Is Diamond Platnumz good as he is au kuna mengine?? Mbinu za kutoboa kimataifa.

pinno

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
1,213
Reaction score
1,229
Naomba kwanza nianze kwa kudeclare interest, Mimi ni fan wa Diamond!

Ni fan wa Diamond si kwa sababu huwa napenda mziki wake at first place, Big NOOOOO! Nimejikuta nakuwa fan wa huyu jamaa kwa sababu mimi ni muumini wa Uzalendo ,ambao unanifanya niwe na shauku kubwa ya kuona jina la Tanzania linang'aaa zaid na zaid katika anga la kimataifa.

Napenda nyimbo zake ndiyo lakin si kwa uwingi na level ya kulinganisha navyo penda nyimbo za TID,Ben Paul,Marlow,Belle, Jux,Barnaba, Ibrah, Mangwair (RIP),MB Dog,Christian Bella na wengine wengi

Lakini mwisho wa siku najikuta tu nakubali kuwa He is the best, na ndo King wa hii industry na hii industry haikuwah pata mtu kama yeye (Mr Nice records considered well)

At the same time, Najisikia vibaya pale ambapo Wajasiriamali wabunifu wa Mfano Kenya na Rwanda, wanang'aa zaid katika international spot light kuliko vijana wetu wabunifu wa kitanzania ambao nao wana products nzuri tu, na start ups zao zinakick zaid kuliko hata hao ( Tembelea KINU na BUNI uone vijana hawa)

Najisikia vibaya napoona These big NGOs na other international firms vyeo vingi vya juu ,vinashikiliwa na watu kuitoka nje, same kwa big hotels na chochote kile chenye harufu ya ukimataifa basi sura ya Mbongo huwa ni ya kutafta sana, ukiipata inakuwa bado ina binywa, wakati tuna wasomi wetu wengi sana ambao wanauwezo mzuri sana.

Huku kujisikia vibaya hakuishii hapo tu, kunaenda kwenye michezo,Movie,had kwenye kuuza utalii wetu wa ndani. Na ndo hapo napopata conclusion kuwa pengine tatizo letu wabongo si ubora wa bidhaa, au ubora wa kazi, au Kujituma katika kutengenza kazi nzuri,au Elimu na Maarifa au uzuri wa vipaji, HAPANA, Hivyo vyote tunavyo vingi, na tumejaliwa sana . Tatizo Pengine ni kuwa WATANZANIA SIYO WAZURI SANA KATIKA KUUZA KAZI ZETU,KATIKA KUJIBRAND NA KATIKA KUTANGAZA UBORA WETU.

Ndo maana Marehem Kanumba, japo siyo kwamba alikuwa ni bora kuliko JB na Richie Richie ( According to my sister & My wife ) ambao ni wadau wakubwa wa Bongo Movie lakin aliweza kuanza kupenya na akafanikiwa kuiweka industry ya movie mahali fulani.

Swali ni kuwa is Diamond platnumz really that good??, Kwa sasa yeye ndo msanii bora Africa( MTV Emma),Akitoa wimbo hauwi tena topic ya kujadiliwa Jamii forums tu,tena kwa thread moja kama wasanii wengine, au XXL au FNL tu, inakuwa topic duniani huku mitandao top ya Naigeria,SA,na Kenya. (Watu wenye viburi barani Afrika) ikiongoza kumjadili, huku Vituo kama MTV base,Trace etc vikiback up huku Instagram na Youtube vikisimama kwa muda kidogo kwa views na comments.

Mfano:- ametoa wimbo tar 11 December kwa channel mbili tofaut you tube, moja ina view laki tano na kitu, na ningine yenye English subtitle ina viewers laki nne kasoro (had muda huu napoandika hii post) wakati huo huo Belle 9 alietoa wimbo wiki moja kabla yake, viewers hawajafika hata elf arobain, huku Jux alietoa siku moja kabla yake akiwa na viewers elfu therathin na kitu, Kaka angu Kala jeremiah pia nae kaachia kichupa chake bora kabisa tangu aanze mziki siku hyo hyo lakin viewrs bado hata elfu therathin ( Had muda huu napoandika hii post)

Swali je , kuna mbinu gani nyingine ambazo Diamond anatumia kutangaza mziki wake, ili na wasanii wengine waige? maana kazi zao ni nzuri tu, na wengi wanafanya vyema sana (Hongera kwa Navy Kenzo,Weusi na Vannesa,jIDE na The legend himself AY-Pioneer wa kupeleka mzik wa Tz Nje.

