Kwanza kabisa, huyu dada ana overflow ma confidence kiasi cha kusisimua, dada ana own hiyo mike anaongea kama kakaa na rafiki zake sebuleni kwake anaongea nao, viongozi wetu hawajazoea watu wa aina hii, ukiongeza ni msichana kijana basi ndiyo kabisaa. Tamaduni zetu wengine kidada kikiongea kwa mi confidence kama hiyo, wakubwa (hasa wale walioteuliwa kisiasa na si kwa kuwa vipanga, kwa mfano Kikwete) wanakuwa intimidated. Doubly intimidated dare I say, kwanza na issues zinazozungumzwa, halafu pili issues zinazungumwa na kidada kidogo tu (yai bwena) kinawaangalia machoni na kuwauliza maswali, mara kinawaambia nyoosheni mikono juu kama mwalimu aliye na wanafunzi wake darasani, wazee wetu hawajazoea haya.
Of course Kikwete anachemsha, of course anaanza na "of koz" na kuchomekea "well" nyiingi. Labda ni swala la lugha na huenda Kikwete angeulizwa Kiswahili angeweza kujibu vizuri zaidi, lakini pia, to be fair, inawezekana anajua Kiingereza ila yuko slow, anahitaji muda wa kulitafsiri swali kutoka Kiingereza na kuliweka katika Kiswahili, halafu kulijibu katika Kikwahili kichwani, halafu kutafsiri kutoka Kiswahili kichwani kwenda Kiingereza halafu kujibu kwa kiingereza. ukimsikiliza utaona kuwa ingawa ni kweli Kikwete hawezi ku "think on his feet" na anaboronga, lakini typically style ya Kikwete ni kuanza kwa kuboronga boronga halafu kadiri anavyoendelea anayapanga mawazo yake vizuri, halafu katikati ya kuboronga atasema kitu kitakacho contradict kuboronga kwake -sometimes brilliant- halafu ukimpa muda anamalizia vizuri tu.
Case in point aliulizwa, kwa kiswahili kutoka kwa mtanzania katika hadhira friendly ya Watanzania hapo 42nd St NY,NY, kuhusu uwezekano wa watanzania walio nje kutumia channels za serikali kuwasaidia watu nyumbani. Akaanza kuongea very unpresidential, "mna hela nyinyi? Au mnataka kulaumiana tu?" baadaye sijui akajishtukia anachemsha and this was not in line with building the spirit of patriotism and love of country and folk, akabadili tune, akamalizia vizuri kwa kusema kuna njia nyingi tu za kusaidia, na ukitaka kusaidia unaanza na walio karibu yako, kama familia na kama unataka kusaidia zaidi unaweza kutumia njia zisizo za kiserikali, kawa ameongea doctrine ya serikali kutojihusisha na biashara, akawa ame encourage patriotism na love of country and folk at one go, lakini alianza kama anakunywa kahawa Saigoni vile.
Lakini hii style tunaiweza wenyewe watanzania katika media zetu, media mabazo rais akiulizwa swali analijibu kwa speech ya nusu saa. katika media ya kimataifa ambapo kila neno ni soundbyte Kiwete anaonekana mtupu, hata ukisikiliza huyu binti alivyomuuliza Kikwete, wakati huyu binti anaendelea kwa Waziri wa South Afrika kwa kweli alikuwa amemkatisha Kikwete, ni kama vile Kikwete alikuwa ana warm up tu na ndiyo kwanza anataka kuanza kujibu, huyu dada akaendelea mbele.
Alipoanza kujibu alikosa kulielewa swali, akawa anaelezea mambo basic kabisa ya investment kama vile fiscal incentive (sasa unafikiri investor anakuja nchini kwako kueneza injili, this is a no brainer na inaonyesha Kikwete hawezi kufikiri kwa haraka) mambo ya workshop na investment opportunity blah blah, hapo huyu dada akamshtukia jamaa hana analosema, akamuuliza tunajua hayo yanafanywa kote na nyie mmekuwa mnayafanya, tuambie unafanya nini tofauti.
Kikwete kashindwa kujibu, quite frankly inawezekana ndiyo mara ya kwanza anasikia mtu anamuuliza hili swali.This type of thinking is very western na sisi hatuko fast kiasi hiki, ndiyo kwanza tunaanza kuamka kwamba kuna financial crisis, wewe unatuuliza tunafanya nini differently? Of course Kikwete kamwambia we are doing nothing differently (and expect to be successful right?). Kwa kifupi kwa watu wanaofuatilia mambo dada kamuumbua mzee mzima, kwa sababu katika maneno yote aliyotakiwa kusema Kikwete hakutakiwa kusema we are not doing anything differently, angeweza hata kusema, kwa ukweli kabisa, kwamba jamani eeh, hii tafrani kubwa sana na hivi sasa ndiyo tunakaa sawa na tunajadiliana tufanyeje, na ndiyo moja ya sababu ya mkutano huu, anarudisha swali kwenye hadhira.Actually hiki ndicho alichofanya yule Waziri wa South Africa. All politicians all full of it, but some know how to cover it and sell it, Kikwete does not.Huyu bwana wa South Africa naye hakuwa na jibu, probably kwa sababu hii hii ya Kikwete, na wao ndio kwanza wanaamka, lakini yeye alijua kujibu, halafu hakuwa na tatizo la lugha, akawa anaflow sijui restructuring, sijui labor, sijui tough decisions, mwishowe akaona isiwe tabu, nishadanganya sana kwamba najua tunachofanya ngoja niwe mkweli tu kwani honesty is the best policy, na kama mtu atataka kunishtaki kwamba nimedanganya always nitaweza kusema mbona hapa mwisho nilisema ukweli? Akasema "we are still feeling our way through" translation, we dont know jack, we are just findiong out what to do now.
Kwa hiyo Kikwete anapoongea na media za kimataifa inabidi ajue kuwa watangazaji nao wana reputations zao za ku protect, na wakishagundua kwamba wewe huna nyimbo wanaku skip, ndiyo maana ingawa Kikwete na Waziri wa South Africa wote walikuwa wana bluff, lakini Kikwete alipewa air time ndogo sana kulinganisha na yule waziri wa South Africa, kwa sababu hajui ku bluff, dada wa watu akaona isiwe taabu bure, nisije kumuaibisha baba wa watu kesho nikatengeneza headline "Kikwete akiri serikali haifanyi chochote kipya kuhusu janga la uchumi". akaona heri lawama kuliko fedheha, akamkatisha, watu weeeeeeeee.
Labda angepewa dakika chache za kusema zidumu fikra za mwenyekiti, Kikwete angeweza kujieleza vizuri.