Iringa: Upelelezi wakamilika, mtoto anayedaiwa kuwalawiti wenzake kupandishwa kizimbani

Iringa: Upelelezi wakamilika, mtoto anayedaiwa kuwalawiti wenzake kupandishwa kizimbani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kesi nane za ukatili wa kingono kati ya 19 zinazohusu watoto waliodhalilishwa na mtoto mwenzao mwenye umri wa miaka 15 mkoani Iringa, zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki hii.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bulumbi amesema kuwa uchunguzi wa daktari umebaini kuwa watoto wote wamedhalilishwa na mtoto huyo ambaye anashikiliwa na polisi kulinda usalama wake.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwapatia zawadi za pipi, pesa na kuwaruhusu kuangalia televisheni nyumbani kwao, ili wakubali udhalilishaji huo.

Matukio ya ukatili wa kingono mkoani Iringa yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku, ambapo mwaka 2021 pekee watoto 384 walifanyiwa ukatili wa aina hiyo.

Wadau wa kupinga ukatili mkoani humo wamewataka wazazi kuchukua nafasi yao ya malezi ili kuwanusuru watoto na ukatili wa kingono.

Source: TBC

Soma: Iringa: Watoto 19 wafanyiwa unyanyasaji wa kulawitiwa na mtoto wa miaka 15
 
Toto limerawiti wenzake, halafu Jeshi linalihifadhi na kutoa sababu kuwa ni kwa ajili ya usalama wake.

Hilo likitoka inabidi jamii illiwajishe kwa kupigwa mawe mpaka kifo.

Limeharibu watoto wetu.
 
Kosa tunalo lifanya wazazi tunajua kuzaa tu ila mengine tuna muachia Mungu kulinda watoto.

Umri kuanzia 0-18 bado yupo kwenye uangalizi mkubwa wazazi na jamii. Ila mtoto akishajua kutembea, kuongea na kula basi umeshusha mzigo na kuacha ajifunze mwenyewe.

Tujifunze kwa wahindi jamani tuliopo nao
 
Watu wa iringa punguzeni ugwadu basi mbona mitoto ya chuo ipo kibao kwanini mnabaka?
 
Toto limerawiti wenzake, halafu Jeshi linalihifadhi na kutoa sababu kuwa ni kwa ajili ya usalama wake. Hilo likitoka inabidi jamii illiwajishe kwa kupigwa mawe mpaka kifo. Limeharibu watoto wetu.
Uko wapi utawala wa sheria?
 
Aiseee kaharibu vizazi vya mbeleni. Ale mvua za kutosha bila kujali umri wake
 
Dah tumuombe mungu atuongozee watoto wetu,

Hizi teknologia saa nyingine ni shida
 
Watu wa iringa punguzeni ugwadu basi mbona mitoto ya chuo ipo kibao kwanini mnabaka?

Habari inamhusu mtoto wa miaka 14/15 kuwalawiti watoto wenzake kwa kuwadanganyia pipi, pesa, kuangalia tv nyumbani kwao, nk.
 
duu!! toto hatari hilo, lishapunguza idadi ya wanaume, yani kila kukicha idadi ya wanaume inapungua,

wanawake wana tabu, sijui watakuja kuolewa na kina nani wakati wanaume wanazidi kupungua.
 
Back
Top Bottom