tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Alitekwa na watu wasiojulikana.Kwa hiyo waliomteka kina nani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alitekwa na watu wasiojulikana.Kwa hiyo waliomteka kina nani
Hakimu kukataa kujitoa kwenye kesi sio kujiandaa kulipa kisasi. Mahakimu weledi hutenda kulingana na sheria na kuuchambua ushahidi. Kesi nyingi za serikali zina madoa ya kisiasa na haziwapi shida mahakinu wanaojitambua.Asiwe kama hakimu wa kesi ya sugu kapokea maagizo katoa hukumu kalala mbele
Hivi huyu hakimu si alikataa kujitoa dogo aliposema hana imani nae? Tutegemee hukumu ya namna gani?
Mungu Ni zaidi ya madereva atamsimamia.Chuo walimsimamisha kumfurahisha Makonda...
Mungu ametenda haki hatimae imekuwaNamuombea kwa Mungu amsaidie.......Awe na ujasiri tu na kufahamu kabisa nchi yake kwa sasa kila mtu sio raia wa hapa.....ni mkimbizi
Huyo ni bingwa sana wa kuchanganya dini na siasa. Unakumbuka wakati ule wa dawa za kulevya? siku hiyo alienda kusali makanisa matatu sasa umewahi kuona wapi mkristo anasali makanisa matatu kwa siku moja au mwisilam kuingia kuswali misikiti mitatu kwa sala ya ijumaa tu?Eti ndiye Amiri jeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam. Jamani imekaaje watu wa Dar kila kukicha kamanda wenu mkuu ni vilio tuu hadharan? hamjisikii aibu?
Kamanda wa hivi anaweza kuona panya chumbani akapanda juu ya kabati kujificha.
Hii hukumu ukiiangalia kwa makini unapata picha nani alimteka Nondo na pia nani ni mhusika mkuu wa utekaji wa watu wenye maoni kinzani na viongozi wa serikali.Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.
Mliopo iringa update muwe mnatupa.
UPDATE
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru
View attachment 921914
====
ABDUL NONDO ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA
Swali la Hakimu la msingi, ni Je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga?? Pili, mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga.
Tatu, hakuna ushahidi toka jamhuri kuwa mshatikiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi wa hisia.
Nne, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa kwa kila namna na hata kielelezo kilicholetwa na Jamhuri kinatia mashaka sana, kwa mkanganyiko huu makahama imejizuia kuyaamini maelezo yaliyoletwa mahakamani.
Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatikiwa alitekwa au hakutekwa, hilo ni jukumu la polisi.
Hivyo basi, mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru.
Mwisho kabisa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unawashukuru mawakili wake waliosimamia kesi ya Abdul Nondo tangu mwanzo, lakini kipekee zaidi tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika hukumu hiyo.
Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2018.
Na: THRDC