Kitendo cha Tanzania kubaki kuwa na amani ya hali ya juu katikati ya msitu WA fujo na ukosefu wa usalama ni dalili tosha kwamba vyombo vyetu ni imara.
Kenya nchi moja tu ya Somalia kati ya nchi zinazowazunguka, ilipoingia katika machafuko, mumeshindwa kuidhibiti hiyo hali, matokeo yake mkajiingia kwa kushindwa kuwa na intelligence nzuri katika vyombo vyenu kujua kwamba kwa kwenda Somalia hali ya amani ingezidi kuchafuka hapo Kenya.
Mara nyingi sana kumejitokeza vitendo vya kigaidi hapa Tanzania, kuanzia katika mapango ya Ambani, Kibiti, Mwanza na kule Arusha, lakini POLISI na JWTZ haraka Sana wameweza kudhibiti hiyo hali kwa ufanisi mkubwa sana, kabla havijawa " out of control".
Mfano mzuri no jinsi walivyodhibiti ujambazi hapa nchini. Kuanzia miaka ya 1998, baadhi ya majambazi toka Kenya walijaribu kuja Tanzania kufanya ujambazi, nadhani kilichowakuta bado tunakumbuka, au watu waliokuwa wanajishughulisha kuwauwa albinos, kilichowakuta tunafahamu vizuri, siku hizi ni historia kuhusu mauaji ya albino.