mission zao hapa duniani.
Kwa hiyo hao WanaIsrael wa kipindi kile walienda wapi kama waliopo asili Yao sio Ile?
 
Maswali unayouliza ni ya kitoto halafu yanaonesha unauelewa mdogo ila unaigiza ujuaji.
Kila la kheri
Sawa we mkubwa baki na uelewa wako finyu. Ungetakiwa pia unijibu Israel ina raia pia Druze na samaratin na mabedui so hao unawazungumziaje
 
Umeeleza historia za bc na ac, zilizopendwa.
Taifa la Israel hadi sasa limeshapigana na kila nchi zinazoizunguka. Ameshapigana na wairan zaidi ya mara 3. Kila baada ya miaka 4 lazima atwangane na jiran yake. Jana hata jiran mmoja wanayependana nae, kwasababu muisrael anajiamini yeye ndiye taifa teule na muhimu kuliko yeyote duniani. Kama kupigana na Iran, kitawaka tu. Sio Iran pekee, bali nnchi zote zinazoizunguka Israel patachimbika.

Ushahidi List of wars involving Israel - Wikipedia
Hayo ndio mnasikilizaga mazinge aliwadanganya ndio unatuletea sisi ugoro huu?
 
unaijua dron anazo tumia Rusia nani kamfundisha tengeneza na nani anamuuzia hizo 300 ni robo ya robo ya makombora yote
 
Acheni kuandika vitu msivyovijua, hiyo Israel iliyopo sasa pale mashariki ya kati sio Israel iliyokuwepo hapo kale ilioandikwa katika vitabu vya dini kama Biblia na Quran.

Israel iliyopo sasa ni sinagogi la shetani au khazarian Tribe.

Hao wanaojiita waisrael waliopo mashariki ya kati ni mazayuni yanayoandaa mazingira ya mpinga kristo wakishirikiana uingereza(6), marekani(6) na hao mazayuni(6) wenyewe waliopo sasa hapo mashariki ya kati.

Tafuta historia ya khazarian Tribe (Ashkenazi Jews) utaelewa hasa chanzo chao na mission zao hapa duniani.
Hujui hata biblia walitabiriwa na yeremia na ezekiel wataenda ulaya kama watumwa ila watarudi kwenye nchi yao
 
Sawa we mkubwa baki na uelewa wako finyu. Ungetakiwa pia unijibu Israel ina raia pia Druze na samaratin na mabedui so hao unawazungumziaje
Kama Kuna kitu haukielewi niulize nikujibu, hizo habari unazouliza za kuokoteza hazitakujenga,
Hao unaotaja ni aina ya jamii zilozotawala Israel kwa miaka tofauti na zipo jamii nyingi kabla ya hata hawa wapalestina, Ottoman (waturuki) n.k waliokalia Israel kabla
 
Acha uongo bwana ottoman imekuja tu juzi
Israel ipo tokea kipindi cha kina jacob mtoto wa isaka ambaye baba yake ni ibrahimi

Israel wana kabila 12 kipimo cha dna kinasema waisrael hata kama anaishi russia dna zao zina match
 
Kama Kuna kitu haukielewi niulize nikujibu, hizo habari unazouliza za kuokoteza hazitakujenga,
Hao unaotaja ni aina ya jamii zilozotawala Israel kwa miaka tofauti na zipo jamii nyingi kabla ya hata hawa wapalestina, Ottoman (waturuki) n.k waliokalia Israel kabla
Nadhan hujanielewa. Nachosema ukiacha hao Jews wapo Samaritan kuna Druze na bedui na hawa nao walikuwa weusi au nao waliletwa na uingereza. Bahati nzur hayo maeneo nimefika san sio mara moja so nilichokuwa nataka wewe unifafanulie ni hao waisraeli halisia wako wapi muda huu na hii lugha ya Hebrew inayoongelewa pale Israel hawa waleo wameipata wapi? Twende taratibu mjomba tueleweshane.
 
