Iringa: Maria Ngoda aliyefungwa kwa kukutwa na nyama ya swala aachiwa huru na Mahakama Kuu

Iringa: Maria Ngoda aliyefungwa kwa kukutwa na nyama ya swala aachiwa huru na Mahakama Kuu

Mbona mwanzo hamkusema hilo kwamba Kesi inasimamiwa na UWT? Angalizo: Tusipende sana vya kunyonga. Kama ni credit (Kongole) mwachie anayestahili na huyo baadaye atakuja kukushukuru ww au kukupongeza kama kweli ulihusika na Mafanikio yaliyopatikana.
Sifa na pongezi lazima ziwaendee UWT jumuiya ya CCM chini ya mwenyekiti wake mama marry chatanda pamoja na katibu mkuu wake Mheshimiwa jokate mwegelo walio amua kumpigania mama huyu mnyonge baada ya kusikia hukumu iliyokuwa imetolewa kwa mama huyu.
 
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa leo imemwachia huru Maria Ngoda aliyehukumiwa miaka 22 jela kwa kosa la kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala Novemba 3, 2023, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), Jokate Mwegelo ameeleza.

Bi. Ngoda ameachiwa baada ya kushinda rufaa iliyosimamiwa na UWT.

Pia soma > Kumfunga Maria jela miaka 22 kisa nyama ya swala ni matokeo ya kuwa na wanasheria waliokosa hekima na busara

----
Ndugu zangu Watanzania,

Umoja wa wanawake wa CCM Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa mama marry chatanda kama mwenyekiti pamoja na katibu mkuu wake Mheshimiwa Jokate Mwegelo, imefanikiwa kumrejeshea tabasamu na furaha mama Maria wa Iringa ambaye alikuwa amefungwa kifungo cha muda mrefu kwa madai kuwa alikutwa na nyama ya porini kinyume na sheria.

Leo februari 16 ndio ilikuwa siku ya hukumu baada ya umoja huo wa CCM kumkatia rufaa mama huyo mnyonge na aliyehitaji msaada wa hali na mali ambapo mahakama imetoa hukumu na kumuachia huru mama huyo mnyonge aliyetetewa na chama cha Mapinduzi kinachowajali, kuwatetea na kuwasemea wanyonge.

Hii ndio sababu ya CCM kuendelea kuwa kimbilio la wanyonge na kuendelea kuungwa mkono na kupigiwa kura za ndio kwa kishindo kila uchaguzi. Sasa unafikiri ni vipi mama huyu ambaye amebubujikwa machozi ya furaha baada ya kutolewa gerezani atashindwa kuipigia kura CCM?

Ni vipi ataacha kuiunga mkono CCM? Ni vipi ndugu, jamaa, marafiki na watoto wake wataacha kuipenda CCM iliyo mtetezi wa wanyonge?

CCM ni mabingwa wa kutengeneza Matatizo halafu wakiyatatua wanashangilia na kupongezana.
 
Picha zako umeziona lakini?
 
Picha zako umeziona lakini?
Hakuna mahali popote unapoweza kuzipata picha zangu .zinazosambazwa siyo zangu na ndio maana nimejikalia kimya tu nikiwaacha mkiendelea kushangilia maana najuwa tayari nimeshawashinda tayari.
 
Sijui Bwana Hakimu Said Mkasiwa anajihisi nini huko alipo kutaka kumdhulumu fukara wa watu uhuru wake kwa kitu cha kipumbavu kabisa.

Laana ya milele imuandame kwa dhulma ya haki aliyotaka kuitenda.
Unamlaumu hakimu ama Sheria, unafahamu sheria inasemaje kuhusu mtu akikutwa na nyama pori, ya kiwango kile?

Hata kama sheria ingesema anyongwe, hakimu hana namna isipokuwa kusema anyongwe!

Umesoma hukumu ukajua sababu ya yeye kuachiwa? Unajua kwamba ni teknikalities kwamba wakati wa mahojiano hakupewa nafasi ya kuita mwanasheria na pia alihojiwa zaidi ya muda wa saa 4 kama sheria inavyptaka na si kwamba kifungo ni batili?

Najua hujasoma mpaka form four lakini mambo mengine ulizaga kabla hujalalamika!
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa imemuachia huru, Maria Ngoda ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa kukutwa na vipande 22 vya nyama ya swala.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 16, 2024 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Elvin Mgeta ambaye amesema kuwa kutokana na hoja zilizowasilishwa na mkata rufani, Maria hana hatia na yupo huru.

Maria alihukumiwa kifungo cha miaka 22, Novemba 3, 2023 na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Said Mkasiwa baada ya kumtia hatiani.

Chanzo: Mwananchi
 
Natoa hongera kwa UwT kumpigania huyo mama haijalishi wakilitumia suala hilo kisiasa.
hakimu aliyemhukumu alipaswa acharazwe viboko akiwa uchi mbele ya halaiki.
 
Nje ya mada . Hivi kuna uwezekano wa mahakimu na mawakili kuwa makada wa ccm?
 
Wewe mbona hawakutetei ukapata ajira huko wanakuacha unakuwa ombaomba tu humu jukwaani?
Lucas mwashambwa ni mfa maji! Alianza kumsifia Mama, alipoona amempotezea, akahamia kwa Tulia! Baada ya kuona na yeye amempotezea, sasa amehamia kwa Paul Makonda!

Kote huko anahangaika tu. Njaa imemkaba mpaka kooni! U CHAWA wenyewe hauwezi! Maana anamsifia mtu mpaka anagundua kabisa dogo ni mnafiki na ana njaa kupitiliza.
 
Mimi sina njaaa maana ni mkulima mchapa kazi na ninaye kula kwa jasho langu.
 
Back
Top Bottom