luangalila
JF-Expert Member
- Jan 12, 2014
- 6,346
- 6,928
Hii habari niliyo isikia punde toka katika taarifa ya habari ya Ufm
Ni huko Iringa mitaa ya Kiesa ambapo mtoto mmoja wa umri wa miaka 15 anaedaiwa kuwalawiti watoto wenzie zaidi ya 10 kwa kuwahadaa kwa vipipi na kuwawashia luninga nyumban kwao kisha kuwafanyia mchezo huo mbaya wa kikatili, kwa mujibu wa taarifa mtuhumiwa alianza mchezo huo tangia mwaka 2019 alipohamia mtaa huo, taarifa pia inasema mtuhumiwa kwa sasa yupo chin ya jeshi la Polisi
Hii ni wake up call kwa wazazi tuongeze umakini kwa watoto tuangalie ni nani anacheza nae na tabia za hao watoto, sasa imagine kototo cha miaka 15 kinawalawiti wenzake
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Iringa: Watoto 19 walawitiwa na mtoto mwenzao
Watoto 19 wenye umri wa kati ya miaka minne hadi 14 wa eneo la Kihesa Kilolo Mkoani Iringa wamegundulika kuwa wamefanyiwa vitendo vya ukatili kwa kulawitiwa na mtoto mwenzao mwenye umri wa miaka 15 ambaye alianza kufanya vitendo hivyo kuanzia mwaka 2019 baada ya kuhamia mtaa huo.
Mmoja wa waathirika, mtoto mwenye umri kati ya miaka sita mpaka tisa amekuwa akidanganywa na mtuhumiwa kwa kupewa zawadi ndogondogo na kupelekwa nyumbani kwao kutazama runinga ambapo ndipo vitendo hivyo vimekuwa vikifanyika.
Hata hivyo, mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.
“Jumamosi tulienda kuwachunguza watoto afya pale Frelimo (hospitali), tukakuta wapo vizuri lakini wa kwangu ndiyo ambaye alikutwa amelawitiwa zaidi na kuharibika, naumia sana kwa hili,” alisema mzazi mmoja.
Naye, Elizabeth Swai ambaye Mkuu wa Dawati ya Watoto na Jinsia Mkoa wa Iringa amewaambia wakazi wa eneo hilo kuwa:
“Idadi ya watoto waliofanyiwa ukatili huo inazidi kuongezeka, tulipokuwa Kituo cha Polisi tuliendelea kumfanyia mahojiano mtuhumiwa akatutajia watoto wengine watatu, nao walipokuja wakataja wenzao wengine.
“Mpaka sasa kesi hii imefikia watoto 19 wameletwa pale kwetu na idadi inaendelea kwa kuwa wanaendelea kutajana.”
Source: UFM