KWELI Isaac Mnurwa akamatwa kwa tuhuma za kusambaza video ya Rais Samia akiwa na Peter Greenberg

KWELI Isaac Mnurwa akamatwa kwa tuhuma za kusambaza video ya Rais Samia akiwa na Peter Greenberg

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Inadaiwa kuwa kijana Isaac Mnurwa amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma zinazodaiwa ni kusambaza video ya Rais Samia akiwa na Peter Greenberg.

Tunaomba kufahamu ukweli wa taarifa hii.

1657978076728.png
 
Tunachokijua
Mei 12, 2022, taarifa za kukamatwa kwa Isaac Mnurwa zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Isaac Mnurwa alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchafua Rais Samia Suluhu Hassan kwa ku ‘like’ na kushiriki kusambaza video fupi ambayo ni kipande cha filamu ya Royal Tour inayomuonesha Rais Samia Suluhu akiwa na Peter Greenberg.

Peter Greenberg ni mwanahabari kutoka kituo cha televisheni cha CNBC cha nchini Marekani aliyeongoza utengenezaji wa filamu ya Royal Tour iliyotengenezwa kutangaza utalii wa Tanzania ambapo Rais Samia alikuwa ni sehemu ya filamu hiyo.

Ukweli ni kwamba kijana huyo alikamatwa na polisi tangu Mwezi Mei 2022 na alishikiliwa katika kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam. Aliachwa huru kwa dhamana na baada ya kuachwa huru, alipewa utaratibu wa kuripoti kituoni hapo mara kwa mara.

Hata hivyo, hakuna shtaka lolote lililofunguliwa na dhidi yake.
Back
Top Bottom