Wapi katajwa Mohamed Said? Badala yake nimeeleza 'tumeelekeza..' nikimaanisha sisi. please acheni spinning.
Kuna kitu kinaitwa Paranoia( heavily influenced by anxiety or fear, fear of unknown n.k ) samahani kukuingiza anga kama hizo.Ulipotaja 'kupata kipato kupitia machapisho yao' ni kina nani hao kama hukumkusudia huyu mzee ambaye ndie aliyeandika historia ya wazee wetu? Kuna sehemu hapo juu umesema sisi tunajadili FRUSTRATION za Mohamedi said kama sio dharau na dhihaka ulikusudia nini?
Ulipotaja 'kupata kipato kupitia machapisho yao' ni kina nani hao kama hukumkusudia huyu mzee ambaye ndie aliyeandika historia ya wazee wetu? Kuna sehemu hapo juu umesema sisi tunajadili FRUSTRATION za Mohamedi said kama sio dharau na dhihaka ulikusudia nini?
Al.murad CHAMVIGA huyu kijana Nguruvi3 amekuwa akirusha rusha kashfa kama wale kina dada wa uswahilini! Kavaa kanga moja halafu natoa kichwa dirishani, anasema ovyo akiulizwa anasema "kwani umeskia nimetaja jina mie" mnikome babu ee!!
Kijana anaonekana amekulia kama sio kigogo! Basi tandika mikoroshoni pale!
Manake kule kuna wanafiki kama siafu!
Teh teh teh teh!
Nguruvi,
Sipendi kusema hili kwa sababu zilizo wazi nahofia watu kusema najipendekeza.
Huyo bi mkubwa unaemtaja ni mama yetu.
Namuheshimu kama mama yangu huenda ikawa kasahau maana ni miaka mingi
imepita...
Aklijuana kwa karibu sana na mama zetu akina Bi Bahia, Mwalimu Sakina, Tatu
biti Mzee, Bi Halima, Bi Mahunda, Hawa biti Maftah na wengine wengi...
Wengi katika hawa wametangulia mbele ya haki.
Mimi naandika na nataka nisomwe.
Nikiandika matusi au maneno ya ovyo wasomaji watanipuuza na kunidharau.
Hata wewe hutopenda kufanya mnakasha na mie kwa kuhofu kuvunjiwa heshima
yako.
Lakini kubwa kabisa mimi nimekwenda kumbini na pia nimefunzwa adabu na mama
yangu.
Zaidi ni Muislam nimefundishwa kuwa kama sina jema la kusema nikae kimya.
Ondoa hofu utasoma maneno ya kijenga historia ya nchi yetu hutosoma karaha labda
kama utakarihika kusikia nasema habari hizi kanieleza shangazi yangu Bi. Sikudhani biti
Salum wa Temeke.
Ngoja tuagane kwa hii.
Siku shangazi yangu kaolewa pale Kirk Street nyumba ya mumewe ilikuwa inatazamana
na nyumba ya Bi Mluguru biti Musa mama yake Abdu Sykes.
Katika kusherehekea harusi Abdu Sykes akatoa bastola yake akawa anapiga risasi juu.
Bi. Mluguru alikasirika sana maana alikuwa anaona kuwa lile ni jambo la hatari na kwa hakika
ile bastola siku nyingi ikimkera sana.
Aliivizia alipoipata siku moja akaitupa chooni.
Mkasa huu kanihadithia baba yangu.
Kuhusu kuwa nimesema Nyerere kaomba nk. nk. unanisingizia na wala sitakupa changamoto
kuwa ulete ushahidi wala sitajitetea.
Maandishi yangu yanajitosheleza.
Ubishi haujengi tuko hapa kubadilishana fikra na si lazima tukubaliane.
Nadhani wa kutulizana kwa hili ni wewe.
Uliowataja hawatakuja huko kwasabab wamekaa kidini dini.they can't see outside the box.
Salaam Sheikh Mohamed Said,
Wallahi nimefurahi kusoma hiko kisa cha Bi. Mluguru
Kwa hakika ni kisa kilojaa hikma na mafunzo ndani yake!
Allah akupe umri mrefu na akuepushe na wale wote wasio kutakia mema!
Muda wangu haunitoshi kwa sasa, lakini na ahidi kurejea na kuandika kila nitakapo jaaliwa!
Inshallah Mwenyezi Mungu atulipe sote kwa yaliyo mema!
