Heri ya mwaka mpya ndugu zangu wakijiji, Mungu ni mwema ametupa neema ya mwaka 2023 ni mwaka mwingine ya zamani yamepita acha kutembea na fikra za 2022. Nirudi kwenye mada husika......
Maandiko yametuasa wanaume tuishi na wanawake kwa akili, ndoa na mahusiano ya sasa yamekuwa na changamoto sana hata kufikia wengine kuona na kusema ndoa ni jehanamu kwasababu ya wanaume kuto tumia akili, yes namaanisha ukiona mahusiano yanakusumbua ukweli ni kwamba hautumii AKILI.
Wazee wetu walioa wanawake zaidi ya mmoja na hao wake waliishi vizuri Kwa sababu wazee wetu walitumia akili, usijesema eti wanawake wa miaka ya nyuma hawakusoma, eti hawakuwa wasumbufu hapana ni akili tuu.
Tuanzie hapa, mwanaume unajua fika na kwa mifano unaona kuwa mwanamke akikuzidi kipato atakusumbua lakini bado unataka hao hao waliokuzidi kipato kwa kuwa anakupa kupa Hela na ukajiliwaza kwamba aah huyu hana shida maisha yakisonga mbele akaanza kuonyesha rangi zake unaanza kulalamika Tena!
Mwanaume unajua na unaelewa kabisa kuwa mwanamke aliyekuzidi elimu ni changamoto huwezi ukamwambia jambo bila kubisha na kukuona huelewi mambo kitu ambacho Kwa mwanaume ni dharau lakini for the sake of mbunye unajichomeka huko, halafu unarudi kuanza kusumbua wananzengo
Mwanaume unajua kabisa na unaelewa kabisa mwanamke akikuzidi umri ni tatizo lakini mwanaume umekomaa eti age is just a number, unafikiri akikunyima mbususu utamfanyaje zaidi utakuja kulia lia, na ujue ni aibu mambo mengine kueleza kwa mashemeji eti mke wangu ananinyima au kwa pasta au sijui baba paroko, matokeo yake utatafuta mchepuko na mchepuko akuwekee dawa uwatese wanao for the sake of mbususu.
Mwanaume lazima utambue Kuna mambo kwenye ndoa unayatolea uamuzi sio kila jambo unamsikiliza mkeo, Adamu alimsikiliza Eva likawa anguko, Samson alimsikiliza Delila tunajua kilichotokea, Anania akamsikiliza Safira tunajua kilichotokea, wanawake wanapenda na kutamani kufanya kile mume alichosema, ukiona mke anafanya jambo bila kupata ruhusa kwako ujue Kuna mahali uliuza akili yako, mwanamke anapanga tu safari bila kukwambia lazima Kuna mahali umekwama, sio kila jambo unaweka democracy hayo mambo hayapo hivyo, mwanamke anabadilika kulingana na mazingira.
Mwanaume mwenzangu tambua huwezi kumbadilisha mwanamke tabia ambaye umekutana naye ukubwani ondoa hiyo dhana, tabia zingine ni malezi aliyolelewa, Sasa unakutana na Binti anamiaka 25, utambadilishaje tabia?? Wengine ni wachoyo, kiburi cha asili, wengine wana asili ya uchawi hivyo Kuna kile kiburi cha kichawi, unapokuwa umepata mchumba jitahidi basi kufuatilia historia yake ya nyuma hiyo ni kwa ajili yako mwenyewe.
Mwanaume kumbuka Director wa ndoa ni mwanaume sio mwanamke ukimpa usukani mwanamke imekula kwako, mwanaume ndio anaamua tutaishi wapi, wanangu watasoma wapi, wataishi maisha gani, hiyo itafanya mwanamke arudi kwenyw nafasi yake ya kutunza na kulea familia ndilo jukumu lake la asili.
Mwanaume lazima ujue mkeo anapenda vitu gani hii hurahisisha hata mnapokwaruzana kuyamaliza kiurahisi wenyewe Kwa wenyewe, kuliko kila jambo wewe unalipeleka Kwa wananzengo, hajakuwekea maji ya moto tu, wewe unakimbilia Kwa wananzengo
Mwanume usijekuona mkeo ni malaika kwamba hawezi kuchepuka utajidanganya bure, ni binadamu huyo Kuna mahal anaweza teleza, usiifanye kuwa big deal sana, wala usijione una haki sana ya kummiliki mmekutana ukubwani huyo, ndio maana wazee wa zamani ukikamatwa na mke wa mtu unalipishwa tu ng'ombe halafu mwenye mke anaamua kuendelea naye au kumuacha, sasa wewe unaumiaaa mpaka unataka kujitoa roho for the sake of mbususu?
Vijana mnaotaka kuoa tafuta mwanamke wa saizi Yako unayemmudu kulingana na uwezo wako, wanawake wote wanapenda pesa, usijidanganye kuwa nataka asiyependa pesa hautampata labda sema asiyeomba pesa nyingi, na asiye ombaomba, sio unataka pisi Kali maarufu wakat huna laki ya karibu utajiumiza bure niishie hapo
#TUISHI NAO KWA AKILI#