Sitaki kuamin kwamba ni msanii bora kuliko wote wali wahi tokea ndo maana amekuwa na record ambazo hazijawahi tokea, sitaki kuamin kwamba ni bahati, kwamba sijui ananyota kali kuliko wengine, sitaki kuamini , sitaki kuamini, Nachodhani ni mbinu fulani ya kibiashara ambayo wengine hawajaijua, au hawaujui, na hata wafanyabiashara na wafanyakazi wengi sisi tunaojaribu kupenya katika masoko ya kimataifa ni wakati sasa wa walau kujifunza vitu vichache vilivyowork kwa huyu jamaa na kuangalia namna ya kuviapply katika field zetu, iwe ni katika Employment,Business,Entertainment etc etc.

So Thread hii itumike kwa wadau mbalimbali kutoa mawazo yao, unadhani ni mbinu gani, au ni njia zipi zimemfanya Diamond kupenya katika international markets, ili Wasanii wengine na hata watu wa field nyingine waweze kucopy ili tuzid kupenya kimataifa zaid na zaid.

Wasanii wengi wanatoa video kali sasa hiv, na video nyingi zinapata access kwenye international media, lakin bado hawajapenya, so ina maana kuna kitu zaid ya kuwa na video kali, Collabo ??? wasanii wengi tu washafanya collabo za kimataifa lakin still hawakufika alipo fika Diamond, so Ni kitu gan kingine ambacho hatukijui?? Ni kama kwenye soko la ajira mtu akwambie uwe na PHd au Masters ya kitu fulani ndo upate kazi mahali fulani lakin still unakuta bado wabongo wenye hizo qualification wanapuliza, ina maana kuna code fulan bado hawajaibinya sawa sawa, so ni code gani hiyo???

Karibuni!!!
 
Nyota ya kupendwa + ujanja + kuwa mtu wa watu (jamaa hajioni ye ndo yeye kama wengine) + Mungu + managers + kujali wafanyakazi wake + kurudisha fadhila kwa kuinua vipaji vya watu wa chin ka harmonize etc etc
 
Kushirikiana na chama tawala nako pia mtu kama kala jeremaya yeye nyimbo zake za ukawa tu na kampeni ukawa atatoboa kweli? Siri ya mafanikio kuwa ccm damu bhaaas!
 
Dah! Unaonekana ni mwerevu, ila unatia huruma. Eti hujajua siri ya Diamond kutoboa.!? Hauko makini. Jiongeze kidogo.
 
Sijajua jamaa, ndo unijuze aisee,
 
Dah! Unaonekana ni mwerevu, ila unatia huruma. Eti hujajua siri ya Diamond kutoboa.!? Hauko makini. Jiongeze kidogo.

Sijajua jamaa ndo unijuze aisee
 
Kufika alipofika Diamond sio kitoto, ni nguvu kubwa sana imetumika. Ila mwisho wa siku kikubwa ni kuja kukubalika kwa MASHABIKI (ambao wapo bega kwa bega kufuatilia kazi zako) na WADAU WA BURUDANI (mf. BET, MTV etc)

Wasanii wetu wengi kipindi hiki wamekuwa wakijitahidi kuwekeza tu kwenye video kali, ni vizuri sana lakini bado haitoshi.

Diamond anawekeza kwenye kazi zake.., Kuanzia kwenye team yake WCB => Managers wanne hapa Tanzania, manager mmoja Nigeria special kwaajili ya West Africa, anamawakala nchi jirani, photographer, videographer, dancers, stylish, mlinzi, studio, na anayelink na diehard fans wa watsaap groups/insta ambao kukitokea tu sherehe flan lazima awachukue na mashabiki wa kutosha... Hiyo team ni noooma, lazima uwe juu.

