#COVID19 Iringa: Mikusanyiko yazuiwa kudhibiti Corona

#COVID19 Iringa: Mikusanyiko yazuiwa kudhibiti Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesitisha kwa muda shughuli zote zisizo za lazima zinazohusisha mikusanyiko pamoja na makongamano yasiyo ya lazima, ikiwa ni moja ya jtihada za mkoa huo katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Sendiga amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona maambukizi ya virusi vya corona mkoani Iringa yanaendelea kuongezeka.

Amewataka Wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka, na kuvaa barakoa wawapo katika maeneo yenye watu wengi ikiwa ni pamoja na kwenye vyombo vya usafiri.

WhatsApp-Image-2021-07-22-at-11.32.07.jpeg
 
Waliopigia debe korona enzi za Magu kuwa hatua hazichukuliwi sasa ndio wavunjaji protokoli za kovidi lialia...what a turn of events.
Mbona hii turn unaiangalia upande mmoja? Wote wameturn mkuu
 
Mikusanyiko yote iwe ya lazima na isiyo ya lazima yaweza kueneza covid. Angesema amepiga marufuku mikusanyiko yote angeonekana yupo serious. Agizo lake kama mengine yaliyoanza na yanayofuata yamelenga kongamano la KATIBA Tazama watu walivyolundikana kwenye mabasi , masokoni, makanisani, wanafunzi madarasani nk.

Aseme huku amechukua hatua gani. Watanzania sio mbumbumbu kiasi hicho.
 
Mikusanyiko yote iwe ya lazima na isiyo ya lazima yaweza kueneza covid. Angesema amepiga marufuku mikusanyiko yote angeonekana yupo serious. Agizo lake kama mengine yaliyoanza na yanayofuata yamelenga kongamano la KATIBA Tazama watu walivyolundikana kwenye mabasi , masokoni, makanisani, wanafunzi madarasani nk... Aseme huku amechukua hatua gani. Watanzania sio mbumbumbu kiasi hicho.
Umemaliza kila kitu. Virus vya korona hawachagui aina ya mikusanyiko. Kama angekuwa na nia kweli angesema mikusanyiko yote iepukwe.
 
IMG_20210722_170113.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesitisha kwa muda shughuli zote zisizo za lazima zinazohusisha mikusanyiko, yakiwemo makongamano, kutokana na maambukizi ya COVID-19 kuongezeka mkoani humo. Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
 
Back
Top Bottom