Mkweli toka moyoni
1) Atakutafuta na kuongea na wewe mara nyingi kwa kadri atakavyoweza. Hii inawezekana kwa njia ya simu, email, barua, au hata kutuma salamu za mdomo kupitia watu wengine kama marafiki, ndugu na jamaa.
2) Atatimiza ahadi aliyokupa. Akisema atakutafuta kwa ajiri ya maongezi, kukupigia simu au ahadi nyingine yoyote atafanya hivyo kwa muda aliousema awali
3) Ataonyesha kujali kwa mambo unayoyapenda, kwa mfano kama unapenda kwenda muziki, filamu, aina fulani ya chakula, maua, au mambo mengine unayoyapenda ataungana na wewe ktk kufurahi hata kama itatokea kati ya mambo hayo sio hobi yake
4) Mwanaume wa aina hiyo atakuwa wazi kuonyesha hisia zake kwako, atakuwa wazi kwa kadri awezavyo, hii itakuwa ni pamoja na kukueleza jinsi gani anajisikia anapokuwa karibu na wewe
5) Atakufunza utamaduni wa kujenga urafiki wenye dhamira ya dhati, matumaini ya muungano imara na usiokuwa na tamati kati yenu na ukweli halisi pendo toka moyoni
Aliyekosa ukweli
1) Mwanaume asiyekuwa na nia kwanza atakuwa mgumu kutimiza ahadi alizotoa mwenyewe kwako, atakuwa na sababu nyingi na maelezo marefu yasiyolenga kukutia moyo wala nguvu
2) Wakati mwingine atakuwa mbali na wewe, hatopenda kuongea na wewe kwa kirefu, na akilazimika kuongea atafanya hivyo kwa muda mfupi tu na kukupa sababu kedekede kwanini hapaswi kuongea muda mrefu
3) Anaweza kukuambia atakuja muda fulani lakin asifanye hivyo na bado asikueleze sababu za kushindwa kuja kwake kama hutosumbuka kumuuliza
.