The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 10,805
- 14,181
Mkuu katika tabia ambayo muislamu safi kama wewe tunatarajia awenayo ni uvumilivu na upendo kwa wasio waislamu ,Pombe ni haramu kwa mujibu wa quran ,Je kwa mujibu wa dini za asili za wachaga ni haramu pia ? Je waabudu milima nao kwao ni haramu ? Kiongozi tusipokuwa wavumilivu,itatokea siku dini itakuwa na kitabu chao kitachosema kuvaa kanzu nyeupe ni haramu ,hatuta wabishia tutawasihi wao wasivae ila waheshimu uislamu na waislamu .Unapoanza kuamini dini yako ndo standard sahihi na zawengine ni chini ya dini yako unaanzisha vita isiyo na mwisho wala faida ,Natumaini kama wewe muislamu wa kweli kwa nini utumie nguvu kubwa kupinga kitu haramu ,kwani mungu wako ni mdhaifu kiasi cha kuhitaji msaada wa mtu mdhaifu kama mimi na wewe.
Njia pekee ya kuupa uislamu heshima ,kwanza ni kuujua uislamu kwa undani ,kisha kuwahurumia na kuwapenda wasio waislamu ili kwa upendo wako na uvumilivu huenda wakavutiwa kujua mungu wako ni yupi na hatimaye nao wakaslimu.