Iringa na Njombe ilivyoshambuliwa na chawa

Iringa na Njombe ilivyoshambuliwa na chawa

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kwa ambao hamjui chawa nawasihi mtembelee vijiji vya Iringa mjionee!

Kutokana na jiografia ya ubaridi, wadudu hawa wamekita kambi mkoa huu! Inahitajika tahadhari kubwa sana kukwepa chawa uwapo mkoa huu.

Hoteli na lodge nyingi wanatumia mablanket mazito ambayo siyo rahisi kufuliwa Mara kwa Mara kutokana na hali ya hewa, hali hiyo imechangia sana kuzagaa kwa chawa!

Ukifika mkoa huu usipokuwa makini unaweza ukasalimia mtoto mdogo shikamoo ukizani ni mzee mwenye nywele za Mvi kumbe ni mayai ya chawa yametanda kichwani!

Wabibi wa huku miongoni mwa starehe ni pamoja na ile ya kuua chawa kwa vidole ama ile ya kung'ata kwa meno.

Ukiwa kijijini kama unaendesha chombo unatakiwa kwenda pole pole la sivyo unaweza kugonga mtu aliyesimama barabarani akiua chawa kiunoni!

Ajabu kuliko yote! Ni vile chawa wakiwa kiunoni wanakuwa weupe, na wakihamia kichwani wanabadilika rangi wanakuwa weusi!

Usiombe umkute mtu ana chawa halafu miguu nayo iwe imetafunwa na funza mithili ya vidole kuwa kama Tangawizi! Unaweza kuondoka Iringa bila kuaga!

Chawa wa Iringa Kiboko!
 
Ukweli mtupu! Nimetembelea maeneo ya Malangali, Ifunda, Nyololo, Makambaku, Ulayasi na Madaba chawa ndio kwao na mimi nimeondoka nao.

Nimerudi Same nimefua nguo kwa maji ya moto nikanyoa na mkulungu (kipara) angalau sasa nina ahueni.
 
Mzee hapo kwa ifunda nakubishia hamna chawa Wala kukunguni kidogo watu wa hapo wamedevelop kidogo
Ukweli mtupu! Nimetembelea maeneo ya Malangali, Ifunda, Nyololo, Makambaku, Ulayasi na Madaba chawa ndio kwao na mimi nimeondoka nao.

Nimerudi Same nimefua nguo kwa maji ya moto nikanyoa na mkulungu (kipara) angalau sasa ninaaahueni.
 
Back
Top Bottom