Is our president serious?

Is our president serious?

NN & P53 ............SIyo kama wamjibie at least wangejaribu kumpika vizuri..si mnaona wenyewe anavyochemsha hapo ni kwamba hana clue kabisa na what is going on ndani ya nchi yake...angalia ameulizwa swali la finacial crisi...amejikanyaga kishenzi na anajibu kuwa he will continue to do the same what the hell....yaani badala ya kufikiria changes for the future...oh well!...i am just confused aisee baada ya kumsikiliza raisi wetu kwa kweli....
 
Hao vijana "waliosoma" hawawezi kumjibia maswali Kikwete. Kwanza hao vijana "walisoma" na wenyewe I doubt kama wangeweza kujibu kila swali kwa ufasaha...

Mi nadhani ni bora awe anatumia Kiswahili kujibu hayo maswali yaulizwayo kwa lugha za kigeni

NN, we unadhani swala ni lugha?

Mi nadhani ukizoea blah blah alafu ukaletwa kwenye uwazi lazima upate bumbuwazi maana unajua watu watakukamata ukidanganya..
 
Hao vijana "waliosoma" hawawezi kumjibia maswali Kikwete. Kwanza hao vijana "walisoma" na wenyewe I doubt kama wangeweza kujibu kila swali kwa ufasaha...

Mi nadhani ni bora awe anatumia Kiswahili kujibu hayo maswali yaulizwayo kwa lugha za kigeni
Tatizo sio lugha bali uwezo!kwa nini Dominique Strauss Khan,mother language yake ni french ila anajibu vizuri kabisa kwa ki english!
 
Tatizo sio lugha bali uwezo!kwa nini Dominique Strauss Khan,mother language yake ni french ila anajibu vizuri kabisa kwa ki english!

Point! au Chavez hajui english lakini akiwa kwenye mikutano ya kimataifa anatumia lugha yake let mkarimani atafsiri....

Hapa kikwete swala siyo lugha ila ni poor communication skills...kuna watu humo ndani wanatumia lugha zao wanaongea french....na yeye angetumia tuu kiswahili...kuongea english siyo sababu ya kunekana better bwana....sema siye waswahili tunaona kuongea english unaonekana better than...
 
Tatizo sio lugha bali uwezo!kwa nini Dominique Strauss Khan,mother language yake ni french ila anajibu vizuri kabisa kwa ki english!

inawezekana na uwezo pia lakini lugha nayo inachangia.nadhani angeulizwa swali lilelile lakini kwa kiswahili majibu yake yangekuwa tofauti sana.
 
NN, we unadhani swala ni lugha?

Mi nadhani ukizoea blah blah alafu ukaletwa kwenye uwazi lazima upate bumbuwazi maana unajua watu watakukamata ukidanganya..

Inawezekana ikawa vyote viwili mkuu maana kuna kauli zingine huyu bwana alizowahi kuzitoa katika lugha ya Kiswahili zinazoweza kufanya akili yako izunguke kidogo...lakini ukitatua moja(lugha) kwa kiasi fulani unaweza kuboresha ujuzi/uwezo wako wa mawasiliano
 
Bob geldoff ndio mtu anaeongea most sense hapa.. hawa wanasiasa na wachumi-cum-wanasiasa hawana mpya. Rais wetu hajui anaongeanini. Anaanza kuflirt na huyu demu. The man is such an imbecile. Elimu jamani, does he not have a degree in economics
he dares say that 'some of these issues are difficult to comprehend' wakati yeye alijinadi kuwa ni mchumi and tumchague based on that. Wasteman.
 
Point! au Chavez hajui english lakini akiwa kwenye mikutano ya kimataifa anatumia lugha yake let mkarimani atafsiri....

Hapa kikwete swala siyo lugha ila ni poor communication skills...

hapana poor communication skills ni sawa tu na tatizo la lugha ambavyo sidhani ndio tatizo la Kikwete.

Hapa tatizo kubwa ni uelewa wa Kikwete katika mambo mbalimbali yanayohusiana na uchumi na njia mbalimbali mbadala ambazo yeye kama kiongozi anaweza kuzitumia kuhakikisha Taifa haliingii katika janga hili la kiuchumi au kuweza kulitoa taifa katika janga hilo.
 
Point! au Chavez hajui english lakini akiwa kwenye mikutano ya kimataifa anatumia lugha yake let mkarimani atafsiri....

Hapa kikwete swala siyo lugha ila ni poor communication skills...kuna watu humo ndani wanatumia lugha zao wanaongea french....na yeye angetumia tuu kiswahili...kuongea english siyo sababu ya kunekana better bwana....sema siye waswahili tunaona kuongea english unaonekana better than...


sasa Kelly which is which?lugha ndiyo hicho chombo cha mawasiliano ambacho skills zake ni speaking,reading,writing and listening.unaposema tatizo siyo lugha ni communication skills yaani sikuelewi unamaanisha nini.
 
Love him or hate him, Mkapa would have stolen the show there.....
 
