Isaka alitajirika ndani ya mwaka mmoja jifunze nini alifanya

Isaka alitajirika ndani ya mwaka mmoja jifunze nini alifanya

STONES 12

Member
Joined
Jan 3, 2025
Posts
16
Reaction score
20
Habari zenu wapendwa
Tukisoma kitabu Cha mwanzo biblia inatuambia Isaka akiwa katika nchi ya wafilisti gerari huko alipanda mbegu kila kilo moja ya mbegu aliyoipanda alipata kilo mia za mavuno
Biblia inamzungumzia Isaka ndiye Aliyestawi zaidi katika nchi Ile kuliko wote

Mwanzo 26:12
Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA akambariki.
Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng’ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.

Nini alifanya Isaka ?
Mungu akambariki ndani ya mwaka mmoja akawa na mali nyingi

Jibu ni hili Isaka alitoa sadaka ya kupanda mbegu kabla ya kuingia shambani wakulima wengine hawakufanya hivyo
Hili jambo lipo kiasili ni lazima utoe ili upate Mungu atakupa maelekezo Nini ufanye kuanzia mwanzo wa kazi yako ardhi ipi Ulime? ili upate mazao mengi

Nini tunajifunza kwa baraka ambazo Mungu anatoa ni kwamba ukitoa sadaka ya kupanda mbegu ni haki yako kupata mavuno makubwa
Faida ya Sadaka hii Mungu anaanza kukubariki kwa baraka za rohoni tayari unakuwa unajua Nini unachoenda kukifanya

2 Wakorintho 9:6-7
Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
ila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

Isaka alitumia rasilimali ardhi kupata mavuno makubwa kwa kila kilo moja ya mbegu alipata mavuno kilo mia 1×100

Tumia rasilimali watu kupata utajiri ndani ya mwaka huu mmoja ni haki yako kutajirika ni jambo rahisi zingatia mali iwe kwenye daftari andika mpango wa biashara Nini unachotaka kukipata mwaka huu

Ukitaka kujua faida utayopata kwenye biashara kila mali uliyoiweka dukani kwako piga hesabu kwamba hiyo bidhaa moja au katoni utauza kwa watu mia
Chukulia mfano dukani kwako unabidhaa 100 kwa watu 100 utakuwa umeshajua utauza katoni ngapi utauza bei gani faida utazipata kiasi gani mwaka mzima

Jifunze pia hii
 
sijaona mstari isaka anatoq sadaka ya mbegu. Tuwe makini tusijepotosha mqandiko.

Isaka qlirithi. Isaka alikuwa na kibali cha Mungu hivyo kila alichogusa kilifanikiwa kwa wepesi.
Mambo ya sadaka hayana uhusiano na mafanikio ya Isaka. Sipingi sadaka tutatoa ila kusema kupanda mbegu ndio sadaka ni uongo.
 
Kasome mwanzo 26 yote Nini kilitokea utaona ilivyotokea njaa lakini Mungu alimpa maelekezo Isaka asiende misri abaki pale kwa wafilisti
 
Kasome mwanzo 26 yote Nini kilitokea utaona ilivyotokea njaa lakini Mungu alimpa maelekezo Isaka asiende misri abaki pale kwa wafilisti
Hujaweka mstari unaoonyesha isaka alitoa sadaka kabla ya kupanda mbegu. Maana kiini cha mada ni sadaka nilitegemea mstari kiini uwepo kwenye mada sio mimi kuutafuta pembeni mkuu.
 
Hujaweka mstari unaoonyesha isaka alitoa sadaka kabla ya kupanda mbegu. Maana kiini cha mada ni sadaka nilitegemea mstari kiini uwepo kwenye mada sio mimi kuutafuta pembeni mkuu.
Baraka ambazo Mungu alimbariki Isaka ni sababu ya agano aliloliweka na baba yake ibrahimu sisi wakristo agano letu ni damu Yesu uzao wa ibrahimu lakini nikuulize swali Kuna agano linalofanyika bila kutoa sadaka?
Yani unaweza kwenda kanisani ukaomba kubarikiwa bila kutoa sadaka?
Jibu hili limekuja kujibiwa katika 2 wakorintho 9:6
 
Sadaka ni ibada. Isaka alitoa sadaka kama Baba yake.
Ila kupanda zile mbegu sio sadaka.
Hapo ndio nilikiwa nawasiwasi napp tu. Mambo ya kupanda sadaka ni mapokeo.
 
Back
Top Bottom