Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Ashukuriwe Mwingi wa Rehema, M Mungu, kwani kuachiwa kwa Mpiganaji Nondo ni ushahidi tosha kuwa uongo wa Jamhuri umeshindwa.

Kelele zetu pamoja na kelele za kimataifa kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu TZ nazo zimesaidia sana kuishinyikiza serikali kuiachia mahakama kuwa chombo huru.

Wadau msichoke, tuendelee kuishinyikiza serikali kuacha aina zote za ukandamizaji. Zitto, Fatma Karume, T Lisu, Msigwa nyie ndio viongozi wetu katika mapambano haya.

Tunashuhudia kupungua kidogo kwa kelele za unyanyasaji ama viongozi wa serikali wao kwa wao kupingana kuhusu kauli zao wenyewe. Ni vigumu sasa hivi kujua serikali ni nani. Ama mkuu wa mkoa ni sehemu ya serikali au wizara ndio serikali. MMoja anapotoa tamko katika madaraka aliyonayo na mwingine kuja kusema si msimamo wa serikali bila ya kujua nani amekosea, ndio ujue serikali imechanganyikiwa. Big up wadau!!!!!!
 
Back
Top Bottom