Is It Possible?


Unajua hawa viumbe wanaangalia pia na mtu kwanza anakupima akiona umelegea ndio anaanza madudu yake, mi mwanzoni aligoma kabisa kutunza nikamwambia poa nikaa kimya siku moja akatokea hm eti nimekuja mwona mtoto hakyanani hatokaa asahau siku ile na ndugu/wazazi nilishawaambiaga kwamba huyu mtu bora asuse milele asijetokea hapa na akitokea naomba kila mtu akae pembeni aniachie mwenyewe hiyo kazi. Na alipotokea kila mtu alibaki kimya tukabaki wenyewe. Alishika adabu mbona hawa bwana huwa wanakupima kwanza ili aone ukimchekea imekula kwako.

Muwahi huyo mj1 kabla mtoto hajatimiza miaka 7 kwani baadae unaweza jikuta mtoto unanyang'anywa wakati akiwa mdogo ulihangaika nae peke yako shaurilo.
 

nyamayao dada yangu nilikuwa nimecross fingers usiingie humu maana najua ningekuwa karibu yako ningekula vibao.
Nawasoma but nashukuru mmenizindua usingizini.
 

Mmhhh hapo kwenye blue bold hebu nieleweshe vizuri........I believe you can definitely date someone else while separated/divorced.
Hapo kwa red, mnaweza kuachana peacefully na mkakubaliana process za kufata....ila ukumbuke kuwa kabla hamjafikia hapo mlikua na ugomvi uliopelekea kufikia maamuzi ya kuachana kwenu. Au ngoja nikusaidie kuwa kuna wanandoa wengine hata wanapofikia kuachana kuna mmoja wao anakuwa hakubali matokeo ndio maana wanakua hawaachani kwa amani ni ugomvi mwanzo mwisho. Ila kwa waliokubaliana ndio tunasema wameachana kwa amani.
 

halafu m2 utaachaje kum2nza mwanaoo but unataka kujua anaendeleaje? nanni anakusaidia kum2nza? ovyooo kabisa....halafu MJ1anaulizwa mbona nguo za baby ni zile zile bado 2 hajammwagia hata maji yaliyopo karibu, yaani kaja mikono mi2pu na maswali ya kijinga juu? MJ1 huyu kaka ni mzigo na anjua jinc ya kukuchezea haswa, hana mapenzi hapo aache kujiliza liza yamemshinda huko ndio kakumbuka shuka wkt kunakucha....ndugu waweke pembeni kwenye hili saga then chukua maamuzi yako mwenyewe kwa faida ya maisha yako/mtoto wako....na kweli wanaangaliaga pa kuchezea, mie mbona kumkimbiza uchi ningeweza pia.
 
inawezekana sana MJ1 mkabaki kuwa friends lakini kualikana tafrija na harusi hapana. Inategemea pia mmeachana kivipi. Kumbuka kuna wanaoachana sababu ya shinikizo la wazazi, mama kavalia njuga kwa sababu zake binafsi mkwewe hamtaka. mwanamme kwa kuogopa kupata radhi ya mama ikabidi waachane. mnaweza kubaki kua friends tu. pia kama ni wastaarabu miwivu ni mambo ya kizamani mkishaachana. sitaki kusema sana ya kwangu maana mnaweza msiniamini maana wengi hunishangaa mimi na mzazi mwenzangu, lakini inawezekana mkawa marafiki wazuri. ukitaka zaidi from my experience ni pm nitakueleza.
 
nyamayao dada yangu nilikuwa nimecross fingers usiingie humu maana najua ningekuwa karibu yako ningekula vibao.
Nawasoma but nashukuru mmenizindua usingizini.

ulimpenda/ullimjali/ukamdhamini/akauchezea moyo wako/akamtelekeza na mtoto....huyo mwanaume wa kazi gani kama wewe ndio kidume ndani (unam2nza mtoto/msomesha etc)....huyu bwana alivyoenda hakutegemea mambo yangeenda kombo sasa yameenda kombo ndio anatafuta pa kujifichia....na ningekunasa vibao uamue moja chap chap....unamrudia/humtaki tena...stori ingekuwa imeishaga 2nasonga mbele na ishuz nyingine za maisha, sasa wewe huyu huyu kila cku wa kumfikiria na kukupasua kichwa na maamuzi huchukui, u have only one life 2 live.....
 
Binafsi baada ya kuachana sitaki mahusiano yoyote zaidi ya kupeana taarifa za mtoto kwishaaaaa......michango akachangishe hawara zake na aende nao kwenye hizo shuhuli,kwani hakuuona umuhimu wangu kwa muda huo niliokua nae mpaka ajilete sasa hivi kama sio wanga kitu gani.....anipishe.
 

Na mimi nilimuuliza hilo swali mpenzi we hutaki kumtunza sasa unataka kujua hali yake ili iweje? nilimtimuaje? kutoka hapo akili ilimkaa sawa yaani unaleta sura yako ndio mtoto anakula au akiumwa tunaipeleka hosp manesi wakiiona anatibiwa bahati yake alitoka mbio maana hasira nilikua nazo ningemvunjia hata kioo cha gari pumbafu zake za wakati ule.

