Iringa: Maria Ngoda aliyefungwa kwa kukutwa na nyama ya swala aachiwa huru na Mahakama Kuu

Mbona mwanzo hamkusema hilo kwamba Kesi inasimamiwa na UWT? Angalizo: Tusipende sana vya kunyonga. Kama ni credit (Kongole) mwachie anayestahili na huyo baadaye atakuja kukushukuru ww au kukupongeza kama kweli ulihusika na Mafanikio yaliyopatikana.
Sifa na pongezi lazima ziwaendee UWT jumuiya ya CCM chini ya mwenyekiti wake mama marry chatanda pamoja na katibu mkuu wake Mheshimiwa jokate mwegelo walio amua kumpigania mama huyu mnyonge baada ya kusikia hukumu iliyokuwa imetolewa kwa mama huyu.
 

CCM ni mabingwa wa kutengeneza Matatizo halafu wakiyatatua wanashangilia na kupongezana.
 
Picha zako umeziona lakini?
 
Picha zako umeziona lakini?
Hakuna mahali popote unapoweza kuzipata picha zangu .zinazosambazwa siyo zangu na ndio maana nimejikalia kimya tu nikiwaacha mkiendelea kushangilia maana najuwa tayari nimeshawashinda tayari.
 
Bi. Ngoda ameachiwa baada ya kushinda rufaa iliyosimamiwa na UWT.[emoji1787]
Ni uongo kabisa labda ututhibitishie vinginevyo. Ina fanana na msemo huu"Rob Peter to pay Paul"
 
Sijui Bwana Hakimu Said Mkasiwa anajihisi nini huko alipo kutaka kumdhulumu fukara wa watu uhuru wake kwa kitu cha kipumbavu kabisa.

Laana ya milele imuandame kwa dhulma ya haki aliyotaka kuitenda.
Unamlaumu hakimu ama Sheria, unafahamu sheria inasemaje kuhusu mtu akikutwa na nyama pori, ya kiwango kile?

Hata kama sheria ingesema anyongwe, hakimu hana namna isipokuwa kusema anyongwe!

Umesoma hukumu ukajua sababu ya yeye kuachiwa? Unajua kwamba ni teknikalities kwamba wakati wa mahojiano hakupewa nafasi ya kuita mwanasheria na pia alihojiwa zaidi ya muda wa saa 4 kama sheria inavyptaka na si kwamba kifungo ni batili?

Najua hujasoma mpaka form four lakini mambo mengine ulizaga kabla hujalalamika!
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa imemuachia huru, Maria Ngoda ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa kukutwa na vipande 22 vya nyama ya swala.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 16, 2024 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Elvin Mgeta ambaye amesema kuwa kutokana na hoja zilizowasilishwa na mkata rufani, Maria hana hatia na yupo huru.

Maria alihukumiwa kifungo cha miaka 22, Novemba 3, 2023 na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Said Mkasiwa baada ya kumtia hatiani.

Chanzo: Mwananchi
 
Natoa hongera kwa UwT kumpigania huyo mama haijalishi wakilitumia suala hilo kisiasa.
hakimu aliyemhukumu alipaswa acharazwe viboko akiwa uchi mbele ya halaiki.
 
Nje ya mada . Hivi kuna uwezekano wa mahakimu na mawakili kuwa makada wa ccm?
 
Wewe mbona hawakutetei ukapata ajira huko wanakuacha unakuwa ombaomba tu humu jukwaani?
Lucas mwashambwa ni mfa maji! Alianza kumsifia Mama, alipoona amempotezea, akahamia kwa Tulia! Baada ya kuona na yeye amempotezea, sasa amehamia kwa Paul Makonda!

Kote huko anahangaika tu. Njaa imemkaba mpaka kooni! U CHAWA wenyewe hauwezi! Maana anamsifia mtu mpaka anagundua kabisa dogo ni mnafiki na ana njaa kupitiliza.
 
Mimi sina njaaa maana ni mkulima mchapa kazi na ninaye kula kwa jasho langu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…