Pili wewe kama wewe msanii, diamond anajiweka kistaa muda wote, anajuwa kutoa burudani ya maana anapokuwa kwa stage, timing ya utoaji ngoma kiasi kwamba umsikie redioni january hadi desemba, na nyimbo ambazo hata mtoto mdogo anaweza akakuimbia bila kumung'unya maneno, na video kali sio za gharama tu, hivyo vyote vilimfanya awe msanii wa gharama zaidi Afrika Mashariki. Ndio maana unakuta barnaba, bele9, casim mganga, alikiba wote wapo stage moja ila pesa waliyolipwa kwa pamoja haifikii ya Diamond pekee, hiyo ni impact ya branding na hiyo pesa ndio inafanikisha investment zote kwenye muziki wake

Na kikubwa kujitangaza, kila kikubwa unachokifanya watu wakifahamu hata medias wasipokufuata basi unawapa taarifa ili usikauke mitandaoni, na hiyo inakuongezea hata mashabiki wanaokufuatilia mitandao ya kijamii, na kukuongezea jina zaidi

Na hivyo ndio vitu baadho vinavyofanya uwe msanii mkubwa, wenzetu wanaangalia
-Success (lazima utoe hit songs, na zisiishie kwenu tu zivuke Afrika hadi duniani na zitokee kwenye top charts tofauti)
-Buzz (Una collables zipi? una trend mitandaoni kwa kuzungumziwa kivipi? kuna styles zipi za muziki au dance unazofanya na zinatoboa? )
-Intangibles (Element ipi inayowavuta mashabiki wako either kwa stage/nyimbo zako etc, endorsement deals zipi unazipata, na brand yako kiujumla)
-Impact (Hapa unakuja upo vipi kwenye social medias? nyimbo unazotoa youtubes, itunes, kma ni album zinauza vipi??? hapa ni namba tu...!!)
⬆ HAPO NDIO UNAPOKUJA KUJUA VIDEO KALI PEKEE HAITOSHI....

Je UTANIPENDA??? King Of Afropop...
 
Nimekuelewa sana Kidingi ,
 
Last edited by a moderator:
Mimi navyofahamu watanzania ni wavivu na wanapenda kuridhika sana, mfano vijana wengi wanaohitimu vyuo Tanzania hua hawanaga mawazo ya kufanya kazi nje ya Tanzania wao wanachojua ni TRA,NSSF,BOT,CRDB etc....wakati kuna taasisi nyingi sana za kutest bahati yako...kwenye anga za kimataifa...hata mtu akiajiriwa hua hana mawazo mapya i.e kuanzisha kampuni inayotoa huduma nzuri juu ya kitu fulani unakuta mtu ana experience ya miaka 15 lakini bado muajiriwa tu watu hawana malengo na kutamani kuacha kitu kitakachofaidisha vizazi vyao vya mbeleni i.e. wanigeria wao mtu yupo radhi kuacha ajira na aanzishe biashara endelevu mfano kwenye sekta ya mafuta na gesi kampuni nyingi sana ni za wazawa

kwwnye swala la ubunifu wabongo wengi hawana ubunifu mfano huko kinu,binu, au tume ya sayansi ukienda mara nyingi vijana wengi wanachofanya ni kuchati facebook ubunifu kwa maana mtu hawezi waza kutoa kitu ambacho kitasaidia wengi au kitakacho kua kinatumika na wengi, au ambacho lazima mtu akitumie wakifanikiwa hapo aaah lazima wafike mbali mtu hawezi fikiria kunzisha kitu chenye malengo ya kua na coverage nchi nzima