Hiyo ndiyo tofauti.Sioni tofauti ya hii thread na ya hiyo nyingine alioifungua isipokuwa tu, hii inalenga waislamu na ile nyingine ni ya wote, it's too sad. Wanasema ukitaka kuwa moto kuwa moto, lakini huwezi kuwa moto na baridi pia. Sina ugomvi na mtu ila napenda kuwa na mawazo yasioegemea upande wowote ndio msingi wa kujenga ustawi wa jamii yoyote.
Wickama,
Mwenye kukasirika ana sherehesha zaidi?
Mwenyekukasirika anafanya kinyume chake na zaidi hapa jamvini wanasema
''anatoa povu.''
Mie si umeona nimekuongezea habari za babu yangu Shariff Mwamedi muuza
kuku pale Kariakoo 1950s na habari za mjomba wangu Bwana Hamisi Salum muuza
machungwa na embe?
Hivi hujatanabai kwa nini nimekuletea taarifa za watu hawa na kukuunganishia na
historia ya Baba wa Taifa?
Sawa Mzee MS,
Hebu tupumue kidogo. Utamu wa mnakasha ni kuulizana hata ambiguities. Huoni kama kuna a missing link? Walimnunulia baiskeli, mboga, kumpisha malazi, kumfundisha mavazi rasmi (kaptula-NO). What about cigarettes? Iam curious kujua ni wazee gani walikuwa staunch friends wa Julius lakini pia walikuwa smokers!!!! Haiwezekani kwamba kijiwe chote cha hawa wazee hakukuwa na smokers!!!! We know Julius was a confirmed smoker.
Tafadhali sheikh.
Sawa Mzee MS,
Hebu tupumue kidogo. Utamu wa mnakasha ni kuulizana hata ambiguities. Huoni kama kuna a missing link? Walimnunulia baiskeli, mboga, kumpisha malazi, kumfundisha mavazi rasmi (kaptula-NO). What about cigarettes? Iam curious kujua ni wazee gani walikuwa staunch friends wa Julius lakini pia walikuwa smokers!!!! Haiwezekani kwamba kijiwe chote cha hawa wazee hakukuwa na smokers!!!! We know Julius was a confirmed smoker.
Tafadhali sheikh.
Ulipotaja 'kupata kipato kupitia machapisho yao' ni kina nani hao kama hukumkusudia huyu mzee ambaye ndie aliyeandika historia ya wazee wetu? Kuna sehemu hapo juu umesema sisi tunajadili FRUSTRATION za Mohamedi said kama sio dharau na dhihaka ulikusudia nini?
sokwe mjadala huu hauna lengo la udini kwa maana ya kubagua! La hasha.Hapana kahtaan mkubwa, tukizungumzia wapigania uhuru basi tusiweke matabaka otherwise tunajenga chuki na ubaguzi kitu ambacho naona sio kizuri, nchi yetu Ina matatizo mengi sana, tunachekwa mkubwa kwa sisi tunaoishi nje, ninavyowaona mnakashifiana kwasabab tu ya Imani zenu inakatisha tamaa ndio naona ninyamaze kwani mijadala yenye milengo ya kidini huwa sishiriki, we are all one nation, brother and sister wakoloni wamefanikiwa sana kutugawa. na hatuwezi kuona nje ya hapo, ndio maana nawapenda wajapan hawataki kusikia habari za dini, mungu wao ni vichwa vyao.
Kuna kitu kinaitwa Paranoia( heavily influenced by anxiety or fear, fear of unknown n.k ) samahani kukuingiza anga kama hizo.
Wewe ni miongoni mwa watu wenye paranoia. Yaani kuandika machapisho basi ishakuwa Mohamed Said kwasababu yeye ndiye anaandika machapisho pekee duniani. Nimeeleza wazi kabisa 'Sisi tumeelekeza' nimeonyesha wamiliki wa sentensi ni sisi. Jamani labda tuongee Kiyemi au kiyunani maana hili linashangaza.
Kuhusu Frustration za Mohamed Said ni kweli Mohamed anazo hasa akiangalia kuwa historia haijaandikwa kama anavyojua yeye. Hata mimi ningekuwa na frustration! Fikiria Mshume amemlisha Nyerere na familia yake na kumpa pesa za kununua kitoweo ili asiende kuomba mboga, leo familia yake haijulikani hivi hiyo haitoshi kuleta frustration kweli!