Mimi nakataa kabisa kuwa tatizo ni lugha...tatizo ni ujuvi wa mambo ndio mushkeli hapo...Kwani angeshindwa kujibu kwa lugha ya kigeni kama angeulizwa CCM wana mpango gani wa kushinda 2010??
 
Kwanza kabisa, huyu dada ana overflow ma confidence kiasi cha kusisimua, dada ana own hiyo mike anaongea kama kakaa na rafiki zake sebuleni kwake anaongea nao, viongozi wetu hawajazoea watu wa aina hii, ukiongeza ni msichana kijana basi ndiyo kabisaa. Tamaduni zetu wengine kidada kikiongea kwa mi confidence kama hiyo, wakubwa (hasa wale walioteuliwa kisiasa na si kwa kuwa vipanga, kwa mfano Kikwete) wanakuwa intimidated. Doubly intimidated dare I say, kwanza na issues zinazozungumzwa, halafu pili issues zinazungumwa na kidada kidogo tu (yai bwena) kinawaangalia machoni na kuwauliza maswali, mara kinawaambia nyoosheni mikono juu kama mwalimu aliye na wanafunzi wake darasani, wazee wetu hawajazoea haya.

Of course Kikwete anachemsha, of course anaanza na "of koz" na kuchomekea "well" nyiingi. Labda ni swala la lugha na huenda Kikwete angeulizwa Kiswahili angeweza kujibu vizuri zaidi, lakini pia, to be fair, inawezekana anajua Kiingereza ila yuko slow, anahitaji muda wa kulitafsiri swali kutoka Kiingereza na kuliweka katika Kiswahili, halafu kulijibu katika Kikwahili kichwani, halafu kutafsiri kutoka Kiswahili kichwani kwenda Kiingereza halafu kujibu kwa kiingereza. ukimsikiliza utaona kuwa ingawa ni kweli Kikwete hawezi ku "think on his feet" na anaboronga, lakini typically style ya Kikwete ni kuanza kwa kuboronga boronga halafu kadiri anavyoendelea anayapanga mawazo yake vizuri, halafu katikati ya kuboronga atasema kitu kitakacho contradict kuboronga kwake -sometimes brilliant- halafu ukimpa muda anamalizia vizuri tu.

Case in point aliulizwa, kwa kiswahili kutoka kwa mtanzania katika hadhira friendly ya Watanzania hapo 42nd St NY,NY, kuhusu uwezekano wa watanzania walio nje kutumia channels za serikali kuwasaidia watu nyumbani. Akaanza kuongea very unpresidential, "mna hela nyinyi? Au mnataka kulaumiana tu?" baadaye sijui akajishtukia anachemsha and this was not in line with building the spirit of patriotism and love of country and folk, akabadili tune, akamalizia vizuri kwa kusema kuna njia nyingi tu za kusaidia, na ukitaka kusaidia unaanza na walio karibu yako, kama familia na kama unataka kusaidia zaidi unaweza kutumia njia zisizo za kiserikali, kawa ameongea doctrine ya serikali kutojihusisha na biashara, akawa ame encourage patriotism na love of country and folk at one go, lakini alianza kama anakunywa kahawa Saigoni vile.

Lakini hii style tunaiweza wenyewe watanzania katika media zetu, media mabazo rais akiulizwa swali analijibu kwa speech ya nusu saa. katika media ya kimataifa ambapo kila neno ni soundbyte Kiwete anaonekana mtupu, hata ukisikiliza huyu binti alivyomuuliza Kikwete, wakati huyu binti anaendelea kwa Waziri wa South Afrika kwa kweli alikuwa amemkatisha Kikwete, ni kama vile Kikwete alikuwa ana warm up tu na ndiyo kwanza anataka kuanza kujibu, huyu dada akaendelea mbele.

Alipoanza kujibu alikosa kulielewa swali, akawa anaelezea mambo basic kabisa ya investment kama vile fiscal incentive (sasa unafikiri investor anakuja nchini kwako kueneza injili, this is a no brainer na inaonyesha Kikwete hawezi kufikiri kwa haraka) mambo ya workshop na investment opportunity blah blah, hapo huyu dada akamshtukia jamaa hana analosema, akamuuliza tunajua hayo yanafanywa kote na nyie mmekuwa mnayafanya, tuambie unafanya nini tofauti.

