Ishara kuwa ulishaukwaa ila ngwengwe ikala besela

Ishara kuwa ulishaukwaa ila ngwengwe ikala besela

Last month nilipima ngoma kimasihara, nikakuta nipo sawa. Nikakaa kikao na kichwa changu tukakubaliana kupiga chini mademu wote na kubaki na mmoja tu mwenye malengo. Naye akapimwa
 
Ukipata ngoma jua kabisa wew kinga zako ni babakasa
Umeme ukishaingia mwilini haunaga cha bingwa chamsingi tutumie kinga kwa usahihi kwa kila tendo lakini la muhimu zaidi ni usafi usikubali hata siku moja kufanya ngono katika chumba cha guest bubu isiyo na choo na bafu humo humo ndani.

Tena kwa mwanaume geuza utaratibu huu uwe kwako ni wajibu kila baada ya kupizi wahi bafuni nawa kwa sabuni na maji mengi lakini usisahau kunywa maji mengi kila wakati kuruhusu kupata haja ndogo itakayokusaidia kila mara kuondosha vimelea vya magonjwa katika njia ya mkojo unapoenda kukojoa.

(Siyo unabugia bia za 20k afu unaona hasara kujinunulia walahu kopo 2 za lita 1.5 zitakazousaidia mwili pakubwa kuliko hata hizo pakiti zako tatu za Zana ulizouziwa buku na mama ghetto)[emoji23]

Pili jifutie nguo kavu na safi kila mara na usishee na mwezi wako taulo kwa kisingizio cha nafanya naye hivyo haina shida (ni vyema kujijengea kasumba ya kutembea na kibegi kidogo kwa ajili ya kujibebea nguo za ziada)

na wakati mmelala pamoja usiruhusu mgusano wenye unyevunyevu au mazingira hatarishi ni bora kuvaa boksa safi na ukamkumbatia mkalala kwani zikikupanda kuvua hiyo boxer inakuchukua muda gani..hivyo tuwe makini na afya zetu hakuna atakayekuja kutukumbusha juu ya hilo zaidi yetu.
 
Kuna watu hawaamini mpaka leo kuwa ngoma ni ugonjwa dhaifu kama magonjwa mengine pindi unapoingia mwilini kwa mara ya kwanza.

Ikiwa mwili wako ni mwili wenye kinga imara ambayo inaweza kupambana vyema na vijidudu vya maradhi. Na ikiwa wewe ni muumini mzuri wa ngono zembe na mpaka muda huu uko salama usijione wewe ni mwamba bali tambua kuwa umeshawahi kuukwaa mara kadhaa ila shukuru kinga za mwili wako kwa kukupambania vyema.

Zifuatazo ni dalili kuwa umeukwaa tiyari ila mwili unapambana na hali kukuepusha na majanga; dalili hizi utokea siku moja baada ya tendo lisilo salama na kama ukitoboa siku 4 na ukaona zimetoweka jua kuna usalama ila ukiona siku zinayoyoma na hatimaye wiki, wiki mbili hadi mwezi, my friend jua kuna asilimia kubwa gari limeshawaka na huko tiyari kwenye hatua ya kwanza.

Dalili mojawapo inayowapata wengi ni uchovu wa mwili mzima na wakati mwingine kuisi maumivu kiasi ya viungo, mafua,kuwashwa na ngozi na kutokewa na vipele mara nyingi katika mikono au usoni na mgongoni, homa, kichwa kuuma, tezi za kwenye taya au chini ya shingo kuvimba n.k

Ukiona dalili hizo hapo hata kama ulitumia kinga, au kwenye njia yako ya mkojo waona mambo yako freshi UTI na gono hawajakutembelea, wewe jua tu kirusi kimo tiyari ila kupitia mapambano ya siku hizo 4 za moto yakiamuliwa vizuri moto unazimwa na utaendelea kudunda ila jeshi la zimamoto likizidiwa ndiyo basi tena utaendelea kuteketea hadi mwisho.

Kama una kale karoho kepesi ukishaona ulikopita sipo na ni siku ya pili au ya tatu haijatamatika tokea ulipotoka kutenda dhambi na hali yako ya kiafya uielewi-elewi chakukushauri wahi matibabu hospitalini ukapewe vidonge vya kuzuia maambukizi (PEP)kabla hayajaisha masaa 72 (siku 3), sasa zubaa uzikwe.

#tunakumbushana tu kuwa UKIMWI bado upo chezeni salama.

#...kuutibu ni gharama iweje uupate kwa bure..#Stamina.
'kumbuka mpira usije ukaleta drama hapa hakuna demu wa kwenda nae nyama kwa nyama'.....hii vesi sijui ipo kwenye ngoma gani ya bongo fleva!
 
Mwishoni ungeandika -TUACHE UZINZI
Hii ni ngumu kumeza licha ya kuandikiwa mpaka kwenye amri kuu za agano lile la kale tumeshindwa kuacha na tunazidi kuteketea ni vyema kupeana mbinu za kivita kuepuka walahu majanga kidogo maana kwa hali iliyopo tunaelekea kupoteza taifa kwa maana kasi ya maambukizi ni kubwa mno.
 
Umeme ukishaingia mwilini haunaga cha bingwa chamsingi tutumie kinga kwa usahihi kwa kila tendo lakini la muhimu zaidi ni usafi usikubali hata siku moja kufanya ngono katika chumba cha guest bubu isiyo na choo na bafu humo humo ndani.

Tena kwa mwanaume geuza utaratibu huu uwe kwako ni wajibu kila baada ya kupizi wahi bafuni nawa kwa sabuni na maji mengi lakini usisahau kunywa maji mengi kila wakati kuruhusu kupata haja ndogo itakayokusaidia kila mara kuondosha vimelea vya magonjwa katika njia ya mkojo unapoenda kukojoa.

(Siyo unabugia bia za 20k afu unaona hasara kujinunulia walahu kopo 2 za lita 1.5 zitakazousaidia mwili pakubwa kuliko hata hizo pakiti zako tatu za Zana ulizouziwa buku na mama ghetto)[emoji23]

Pili jifutie nguo kavu na safi kila mara na usishee na mwezi wako taulo kwa kisingizio cha nafanya naye hivyo haina shida (ni vyema kujijengea kasumba ya kutembea na kibegi kidogo kwa ajili ya kujibebea nguo za ziada)

na wakati mmelala pamoja usiruhusu mgusano wenye unyevunyevu au mazingira hatarishi ni bora kuvaa boksa safi na ukamkumbatia mkalala kwani zikikupanda kuvua hiyo boxer inakuchukua muda gani..hivyo tuwe makini na afya zetu hakuna atakayekuja kutukumbusha juu ya hilo zaidi yetu.
Utafanya yote hayoo ila umemla denda (mate).. umetumia kondom kama 20 hivi na hizo kanuni zako za kunywa maji lita 50 etc.. then anakuja kukupatia Hep.B

Haya mambo hayana formula.. tena ukijifanya mzee wa Safety ndio utaukoga mapema.. watu wengi sana wanaojifanya waangalifu hao ndio wanavagaa/kuyabananga.
 
Back
Top Bottom