toughlendon_1
JF-Expert Member
- Feb 7, 2018
- 6,283
- 11,253
Watu wa mikoani wapo serious na nyege
"enyi vijana sikilizeni mnapokuwa masomoni acheni mchezo na mapenzi mnawapa shida wazazi wenuuu"
Badala ya kuendekeza masomo na ajira zenyewe za tabu wanakumbatia MAPENZI....
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Iringa unasikitika kutangaza kifo cha Mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza, Mwaka wa Pili Idara ya Uandishi wa Habari PETRONEL P. MWANISAWA kilichotokea siku ya Jumanne, 1/6/2021 hapa mjini Iringa.
Uongozi unawatangazia kuwa kesho Alhamis, 3/6/2021 kutakuwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu kuanzia saa 8:00 mchana kisha mwili kusafirishwa kwenda Sumbawanga kwa ajili ya mazishi.
Tuungane na Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki katika kuomboleza msiba huu.
Raha Ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umuangazie...Apumzike kwa Amani
-----
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Iringa, Petronel Mwanisawa (22) amefariki dunia kwa kunyongwa na mpenzi wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mtuhumiwa, Prudence Patrick (21), ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho.
Akizungumza na Mwananchi, Kamanda Bwire amesema tukio hilo limetokea Juni 1, mwaka huu maeneo ya Kihesa.
Amesema siku ya tukio marehemu hakurudi nyumbani kwao jambo ambalo si kawaida yake, hivyo wazazi wake waliingiwa na hofu na kuanza kumtafuta.
"Marehemu alikuwa anaishi na wazazi wake, na huyu mtuhumiwa yeye alikuwa amepanga. Kwa hiyo siku ya tukio alitoka kwenda chuo, lakini mpaka usiku akawa hajarudi, ndipo wazazi walianza kupata wasiwasi, wakampigia simu rafiki yake lakini hawakufanikiwa," amesema Kamanda Bwire na kuongeza
"Kwa hiyo jana ndo tukampata, na hiyo ni baada ya mtuhumiwa mwenyewe kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa mzazi wa marehemu akisema alikuwa na Petronel na kwamba amefariki. Baada ya hapo hakupatikana tena," alisema.
Amesema baada ya wazazi kupata taarifa hizo waliripoti kituo cha polisi, ndipo askari walikwenda katika nyumba ya mtuhumiwa na kuukuta mwili wa marehemu.
Bwire amefafanua kuwa, taarifa za awali zinaonyesha binti huyo alinyongwa na mpenzi wake na chanzo ni wivu wa mapenzi.
"Mtuhumiwa tulimkamata njia ya kuelekea Dodoma alipokuwa akijaribu kutoroka na upelelezi wa tukio hilo unaendelea," amesema Kamanda Bwire.
Chanzo: Mwananchi
Hili neno, "mapenzi", linakosewa sana matumizi yake. Mapenzi ni kati ya wanandoa tu, nje ya hapo siyo mapenzi bali ni, "zinaa na uasherati".
Jamii yetu inapaswa kubadilika, mfano, kichwa cha habari hii kilipaswa kusomeka hivi; "MWANAFUNZI WA MWAKA WA PILI AMNYONGA MWASHERATI MWENZAKE".
Akili hawana....malengo hawana...wamejaa umaskini wa fikra na kipato....HAWA vijana wametumwa kufanya mapenzi au kusoma?wazazi kwa kweli tuna kazi kubwa ya kuwalea kwa maadili mema.zile enzi zetu kulikuwa hakuna matukio kama haya.ulikuwa unamaliza chuo hata humjui msichana anafanana na nini lkn siku hizi hawa vijana akili zao zote ni mapenzi.
Yaaani nilichogundua there is no perfect murder. Sijui huwa inakuwaje unakamatwa tuu. Sasa ukiwaza ni kitu gani kilimfanya atume msg huwezi elewa.Ukiua unatakiwa kuwa na akili mingi, sio unatuma tuma vimeseji vya kishamba. Watakunasa.
Mkuu kwani umeona gari zima? Kama trailler ni Double diff je?ahahahaha nimecheka alafu mwanamke mwenyewe alomsababishia majanga ndio huyo ? aisee watu wa mikoani hawapo serious yan huyo ndio akupe kesi ya murderer aisee acha kabisa
polisi wanamshikilia "Prudence Patrick" ndio jin ala mtuhumiwa, kwa hiyo aliyenyongwa sio mwanaume, amenyongwa mwanamke. angalia picha vizuri.Kumbuka aliye nyongwa ni mwanaume
Ndugu vipi, mbona kama unatetea sana matendo machafu yaitwe kwa maneno mazuri mazuri?Suala siyo muktadha bali mtumiaji alichagua maana gani kwenye neno moja lenye maana zaidi ya moja. Hapo upo, Mr Kukariri!???