Kikwete kashindwa kujibu, quite frankly inawezekana ndiyo mara ya kwanza anasikia mtu anamuuliza hili swali.This type of thinking is very western na sisi hatuko fast kiasi hiki, ndiyo kwanza tunaanza kuamka kwamba kuna financial crisis, wewe unatuuliza tunafanya nini differently? Of course Kikwete kamwambia we are doing nothing differently (and expect to be successful right?). Kwa kifupi kwa watu wanaofuatilia mambo dada kamuumbua mzee mzima, kwa sababu katika maneno yote aliyotakiwa kusema Kikwete hakutakiwa kusema we are not doing anything differently, angeweza hata kusema, kwa ukweli kabisa, kwamba jamani eeh, hii tafrani kubwa sana na hivi sasa ndiyo tunakaa sawa na tunajadiliana tufanyeje, na ndiyo moja ya sababu ya mkutano huu, anarudisha swali kwenye hadhira.Actually hiki ndicho alichofanya yule Waziri wa South Africa. All politicians all full of it, but some know how to cover it and sell it, Kikwete does not.Huyu bwana wa South Africa naye hakuwa na jibu, probably kwa sababu hii hii ya Kikwete, na wao ndio kwanza wanaamka, lakini yeye alijua kujibu, halafu hakuwa na tatizo la lugha, akawa anaflow sijui restructuring, sijui labor, sijui tough decisions, mwishowe akaona isiwe tabu, nishadanganya sana kwamba najua tunachofanya ngoja niwe mkweli tu kwani honesty is the best policy, na kama mtu atataka kunishtaki kwamba nimedanganya always nitaweza kusema mbona hapa mwisho nilisema ukweli? Akasema "we are still feeling our way through" translation, we dont know jack, we are just findiong out what to do now.

Kwa hiyo Kikwete anapoongea na media za kimataifa inabidi ajue kuwa watangazaji nao wana reputations zao za ku protect, na wakishagundua kwamba wewe huna nyimbo wanaku skip, ndiyo maana ingawa Kikwete na Waziri wa South Africa wote walikuwa wana bluff, lakini Kikwete alipewa air time ndogo sana kulinganisha na yule waziri wa South Africa, kwa sababu hajui ku bluff, dada wa watu akaona isiwe taabu bure, nisije kumuaibisha baba wa watu kesho nikatengeneza headline "Kikwete akiri serikali haifanyi chochote kipya kuhusu janga la uchumi". akaona heri lawama kuliko fedheha, akamkatisha, watu weeeeeeeee.

Labda angepewa dakika chache za kusema zidumu fikra za mwenyekiti, Kikwete angeweza kujieleza vizuri.
 
Last edited:
Knowledge is the Power

Kuna umuhimu pia wa curriculum za shule zetu kubadilishwa kwa sababu huwa tunasoma ili kufaulu mitihani kwa kutumia uwezo wa kukaririri (cramming) na si kusoma kupata uelewa ili uweze kung'amua mambo zaidi.
 
Nimejaribu kufuatilia na kusikiliza majibu ya Rais; aliposema tunatengeneza "brochure" I had to go get me a Coke.!
 
hapana poor communication skills ni sawa tu na tatizo la lugha ambavyo sidhani ndio tatizo la Kikwete.

Hapa tatizo kubwa ni uelewa wa Kikwete katika mambo mbalimbali yanayohusiana na uchumi na njia mbalimbali mbadala ambazo yeye kama kiongozi anaweza kuzitumia kuhakikisha Taifa haliingii katika janga hili la kiuchumi au kuweza kulitoa taifa katika janga hilo.


Ok uwezo wake wa kuelewa ni mdogo ndiyo lakini suala langu ni kwamba si ana washauri...kwani nini maana ya washauri si kumsaidia raisi kumpa ushauri mzuri katika nyanda mbali mbali.... so wao wanafanya nini?...
 
just curious wakuu:hivi rais angekuwa sumaye tena kabla hajaenda havard kwenye mijadala kama hii ingekuwaje??
 
Wakuu,
jamani twende mbele huku tukitazama nyuma.. Kikwete amechemsha na amechemsha sio kwa sababu ya kujua jibu la kusema isipokuwa hakuona ndani kabisa.. Na wala msijaribu kumpa sifa Mkapa kuwa angeweza kusema vizuri...
Tatizo hapa ni kwamba unafanya nini ama una mkakati gani dhidi ya hali mbaya ya Kiuchumi duniani..Bongo hatufanyi kitu, hatufahamu nini kinachotokea na wala hatuoni ndani zaidi ya kusoma vitabuni..

Jibu la swali la bibie Aisha ni kwamba Tanzania hatufanyi kitu na wala hatuna mkakati wowote kujiandaa na hali hii...sasa huyo Mkapa angesema vizuri kitu gani hapa..Kama kuna mtu atanimbia ingekuwa Mkapa, angekwisha andaa mkakati huu au ule kupambana na hali mbaya ya uchumi ningemsikia na pengine jibu lingekuwa rahisi..
Ni Mkapa huyu huyu aliyewafuata IMF mara ya kwanza kwa sababu hakuona ndani kabisa... Na alipingana na wachumi wengi nchini ikiwa ni pamoja na kina Dr. Mwapachu..hivyo uwezo wa kujibu swali kama huna mbinu ni Ujinga mwingne..

Kikwete amechemsha kwa sababu hakuna alofanya wala hajui afanye nini na hii yoite inategemea na ELIMU tuliyopewa.. Kila kitu tunategemea mzungu aje kutufanyia na Kikwete amedhihirisha wazi kwamba Tanzania bado kabisa inaihitaji IMF kutupangia mikakati hata kama ni ya kutumaliza...
By the way, Kipapi kimesimama!..huyu Aisha mbongo au? haaa haa haa!
 
Back
Top Bottom