Iringa: Maria Ngoda aliyefungwa kwa kukutwa na nyama ya swala aachiwa huru na Mahakama Kuu

Mama uliyerudishwa uraiani karibuni Sana lakini Tanzania imejaa maigizo ya kutosha. Ulihukumiwa miaka 22 jela rufaa ikakatwa na UWT. Kwangu Mimi hapo ndipo maigizo yalipo.
Imekuwaje leo umeandika kistaarabu kiasi hicho wakati nimezoea kuona wewe muda wote ukitukana matusi na kuombea vifo tu utafikiri wewe ni Mungu? Au simu umemuazima au kumuachia mtu mwingine?
 
Mleta mada umepotosha kwa 100%.
Yule mama ameachiwa huru baada ya kushinda rufaa yake kwenye mahakama ya kanda, kesi ambayo imesimamiwa kwa 100% na chama cha mawakili wa Tanganyika (TLS), na hakuna mtu wala taasisi yoyote iliyowalipa mawakili hao au kugharamia kesi hiyo.

Moderator wa JF mnapaswa kuwa makini na mahiri katika kuchuja taarifa ili kuifanya JF kuwa chanzo cha uhakika cha kutoa taarifa.
 
Acha wivu wewe.kwa hiyo unataka kusema kuwa huyo mama mjane na mnyonge hajaachiliwa huru? Unataka kusema kuwa hujasikia kazi kubwa iliyofanywa na CCM nyuma ya pazia kama alivyotamka mhusika? Usicheze na CCM Wewe. CCM Ni dude kubwa sana ambalo likiamua kuingia vitani lazima lipate ushindi wa kishindoo
 
Mleta mada anapaswa kupigwa ban kwa kuleta taarifa yenye mwelekeo wa kupotosha.
Mama ameachiwa kwa msaada wa TLS na sio UWT.
 
Mleta mada anapaswa kupigwa ban kwa kuleta taarifa yenye mwelekeo wa kupotosha.
Mama ameachiwa kwa msaada wa TLS na sio UWT.
CCM imefanya kazi ya kijasusi na kikomandoo nyuma ya pazia mpaka ushindi wa kishindo ukapatikana ulioleta tabasamu na furaha kwa mama yule mjane .CCM Ni kama maji usipoyanywa utayaoga tuuu.
 
Usiwe mbishi wewe.
Jifunze kusoma na kuelewa.
Nimesema mama ameachiwa huru kwa msaada wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambao walijitolea bure.

Ni uongo na upotoshaji kusema wanawake wa CCM ndio wamehusika katika kufanikisha kuachiwa huru kwa mwanamke huyo.
 
Kama hujuwi kazi kubwa iliyofanywa na CCM nyuma ya pazia basi kaa na ubishi wako hapo hapo. Ukikua utaelewa
 
Acha ujinga wewe. Mimi Niko Iringa alichosema Zanzibar-ASP ndiyo sahihi.

Kama sifa basi wangepewa kina Mgonukulima na wenzake ambao ni viongozi wa BAWACHA Iringa.
 
Alifungwa na mahakama na siyo na CCM .Ndio maana CCM ikaamua kumpigania kwa nguvu zake zote yule mama mjane.
Jifunze hata kuushughulisha ubongo wako.
Mama alishtakiwa kwa kesi ya jinai (maana yake Serikali ya CCM ndio ilimshtaki huyo mama), na kama ilivyokuwa desturi ya mahakama zetu kupokea maagizo kutoka serikali ya CCM, huenda ilishinikizwa kumfunga huyo mama.
 
Acha ujinga wewe. Mimi Niko Iringa alichosema Zanzibar-ASP ndiyo sahihi.

Kama sifa basi wangepewa kina Mgonukulima na wenzake ambao ni viongozi wa BAWACHA Iringa.
Bawacha tangia lini wameanza kutetea wananchi na kuacha kazi ya kutetea matumbo yao inayohusu mapendekezo ya kutaka kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo.
 
Bawacha tangia lini wameanza kutetea wananchi na kuacha kazi ya kutetea matumbo yao inayohusu mapendekezo ya kutaka kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo.
Kuwa na wabunge wawili kwenye Kila Jimbo Kuna tatizo gani?

Hao UWT wanavotaka kuwe na 50 Kwa 50 watafikiaje kwenye lengo Hilo haraka kama si Kwa njia iliyopendekezwa na BAWACHA??
 
Kuwa na wabunge wawili kwenye Kila Jimbo Kuna tatizo gani?

Hao UWT wanavotaka kuwe na 50 Kwa 50 watafikiaje kwenye lengo Hilo haraka kama si Kwa njia iliyopendekezwa na BAWACHA??
Anzisheni majimbo yenu ndio milipe mishahara yenu inayotokana na pesa zenu.lakini pesa za mlipa kodi wa Tanzania hatuwezi kubali mapendekezo yenu yanayooshebulafi na uroho wa madaraka, bila kujali gharama kubwa mtakazo mbebesha mtanzania mlipa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…