Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
- Thread starter
- #41
Una uhakika gani kuwa kinga za mwili wako huwa hazijitetei kwanza mbele ya HIV na kuna wakati unashinda?Ni uongo nakataa...Ukimwi haujaribu ukinasa umenasa mkuu
Je maishani mwako unahisi umeshalala na watu wangapi wenye virusi pasipo wewe kufahamu au unahisi ni kwa bahati tu we ni mzima?
Unachopaswa kujua ni kuwa vile virusi katika ile hatua yake ya mwanzo kabla havijaanza kubadilika-badilika na kuwa sugu huwa ni kama virusi vya kawaida mfano wa mafua iletayo homa na uchovu wa mwili,
na endapo kinga zikiwa imara huwa zinapewa mkong'oto ndani ya siku chache na mambo yanakuwa sawa ila ziki-resist sana ndiyo inakuwa ntolee...
Kingine virusi navyo huwa vinatofautiana nguvu au makali kulingana na aina yake na afya ya mgonjwa anayekuambukiza ikiwa ni kutoka kwa yule anayevifubaza sana kwa ARVs basi unaweza hata usiambukizwe licha ya kufanya ngono isiyo salama.
Balaa ni kwa wale wasiotumia ARVs kabisa,wanaotumia kwa kubipu, wenye aina ya virus kali na waenezaji wa makusudi au cha ngono hao ukikumbana nao chance ya kutoka salama huwa ni asilimia ndogo sana.