Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Yani mind ya hawa wanajiita wapinzani sijui huwaga wanaitoa wapi hasa wakishinda kesi unasikia mahakama imetenda haki wakati ndo jukumu lake la kisa kutoa
 
Ukiona hivyo jua ktk Mahakama kuna ulakini ktk kutoa haki...ama zinaingiliwa ktk utekelezaji wa majukumu ya kutoa haki... Thus why jamii inapongeza haki ikitendeka
 

hapa wewe ndio una makosa ni muhimu kutoa pongezi au asante hata kama ni haki yake mfano umeenda hotel kula unahudumiwa kwa pesa yako lakini ni wajibu kusema asante kwa anaye kuhudumia. mungu katuumba sisi ni haki yake kutupa pumzi ya kuvuta kutuoteshea mazao kwa sababu tule tuishi lakini unatakiwa kumshukuru pamoja kuwa ni wajibu wake lakini anataka ashukuriwe
 
Mkuu umechanganya mafile. [emoji119]
 
Hao majaji naamini wanakuwa katika shinikizo kubwa kutoka kwa serikali kuu, hivyo ni bora kuwashukuru tu...wangeweza kuamua kivingine na Watanzania walivyo hawawezi kufanya lolote
 
Unapotimiza wajibu wako vizuri pongezi unafaa ila sio za kulazimisha
 
Nashindwa kuelewa nisaidieni, ivi Mwalimu,Hakimu na Madakitari wanatofauti gani kiutumishi?
 
Hizi double standards mnazobariki zinatafuna kizazi baada ya kizazi, Daktari akimfanyia Mgonjwa operation Sijawahi ona wanapongezwa kama mfanyavyo kwa mahakimu, mwalimu anafundisha mtoto kutoka kuchora mistari mpaka anaumba herufi Sijawahi ona pongezi lakini hakimu akitimiza majukumu yake anapongezwa. Nooooo
 
Waalimu, tabibu na wakunga, kazi zao zinaaminika au kuchukuliwa kama ni za kutenda wema zaidi kuliko kudhuru.
Kwa polisi, hakimu au mwanajeshi, haitegemewi sana hasa kwa nchi zetu, akutendee haki au wema labda uwe unajuana naye.
Jamii inapata ahueni na mshangao linapotokea jambo kama la Bw Nondo kuachiwa bila kukutwa na kosa.
Wote niliotaja hapo juu wanatekeleza wajibu wao, na kwa wapokea huduma zao hawawajibiki kuwapongeza au kushukuru, ila pale unapotegemea jambo baya Kutokea halafu likatokea jambo jema, wengi hujikuta wakipongeza na kushukuru.
 
Au kwa mfano,Raisi anapofanya kazi ya msingi aliyoajiriwa kwayo;yani kuleta maendeleo nk wajibu wake.
 
Mwigulu mchemba najua unafuatilia uzi huu,vipi unajisikiaje?,baada ya wewe na wapambe wako kushindwa kuithibitishia mahakama ka alijiteka.

Jambo la kushukuru ni ka pamoja na kojikomba kotee kule,umetupwa kando.

Viongozi punguzeni jeurii,kumbukeni kua hapo mlipo ni kwa muda tuu
 
Mkuu nimekuelewa, kwahiyo police na Mahakama hawategemewi kutenda haki! Haki kwao ni bahati mbaya. Na kwakua Raia ni mshangao?
 
Reactions: Auz
Kutekana tekana ni mambo ya kishamba sana!
Huyu dogo aliita media akamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani enzi hizo Mwigulu ajiuzuru kwa kushindwa kulinda raia
Ndipo yote haya yakamtokea
Badala ya kuchunguza hapo hapo wakamuita muongo
 
Hivi Mwigulu Nchemba anajisikiaje akipata taarifa hii?

Malipo ni hapa hapa duniani.
Nakumbuka Mwigulu Nchemba alimkejeli sana huyu Dogo
Ila Mungu sio Mungu wa Juma peke yake kamtendea haki bwana Nondo kupitia hakimu
 
Kwahy ni kweli huwa anaiingiilia Mara nyingine???naona umempongeza hapa kwa kuiachia Mahayana ifanye kazi yake kama vile ni sawa yt? Kuiachia??????
 
Dah k weli mungu ametenda...lkn swali langu n moja ...je aliekua mshitakiwa amechukua hatua gn baada ya kupotezewa mda wake wakati akifuatilia kesi yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…