Pointi ndiyo ipo hapo. Sijui kwa nini wachambuzi hawataki kufukunyua habari na kuzitafakari! Iran alikuwa anatuma ujumbe tu na siyo kuanzisha vita kamili.

Hivi watu walitaka Iran arushe makombora yenye madhara Israel si vita vingezuka pale Mashariki ya Kati, na sababu ya kuzua vita vikubwa ili iweje?

Iran karusha makombora na drone zaidi ya 300! Hata kama zimedunguliwa, lakini zimekosesha utulivu nchini Israel, mfano watoto walishindwa kulala usiku kucha, je, huo siyo ujumbe tosha kutoka Iran? Hivi unaweza kupata utulivu huku angani kuna milio ya droni na makombora ya kutungua ndege?
 
Nimewaza Vita ya Irani na Israeli na Kituko cha Mizinga 300 kutoleta Athari Kwenye Ardhi ya Israeli.

Inawezekanaje Siraha hevy za moto zaidi ya 300? Sio kwamba Irani na Israel wana lao moja?

Hawa Wayahudi na Waajemi wan Undugu wa Kiroho Tangu zamani.

Nikurudishe nyuma kidogo.

Mambo mema ambayo Irani (Waajemi) waliwatendea Wayahudi hapo zamani za kale.

1. Wayahudi walipokuwa wametekwa ndani ya Babeli chini ya Nebkadineza na baadae Mwanaye Belshaza walipata nafuu ya Utumwa kwa Mfalme Koreshi Mwajemi kuiangusha Babeli.

2. Baada ya Koreshi alishika madaraka Mfalme wa Uajemi King Darius( Dario) huyu Mwamba aliandika nyaraka Ikulu akaifadhi ikieleza kuwa baada ya kipindi cha miaka fulani wayahudi waachiwe warudi kwao Yesrusalem kuujenga mji wao uliobomorewa na Nebkadneza miaka 600BC.

3. Tukio lingine ni lile la Mfalme Dario kuwaua Mawaziri na Baraza loote la maliwali alipogundua kuwa walimdanganya kwamba Daniel alikuwa Mhaini asiyetii sheria za Uajemi ambazo zilikuwa Infaliable( yaani hazitenguki). Maliwali walikula kibano cha kufa mtu wao na watoto wao na wake zao wakatupwa kwenye shimbo la Simba zikawasasambua asibaki hata mmoja. Wakati huo Daniel akiwa ndiye Waziri Mkuu Uajemi( imagine Mkimbizi tu)

4. Baada ya Mfalme Dario aliingia Ahasuero, huyu Mwamba alikuta nakala ya Barua iliyoandikwa na kuagiza Wayahudi waruhusiwe kurudi kwao na akatekeleza. Ahasuero akampa barua ya Ruhusa Ezra akiwa na wenzake akina Yoshua, Hagai Nabii, Modekai, Delaya na Zerubabeli wakaenda kuanza ujenzi. Kitu kikubwa ktk Ruhusa hii ni kwamba Ahasuero aliagiza maliwali waliokuwa pande za Siria na Jordani na ng'ambo ya Mto(West Bank) wahakikishe Waisraeli hawasumbuliwi. Soma Kitabu cha Ezra, 1,2 hadi sura ya 6. Mfalme anaagiza ikiwa watapungukia basi wakuu wa mikoa inayozunguka israeli wahakikishe wanachukua sehemu ya Kodi wawahudumie wayahudi wasipate tabu.

5. Kule Jordan wakajitokeza wabishi akina Sanbalati, Tobia, Geshem Mwarabu kutaka kuleta bugudha na kejeli wakadhibitiwa na Waajemi.

