carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Uko sahihi mkuuKwa hii nchi hilo halishangazi
Anapotea mtu anajua kuongea sembuse hilo takataka lisiloongea
Habari, ndugu mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.WATU wasiojulikana wanadaiwa kuiba transfoma katika Kijiji cha Mafinga, Kata ya Kipengere, Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, tukio lililosababisha kukatika kwa huduma ya umeme katika Kitongoji cha Makela.
Tukio hilo linadaiwa kutokea jana, majira ya saa tisa usiku, baada ya umeme kukatika ghafla na kuwaacha wananchi wakidhani kuwa kulikuwa na hitilafu ya kawaida katika mfumo wa usambazaji wa umeme.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mafinga, Eses Chaula, amesema baada ya umeme kukatika, wananchi waliwasiliana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakihitaji msaada wa kurejesha huduma hiyo.
Amesema wataalamu wa TANESCO walipofika eneo la tukio na kufanya ukaguzi, walibaini kuwa transfoma ilikuwa imeshushwa kutoka kwenye nguzo na vifaa muhimu vilivyokuwa ndani yake kuondolewa.
Chanzo : Habari leo
Habari aise, asante kwa kuwasiliana nasi.Hao ni Watumishi wenyewe wa Tanesco wameamua kula Kwa urefu wa kamba zao.
Habari Moisemusajiografii , asante kwa ujumbe wako.Transfoma ambayo inaendesha umeme mkubwa inaibwaje kizembe hivyo?Hao ni wenyeji wa Tanesco ndiyo wamefanya jambo lao.An inside job!
Watumishi wenzenu wameiba sio wewe admin unaekaa ofisini acha kutetea ujinga, nani asiye fundi na vifaa maalumu anaweza kusogelea umeme mkubwa wa HT?Habari Moisemusajiografii , asante kwa ujumbe wako.
Ni muhimu kusubiri matokeo ya uchunguzi kabla ya kuwahusisha watumishi wa TANESCO na tukio hili. Tayari Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, huku jitihada za kuwatafuta wahusika zikiendelea.
Asante.^FL