Iringa: Watu saba wafariki kwa ajali iliyohusisha ambulance na toyo, wengine 15 wajeruhiwa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Watu saba wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali ya gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kugongana na toyo katika eneo la Luganga, lililopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Akizungumza baada ya kutembelea majeruhi wa ajali hiyo leo Jumamosi, Aprili 19, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Linda Salekwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema kuwa taarifa zinaonyesha watu hao walikuwa wanakwenda shambani kufanya kazi, ndipo gari hilo likagongana na toyo hiyo na kusababisha watu hao kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.
 
Duh ,hatari mchezo wa duniani wengine wanazaliwa huku wengine wanakufa ili binadamu waendelee kuteseka ..

Pole yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…