Mwanajamii jitoe fahamu siku moja moja bwana uone kama hajakaa sawa. Mi sasa hv huwa ananikumbushaga we mwanamke ndio ulinifanyaga nini wakati ule huwa namwambia ashukuru kipindi ile nilikua sina kazi so hela ilikua ya kuunga ingekua ndio sasa ningemkaribisha vizuri then ningeenda kumchukulia polisi wamsulubishe kwanza ndio angeelewa namaanisha nini
 
Mji
mie sihitaji hata kuona sura yake achilia mbali sms/simu..........najitahidi kumpatia mwanangu malezi stahili.......hayo ya haki za watoto sijui nini hizo ni hadithi kuna haki hapa duniani tusubiri mbunguni........mambo ya outing/urafiki/mtoto havina nafasi tena......ndugu zangu nimewaambia kama kujipendekeza ajipendekeze lakini nafasi hiyo haipo....kukiwa na shughuli yoyote kifamilia na akahudhuria unamuatendi kama humjui mpaka anajisikia vibaya kipindi kingine wala hathubutu kutia mguu...... kama mapenzi yalikuwa zamani sasa hivi yamebaki mazoea
 

Nyamayao
daah umenifurhisha na comment zako nimependa
inaumiza sana lakini kwa muda fulani unasahau na maisha yanakwenda
yanini kuendelea kuumia na hujui ni kwa muda gani
mambo ya kuja kuangalia mtoto mikono mitupu na madharau juu
daaah kalagabao ishia huko tena usigeuke nyuma ukawa nguzo ya chumvi bure

 
Yaani dada wee acha tu, hawa wanaume hawa!Yaani kama ulikuwepo alikuwa anasubiri tu maisha yanipige apate la kusema, Mungu ni mwema maisha yamempiga yeye sasa ndo anajua kuwa na mimi nipo, Kwakweli Mungu ni mwema nilimuachia kila kitu niliondoka na hati ya talaka tu lakini nilimwambia maneno haya Mungu atayaona machozi yangu na siku moja utakuja kunipigia magoti, ni miaka minne tu ameshaanza kunisumbua

pole ram...hapo ungekuwa choka mbaya walaaa acngekusumbua kabisa, ndio kwanza angejicfia kwamba alikuwa kila ki2 kwako, sasa mambo poa kinamuuma! hawa viumbe hawa bac 2.
 
Ni ngumu sana MJ1 kesho nitaeleza kwa kirefu,naenda kupika
 
Dah sikujua ukisafiri kwenda Vanuatu sredi zinakua na kasi ya ajabu...

Well, MJ1... pata kitu roho napenda, kama ni kualikana sawa, kama ni kutoalikana pia si mbaya!!!
 
Kwa walio bado vijana yaweza kuwa ngumu; kwa watu wazima ni very possible kwani watoto wanaweza ku arrange events na kuwakaribisha wazazi wote; ugomvi wenu ni wenu; when it comes to kids nyie ni baba na mama.
 
Kingine ni kweli it matters mliachana vipi though wengi wanaachana vibaya; Suala la msingi je mme move on?; mme let it go? Sioni sababu ya watu kuwa maadui kama hasira zilishaisha na hakuna mtu anaye mfeel mwenzie tena.

SI vizuri kuwa maadui wakati mnashare watoto. Ndio kuna hasira lakini nategemea baada ya muda zinaisha; na mnabaki friends for the sake of your kids.
 
Habari yako bro. naona upo busy na jukwaa la katiba.
Vp wewe shemeji yetu yule wa zamani hamuendelezi urafiki?

...astaghafirullah...

hakuna urafiki na mtu anayeumia roho kila akiniona na furaha aisee!...



...muonee huruma mjukuu wako mtiifu bana, mbona unamnyanyapaa namna hii?

nyamayao na maty nimewasoma postings zenu mna hasira nae balaa, lol!!!

mwanajamiione, pole mama...ukubwa jaa...
BTW, haya machungu ninayokusoma humu...ushawahi kukaa naye kitako na kumwambia
huyu bwana mkubwa kiuwazi na kiukweli jinsi ulivyomkinai?

...au nawe kama nduguzo (unamjua kilio na machozi yake yana nguvu ya kuyeyusha mshumaa bila moto?)
...maana khaaa,!...ingekuwa ni mimi ningekuomba na radhi na kuacha uende zako salama salmini
bila hata kukubughudhi tena maishani mwako na hizi story za "turudiane, turudiane...!"
 
Mbu, maumivu ya kichwa huanza taaratibu, unayaskia yanagonga kwa mbaaali sana

....mnh? aiseee.... acha ni log off kwanza.
asante kwa kuto ni quote kamanda.
 
Wapenzi aksanteni kwa comments zenu. Asprin nimekusoma babu ila jua tu bado cjayaanza maisha ya upweke so sijayachoka bado

Maty na nyamayao nimewapata vilivyo. Aksanteni sana.

Mbu, sina mengi ya kusema but naamini nilishasema nae sana ila nadhani alijua buttons gani apress nami nadance. But thanx to JF mmenifumbua macho.

MTM,DC,FL, Frank, DA, nyumba kubwa na wengineo woooote,ninawapa shukrani zangu kwa comments zenu ambazo zimenisaidia sana kuanika au kuanua. Mbarikiwe sana
 

Sasa wenzio hawataki kutoa muda hasira ziishe...wanataka kuzima moto kwa kutumia makaratasi!!

Kama kweli mtu wa namna hiyo angekuwa na akili basi angekubalii wakae mbali ili kila mtu pressure yake ishuke..Badala yake anamkanyagia mwenzio kila uchao...Hasira zitaisha namna gani

But one thing is clear...Jamaa anataka kuwa free na wakati huo kuwa attached kwa mtu ambaye hayuko free!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…