Ndugu vipi, mbona kama unatetea sana matendo machafu yaitwe kwa maneno mazuri mazuri?
Au na wewe ni mmoja wa wazinzi na waasherati?
Tuige mfano wa nchi za wenzetu hasa Saud Arabia, Mwanaume na Mwanamke mkikamatwa mnafanya ngono pasipo kuoana mnatangazwa kama "wazinzi" wamekamatwa na siyo "wapenzi" wamekamatwa.
Kiuhalisia na kimaadili, hili neno "mapenzi", wapenzi, linatumika isivyostahili na hii imepelekea mmomonyoko mkubwa wa maadili miongoni mwa jamii yetu.
Maneno kama, "wazinzi", "waasherati", "wafiranaji" yangekuwa yanatumika kwa uwazi katika habari ingesaidia sana kupunguza haya matendo yasiyofaa miongoni mwa jamii yetu.
Na ndiyo maana unaona wanafunzi wanafanya ngono hovyo hovyo na kuitana "wapenzi" sababu hili ni neno zuri tena linahamasisha ngono. Lakini kama jamii ingeacha kutumia hili neno isivyopasa na wafanya ngono nje ya ndoa wakaitwa "wazinzi" au "waasherati" baadhi ya vijana wangeogopa kushiriki hilo tendo kabla ya ndoa kwa kuhofia kuitwa majina mabaya.
Hili neno wapenzi siku hizi linatumika kupunguza uzito wa dhambi, mwenyez Mungu atusamehe lkn hao ni wazinzi na sio wapenzi.Ndugu vipi, mbona kama unatetea sana matendo machafu yaitwe kwa maneno mazuri mazuri?
Au na wewe ni mmoja wa wazinzi na waasherati?
Tuige mfano wa nchi za wenzetu hasa Saud Arabia, Mwanaume na Mwanamke mkikamatwa mnafanya ngono pasipo kuoana mnatangazwa kama "wazinzi" wamekamatwa na siyo "wapenzi" wamekamatwa.
Kiuhalisia na kimaadili, hili neno "mapenzi", wapenzi, linatumika isivyostahili na hii imepelekea mmomonyoko mkubwa wa maadili miongoni mwa jamii yetu.
Maneno kama, "wazinzi", "waasherati", "wafiranaji" yangekuwa yanatumika kwa uwazi katika habari ingesaidia sana kupunguza haya matendo yasiyofaa miongoni mwa jamii yetu.
Na ndiyo maana unaona wanafunzi wanafanya ngono hovyo hovyo na kuitana "wapenzi" sababu hili ni neno zuri tena linahamasisha ngono. Lakini kama jamii ingeacha kutumia hili neno isivyopasa na wafanya ngono nje ya ndoa wakaitwa "wazinzi" au "waasherati" baadhi ya vijana wangeogopa kushiriki hilo tendo kabla ya ndoa kwa kuhofia kuitwa majina mabaya.
Uchafu wa uzinzi mshahara wake huwa HIVYO.....Hili neno wapenzi siku hizi linatumika kupunguza uzito wa dhambi, mwenyez Mungu atusamehe lkn hao ni wazinzi na sio wapenzi.
Hapo utasikia wapenz wamekutwa wakifanya tendo la ndoa akata hata hyo ndoa hawana
Nakubaliana na wewe 100%Hili neno wapenzi siku hizi linatumika kupunguza uzito wa dhambi, mwenyez Mungu atusamehe lkn hao ni wazinzi na sio wapenzi.
Hapo utasikia wapenz wamekutwa wakifanya tendo la ndoa akata hata hyo ndoa hawana
Naona kilichomchoma ni KUTOROKA akiwa amebeba devices zake ... Wazee wa kazi wana locate tu inasoma wapi.. useless kbs[emoji23]Ukiua unatakiwa kuwa na akili mingi, sio unatuma tuma vimeseji vya kishamba. Watakunasa.
Hakujua hata kuzima?!Naona kilichomchoma ni KUTOROKA akiwa amebeba devices zake ... Wazee wa kazi wana locate tu inasoma wapi.. useless kbs[emoji23]
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Watu wa mikoani wapo serious na nyege
[emoji38][emoji38]Unaonekana wewe ni mtaalam wa mambo hayo eee...