Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Naifatilia kwa karibu sana
Duh yaani kaachiwa huru.. kumbe kuna mambo huwa yanakuzwa ili kutisha watu
Sasa Chuo kinafanyaje maana walimchimba mkwara mkubwa sana
Aombe uraia kwanza bila hivyo chuo hakiwezi kumpokea.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

UPDATE

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru

View attachment 921914
====

ABDUL NONDO ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA

Swali la Hakimu la msingi, ni Je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga?? Pili, mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga.

Tatu, hakuna ushahidi toka jamhuri kuwa mshatikiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi wa hisia.

Nne, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa kwa kila namna na hata kielelezo kilicholetwa na Jamhuri kinatia mashaka sana, kwa mkanganyiko huu makahama imejizuia kuyaamini maelezo yaliyoletwa mahakamani.

Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatikiwa alitekwa au hakutekwa, hilo ni jukumu la polisi.

Hivyo basi, mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru.

Mwisho kabisa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unawashukuru mawakili wake waliosimamia kesi ya Abdul Nondo tangu mwanzo, lakini kipekee zaidi tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika hukumu hiyo.

Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2018.
Na: THRDC
Inamaana mpenzi wake na lile kopo la pafyumu walishindwa navyo kuviwasilisha mahakamani!
 
Mahakama pia ingetoa amri ya kurudishwa kwenye masomo yake pale UDSM haraka sana ingekuwa poa sana
 
Haki imetendeka. Sasa wamtafutie kesi ingine kwamba yeye si raia wa Tanzania. Au yeyote ya uchochezi.
 
Shule ndo bac tena; au la atafute private maana jamaa hawatakubaki arudi pale.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

UPDATE

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru

View attachment 921914
====

ABDUL NONDO ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA

Swali la Hakimu la msingi, ni Je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga?? Pili, mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga.

Tatu, hakuna ushahidi toka jamhuri kuwa mshatikiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi wa hisia.

Nne, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa kwa kila namna na hata kielelezo kilicholetwa na Jamhuri kinatia mashaka sana, kwa mkanganyiko huu makahama imejizuia kuyaamini maelezo yaliyoletwa mahakamani.

Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatikiwa alitekwa au hakutekwa, hilo ni jukumu la polisi.

Hivyo basi, mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru.

Mwisho kabisa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unawashukuru mawakili wake waliosimamia kesi ya Abdul Nondo tangu mwanzo, lakini kipekee zaidi tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika hukumu hiyo.

Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2018.
Na: THRDC

Pole sana kwa kukosa masomo UDZIMWI. Who pays. ?
 
Lengo lilikuwa kumuharibia masomo yake ya chuo, na yule mwanamke alietoa ushahidi wa uongo kuwa ni mpenzi wa Nondo, Mungu ampe adhabu inayo mstahili maana ni chukizo kwa Mungu kumshuhudia jirani yako uongo.

Hao wanaomshitaki Nondo ndio waliotengeneza hiyo scenario ya huyo mwanamke ili ionekane ni demu wake. Nchi hii ya kipumbavu sana. Wanawake wengine wanapandikizwa na system. ogopa sana mwanamke, narudia tena pumbavu sana huyo mwanamke
 
Iringa. Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka iliyotoa dhidi yake.

Nondo ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuchapisha taarifa za uongo kwamba “nipo hatarini” na kuzisambaza mtandaoni na kutoa taarifa za uongo kwa askari Polisi Koplo Salim wa Kituo cha Polisi Mafinga wilayani Mufindi kuwa alitekwa na watu wasiojulikana Dar es Salaam na kupelekwa kiwanda cha Pareto Mafinga.

Akitoa uamuzi huo leo Jumatatu Novemba 5, 2018 Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Liad Chamshana amesema katika kosa la kwanza upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha uongo wa maneno ya mshtakiwa na hata vielelezo ilivyotoa mahakamani hapo vilikuwa na walakini.

“Shahidi wa kwanza hadi wa sita hawakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya kosa hilo na badala yake walitumia hisia na mashaka kutoa ushahidi wao na kushindwa kuithibitishia mahakama kwamba mshtakiwa ndiye aliyeandika maneno hayo ya uongo na maana ya maneno hayo yaliyosambazwa kwenye mitandao,” amesema

Katika kosa la pili, Chamshana amesema upande wa Jamhuri ulishindwa pia kuthibitisha kosa la mshtakiwa huyo aliyekwenda katika kituo cha Polisi cha Mafinga kama mlalamikaji kabla hajageuziwa kibao na kuwa mshtakiwa.

“Hakuna ubishi kwamba Machi 7, 2018 mshtakiwa alikuwa Mafinga na alikwenda kituo cha Polisi kutoa malalamiko yake. Upande wa Jamhuri na utetezi wote wanakubali,” amesema.

Amesema cha kushangaza mashahidi wote saba wa upande wa Jamhuri walishindwa kutoa ushahidi unaonyesha namna mshtakiwa huyo alivyofika Mafinga na ule unaoonyesha kabla ya kufika Mafinga alikuwa wapi.

Kwa upande wa upelelezi wa shauri hilo, Chamshana amesema vyombo vilivyofanya upelelezi (Polisi) dhidi yake viliacha majukumu yao ya kipolisi ili viweze kuthibitisha kama kweli au sio kweli mshatakiwa alitekwa na badala yake vikamchukulia kama muhalifu.

“Kwa msingi huo upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kama mshtakiwa alitenda makosa hayo na hivyo Mahakama inamuachia huru,” alisema na kuongeza kwamba upande wa mashtaka unaweza kukata rufaa.

Source: MWANANCHI
 
Aibu kubwa sana kwa Mwigulu si walisema alienda kwa hawara yake kule na kuna sms zimeshikwa za kwamba alikuwa anachat na hawara yake halafu akajidai kutekwa. huu ushahidi uliyeyuka yeyuka vipi mahakamani mapaka tunasoma hapa kwamba yuko huru??
Mwigulu sasa hivi huku mtaani anakubali na kukiri kwamba zile maiti za coco beach ni za watanzania wenzetu
 
Polisi na serikali yao wamemtesa sana Nondo kimwili na kisaikolojia, Mungu amfanyie wepesi kijana mwenzetu arudi chuoni kumalizia shule yake.
 
Haki imetendeka. Sasa wamtafutie kesi ingine kwamba yeye si raia wa Tanzania. Au yeyote ya uchochezi.
Hakimu Aliem-acquit Bwana Abdul Nondo Anaitwa *_Liad Mohamed Chamshama_* Msambaa Wa Lushoto
 
Back
Top Bottom