kwenye mziki wasanii wengi wameendekeza starehe, mziki wa sasa hivi ni hela, hela kwenye video hela kwenye kujibrand pia, mfano chid benz alikua juu sana kama angewekeza kwenye kutengeneza nyimbo nzuri ambazo ziko stock zenye mashairi yenye kuweza kuwashika mashabiki yani mziki wa sasa hivi unahitaji angalau uwe na nyimbo 12 za kuachia kila baada ya miezi 3 au 4 kwa mwaka ili watu wasikusahau na ili uweze kufanya shooo...na pia diamond hua anafanya promo kwenye mambo yake skendo nini na nini zile zote hela zinatumika ndo mana jamaa anastay current mwisho wa siku pia inabidi uwe na management nzuri yenye kukupa support kwenye mziki....kuwekeza kwenye mziki kwa kua na studio, kufanya kazi vizuri bila kua na wasi wasi wa kutokua na nyimbo ya kutoa au kukosa hela za kufanyia video na kutoendekeza starehe...daaah nimetumia simu samahani kama haitakua inatokea vizur...
 
Kushirikiana na chama tawala nako pia mtu kama kala jeremaya yeye nyimbo zake za ukawa tu na kampeni ukawa atatoboa kweli? Siri ya mafanikio kuwa ccm damu bhaaas!

Ah! sikweli
 
Kufika alipofika Diamond sio kitoto, ni nguvu kubwa sana imetumika. Ila mwisho wa siku kikubwa ni kuja kukubalika kwa MASHABIKI (ambao wapo bega kwa bega kufuatilia kazi zako) na WADAU WA BURUDANI (mf. BET, MTV etc)

Wasanii wetu wengi kipindi hiki wamekuwa wakijitahidi kuwekeza tu kwenye video kali, ni vizuri sana lakini bado haitoshi.

Diamond anawekeza kwenye kazi zake.., Kuanzia kwenye team yake WCB => Managers wanne hapa Tanzania, manager mmoja Nigeria special kwaajili ya West Africa, anamawakala nchi jirani, photographer, videographer, dancers, stylish, mlinzi, studio, na anayelink na diehard fans wa watsaap groups/insta ambao kukitokea tu sherehe flan lazima awachukue na mashabiki wa kutosha... Hiyo team ni noooma, lazima uwe juu.

Pili wewe kama wewe msanii, diamond anajiweka kistaa muda wote, anajuwa kutoa burudani ya maana anapokuwa kwa stage, timing ya utoaji ngoma kiasi kwamba umsikie redioni january hadi desemba, na nyimbo ambazo hata mtoto mdogo anaweza akakuimbia bila kumung'unya maneno, na video kali sio za gharama tu, hivyo vyote vilimfanya awe msanii wa gharama zaidi Afrika Mashariki. Ndio maana unakuta barnaba, bele9, casim mganga, alikiba wote wapo stage moja ila pesa waliyolipwa kwa pamoja haifikii ya Diamond pekee, hiyo ni impact ya branding na hiyo pesa ndio inafanikisha investment zote kwenye muziki wake

Na kikubwa kujitangaza, kila kikubwa unachokifanya watu wakifahamu hata medias wasipokufuata basi unawapa taarifa ili usikauke mitandaoni, na hiyo inakuongezea hata mashabiki wanaokufuatilia mitandao ya kijamii, na kukuongezea jina zaidi

Na hivyo ndio vitu baadho vinavyofanya uwe msanii mkubwa, wenzetu wanaangalia
-Success (lazima utoe hit songs, na zisiishie kwenu tu zivuke Afrika hadi duniani na zitokee kwenye top charts tofauti)
-Buzz (Una collables zipi? una trend mitandaoni kwa kuzungumziwa kivipi? kuna styles zipi za muziki au dance unazofanya na zinatoboa? )
-Intangibles (Element ipi inayowavuta mashabiki wako either kwa stage/nyimbo zako etc, endorsement deals zipi unazipata, na brand yako kiujumla)
-Impact (Hapa unakuja upo vipi kwenye social medias? nyimbo unazotoa youtubes, itunes, kma ni album zinauza vipi??? hapa ni namba tu...!!)
⬆ HAPO NDIO UNAPOKUJA KUJUA VIDEO KALI PEKEE HAITOSHI....

Je UTANIPENDA??? King Of Afropop...
Muuza sembe
 
Back
Top Bottom