KINGSLEE
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 830
- 1,046
Kumekuwa na Tabia mbaya sana kwa hawa watu kutunyanyasa pindi tunapokuwa safarin.
Sasa dawa yao ipo jikon.
Tutakomaa nao mpka kieleweke..
Kwa familia zilizokumbwa na Mkasa huu Tafadhal naomba Mnisamehe sana. Mungu Ibarik Tanzania Mungu Ibariki Africa.
=====
TAKUKURU Mkoa wa Iringa, imemkamata Askari wa Usalama barabarani Coplo Steven Philimoni Mchomvu akipokea Rushwa eneo la Ipogoro barabara ya Mbeya Iringa kutoka kwenye Magari majira ya Saa tano asubuhi tarehe 18/01/ 2022 na tayari alikuwa amekwisha fikisha Tsh laki moja na elfu hamsini na mbili.
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa Domina Mukama amesema taratibu zinaendelea ili kuweza kufikishwa mahakamani Askari huyo ambaye picha zake zilisambaa mtandaoni.
"Tulimkamata yule Askari, akiwa anapokea pesa toka kwenye Mabasi na Basi la Mwisho lilikuwa ni Basi la Abiria. Baada ya kumkamata, kama unavyoona zile picha kuna picha ya OCD, nilimpigia simu OCD akaja kwahiyo tukafanya kazi kwa kushirikiana TAKUKURU na Polisi. Zile pesa hatukuzikuta kwenye gari, tulimkagua kwenye mavazi yake na kuziweka kwenye gari". Amesema kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa Domina Mukama
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa amewata Askari na watumishi wote wa serikali waache mara moja tabia ya kutoa na kupokea rushwa kwa kuwa ni kinyume cha sheria za utumishi wa UMMA kama ambavyo walikula kiapo wanapoanza kazi.
Polisi huyo bado anashikiriwa na Jeshi la polisi mkoa wa Iringa na taratibu zote zikikamilika atapelekwa Mahakamani.
Pia soma: Polisi yatoa ufafanuzi kuhusu kusambaa kwa picha ya Askari akiwa na pesa zinazodhaniwa kuwa za Rushwa