IRINGA: Mahakama Kuu Yafuta Hukumu ya Kijana Aliyeshitakiwa kwa Kumbaka Binti Bikra wa Kijerumani

IRINGA: Mahakama Kuu Yafuta Hukumu ya Kijana Aliyeshitakiwa kwa Kumbaka Binti Bikra wa Kijerumani

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Wakati mwingine, lugha ngumu na utaratibu za kisheria zinaweza kufanya haki ionekane kama kitendawili. Kesi ya kijana Selemani inatupa somo muhimu: makosa madogo ya kisheria yanaweza kuleta madhara makubwa.

Shortly, Selemani alishtakiwa kwa makosa ya unyang’anyi na ubakaji wa binti bikra kutoka Ujerumani. Lakini, Jaji Mugeta aligundua kuwa kulikuwa na kasoro katika utambuzi wa mtuhumiwa (Selemani). Hii ilipelekea kufutwa kwa hukumu ya awali na Selemani akaachiwa huru. Kesi ya Selemani inatukumbusha wajibu na umuhimu wa kuzingatia kila kipengele cha kisheria kwa umakini ili kuweza kuipata haki.

Hukumu kwa kiswahili 👇
IMG_20240531_201641.jpg

IMG_20240531_201712.jpg

IMG_20240531_201729.jpg

IMG_20240531_201901.jpg

IMG_20240531_201837.jpg

IMG_20240531_201918.jpg
IMG_20240531_201932.jpg

IMG_20240531_201948.jpg

Credit: Tanzlii
Link 🔗: Selemani Nyigo @ Mwanyigo vs Republic (68 of 2021) [2024] TZHC 2343 (30 Mei 2024)
 
Inawezekana kweli mrufani ametenda kosa. Ila makosa kama hayo na mfanya aachiwe huru, kwa muda?
 
Inawezekana kweli mrufani ametenda kosa. Ila makosa kama hayo na mfanya aachiwe huru, kwa muda?
Yeah, inawezekana kosa alifanya kweli ila uzembe wa vyombo vya usalama kushindwa kufata taratibu zinazohitajika kisheria zinamfanya mrufani awe huru moja kwa moja, labda Jamhuri ikate rufaa kwenda mahakama ya rufani na mahakama ya rufani iamue vinginevyo.​
 
Jaji amechemka.
Sasa mhanga amemtambua mbakaji lakini unakataa ushahidi wake kwa kuwa hakuwa ametoa "unique description" ya mtuhumiwa kwa wapelelezi?#??
 
Nishazoea kwenye mafaili yake anayosomaga mke wangu,
Unakuta neno appelant vs respondent
Au plaintiff vs respondent.

Kiswahili kina ugumu wake aisee!
 
Jaji amechemka.
Sasa mhanga amemtambua mbakaji lakini unakataa ushahidi wake kwa kuwa hakuwa ametoa "unique description" ya mtuhumiwa kwa wapelelezi?#??
Sheria zetu zinahitaji kesi ya jinai kuthibitishwa pasi kuacha shaka.​
 
Hivi tanzania ushahidi wa DNA hautumiki mahakamani?
Swali zuri. Inaruhusiwa lakini ni kama watanzania (mamlaka inclusive) huwa tunajisahau sana katika hili. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Juma CJ katika kesi ya Christopher Kandidus Vs Jamhuri alibaini licha ya kupitishwa kwa Sheria ya Udhibiti wa DNA ya Binadamu, 2009 [SHERIA Na. 8 ya 2009], uchunguzi wa jinai na mashtaka nchini Tanzania bado unasita kutumia kikamilifu ushahidi wa DNA ili kuziba mapengo ya ushahidi na kutatua uhalifu hasa pale ambapo hakuna ushahidi wa moja kwa moja.​
IMG_20240531_211433.jpg

Kwa maana ya kwamba, ingawa sheria ya kudhibiti matumizi ya DNA ilipitishwa mwaka 2009, bado katika vitendo vya uchunguzi na mashtaka ya jinai nchini Tanzania, ushahidi wa DNA haujatumiwa kikamilifu kama inavyotakiwa. Hii inasababisha mapengo ya ushahidi yasijazwe ipasavyo, hasa pale ambapo hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa uhalifu.​
 
Back
Top Bottom