6. Baada ya Ahasuero alifata Mfalme Atashasta kipindi cha Nabii Nehemia, mwendo ukawa ule ule. Katika mwaka wa 20 wa kutawala kwake Atashasta Kamanda wa Jeshi na Intelijensia Hamani akazinyaka taarifa kwamba Kuna Wayahudi hawataki kuitii serikali na mamlaka ya Uajemi( kosa la uhaini). Waliotuhumiwa ni akina Modekai na wayahudi woote(wakimbizi). Kwa kujipendekeza Kamanda Hamani akapanga kuwaua wayahudi wote akianza kumtundika Juu ya Mti Modekai ili washenzi wengine wajifunze. Lahaulaa! Kibao kikageuka Hamani akatundikwa Yeye na Wayahudi hawakufanywa kitu. Walaka uliotolewa kwa maliwali wote na wakuu wa mikoa ukafutwa na wayahudi wasibudhudhiwe.

7. Basi Nehemia na kina Zerubabeli wakafunga msafara wa pili( second importation) wa kurudi kwao wakapewa ulinzi na pesa kutoka kwa Mfalme wa Uajemi.
Kwa hiyo kwa nyakati zote za uhai wa Israeli na Uajemi hawa watu wamekuwa ndugu. Sio undugu wa kikabila bali wa kiroho.

Unaposikia Kuna Mizinga na drone za kibabe 300 zimepiga na hakuna madhara yoyote yaliyotokea usishangae ktk Ulimwengu huu wa Propaganda.
Zimeanza kuvuma kuwa lile shambulio lilikuwa bosheni tu
 
Nadhan hujanielewa. Nachosema ukiacha hao Jews wapo Samaritan kuna Druze na bedui na hawa nao walikuwa weusi au nao waliletwa na uingereza. Bahati nzur hayo maeneo nimefika san sio mara moja so nilichokuwa nataka wewe unifafanulie ni hao waisraeli halisia wako wapi muda huu na hii lugha ya Hebrew inayoongelewa pale Israel hawa waleo wameipata wapi? Twende taratibu mjomba tueleweshane.
Ni kweli mkuu nimeenda Jerusalem nimekutana na watu weusi tii pale kanisa la Sculpture
 
Ni kweli mkuu nimeenda Jerusalem nimekutana na watu weusi tii pale kanisa la Sculpture
Wapo weusi tii coz hata Jerusalem yenyewe wapo migrate wa kinaigeria wengi tu wapo miaka. Nilitaka yeye anisaidie ufafanuz tu.
 
Hawa jamaa akili zao huwa wanajua wenyewe Karakana wanakozipitishia.
Ngoja wasubiri wenzao wanaporusha Makombora wawaonyeshe huwa inatakiwa iweje.
Ila kama kuna imani au kuna kitu wanakiamini hawa jamaa, basi sharti lao kubwa ni kujakikisha hautumii akili zako katika hali na wakati wowote ule.
Ndiyo maana wameagizwa kuwa, ukienda kujisaidia haja hata ndogo ukikosa maji basi josafishe hata kwa mchanga au matope na wao wanatii.

Dah kuna baadhi ya taratibu na shwria zao mtu anaetumia common sense anaweza ku question.. sema ndo hivyo ni dhamb kuhoji
 
Hakuna kitu kama iko. Putin alirushiwa Makombora buku lakini hayakutua katika ardhi yake vipi na wao wanaundugu na Ukraine
 
Hayo makombors hakuna alyeyaona kati ya mimi na wewe zaidi ya zile movie za video zilizorushwa wala hazioneshi kama zinatoka irani na kama zinaenda Israeli hakuna anayeweza kusema

[emoji2955][emoji2955][emoji2955] so yale ya gaza uliyaona kutokea mahali yanayorushwa mpaka yalikofika..

Yaan una question integrity ya vituo vyote vya dunia nzima na technolgy zao kaka hebu kuwa serious .. kwa hiyo Unataka Kusema Hakuna
Kombora Zilizorushwa so Iran na Israel na washirika wake wametuongopea?

Na vyombo vyofe vya habar wakakubaliana..

Dunia hii ya sasa ambayo mtu anaweza akaiweka dunia kiganjan kwake akapata ukweli unahs kuwa hilo Shambulizi ni uongo
 
Tech ipi wote wamerusha video zinafanana kila kitu as if wamepangwa
 
Back
Top Bottom