carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara, Isihaka Mchinjita, amesema mazingira ya sasa nchini si rafiki kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani kutekeleza majukumu yao ya kisiasa.
Akizungumza na Royal TV Plus, Mchinjita pia amedai kuwa mifumo ya uchaguzi nchini haijajengwa katika misingi ya uhuru na haki, akisema hali hiyo imeongeza wito wa kufanyika kwa mabadiliko ya kweli, yakiwemo upatikanaji wa Katiba Mpya na mifumo imara ya uchaguzi inayohakikisha ushindani wa haki.
Mchinjita amedai kuwa baadhi ya watu wanaotetea maslahi ya wananchi wamekimbilia nje ya nchi, wengine wako mahabusu au gerezani wakikabiliwa na kesi mbalimbali za jinai, huku wengine wakichagua kukaa kimya kutokana na mazingira yaliyopo.
Amesema jukumu la kiongozi wa kisiasa ni kusimamia maslahi ya wananchi kwa vitendo, ikiwemo kufuatilia utekelezaji wa mipango ya viongozi walioko madarakani, kubainisha mapungufu na kuwasilisha ajenda mbadala zinazoweza kuboresha maisha ya wananchi.
Ameongeza kuwa viongozi wa upinzani wanapaswa kueleza namna wanavyoweza kutatua changamoto zilizopo endapo watapewa nafasi ya kuongoza, badala ya kuishia kukosoa pekee.
Chanzo : Royal Tv