Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

UPDATE

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru

WhatsApp Image 2018-11-05 at 10.39.52.jpeg

====

ABDUL NONDO ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA

Swali la Hakimu la msingi, ni Je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga?? Pili, mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga.

Tatu, hakuna ushahidi toka jamhuri kuwa mshatikiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi wa hisia.

Nne, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa kwa kila namna na hata kielelezo kilicholetwa na Jamhuri kinatia mashaka sana, kwa mkanganyiko huu makahama imejizuia kuyaamini maelezo yaliyoletwa mahakamani.

Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatikiwa alitekwa au hakutekwa, hilo ni jukumu la polisi.

Hivyo basi, mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru.

Mwisho kabisa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unawashukuru mawakili wake waliosimamia kesi ya Abdul Nondo tangu mwanzo, lakini kipekee zaidi tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika hukumu hiyo.

Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2018.
Na: THRDC

zaidi, soma:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

My take:

Hivi watu wa kitengo hawawezi kukuteka wakapora simu kisha wakaanza kutumiana mesej na demu waliomset wao ajidai demu wako unachat nae wakat ushapotezwa na hujitambui ili kupoteza ushahidi?
Kama alipata wakili mzuri atashinda hii kesi! Kuna sehemu nyingi zina introduce reasonable doubts!
 
Back
Top Bottom