Mag3,
Ukiwa unataka kumpambanisha
Cecil Matola na babu zangu haitakuwa haki.
Cecil Matola hakujaaliwa umri mrefu alikufa mwaka 1933 kwa hiyo hakufanya
mengi ukilinganisha na babu zangu.
Lakini mbona umemtaja Matola peke yake.
Vipi kuhusu
Mdachi Shariff na
Nichodemus Ubwe?
Lipo bandiko hapa JF katika kirago hiki hiki kuhusu
Kleist Sykes kama nilivyoandika
katika mradi wa Oxford na Harvard.
Angalia mchango wa
Kleist ambao ulikuja kuchukuliwa na wanae pale yeye alipokufa
mwaka 1949.
Kleist wanae wawili ni waasisi wa TANU.
Unataka nikupe habari za
Martin Kayamba?
Kwenye kitabu, ''Modern Tanzanians,'' Iliffe katika kuwajulisha wasomaji wake
Martin
Kayamba ni nani kamueleza kwa njia ya mfano tena katika ufunguzi kama kibaraka wa
Waingereza.
Sasa soma hapo chini usikie wenzake walikuwa wanamuonaje.
Katika kitabu changu hivi ndivyo nilivyomuandika
Martin Kayamba:
''In a cruel and cynical obituary on the death of
Martin Kayamba,
[1] Fiah lamented
that Africans did not benefit from
Kayambas education nor from his post as a clerk to
Assistant Chief Secretary.''
[2]
Yapo mengi ningependa uyajue kuhusu
Martin Kayamba.
Endela kunisoma hapa nilivyoweleza
Martin Kayamba katika kitabu changu:
''There was a very big difference between the Tanganyika Territory Civil Servants Association
(TTACA), founded in 1922 by
Martin Kayamba, and the Dockworkers Union, both in leadership
and in direction.
TTACA was a harmless genuine welfare association, free from any conflict with the colonial
administration.
It was a club for clerks and teachers, with newspapers and a football team, encouraged by
the government.'
[1]
Bado sijamalizana na wewe
Bwana Mag3.
Ukitaka kustarehe na
Martin Kayamba soma kitabu chake, ''The Autobiography of Martin Kayamba,
'The Story of
Martin Kayamba Mdumi, MBE, of the Bondei Tribe,'' katika Margery Perham, (ed)
Ten Africans, pp.175-272 uone jinsi babu yako anavyolamba viatu vya Waingereza.
Ukishasoma kitabu hiki rudi hapa jamvini nakusubiri.
Martin Kayamba mjukuu wa
Chief Kimweri.
Kimweri alikuwa Muislam.
Ludwig Krapf alipofika kwa
Chief Kimweri 1848 kamkuta Kimweri kastaarabika kavaa kanzu na kilemba yuko
katika mahakama yake anahukumu anajua kusoma na kuandika Kiarabu.
Hakuwa peke yake akijua kuandika.
Wanae na Waislam wengine Vuga na katika utawala wake wote walikuwa wameelimika.
Hasad ilimsonga roho
Krapf.
Alikuja kwenye ''dark continent'' kakuta mengine kabisa.
Uislam umeenea na watu wanajua kusoma na kuandika msingi wa kujifunza kusoma ni madras.
Wakoloni walipoichukua Tanganyika kitu cha kwanza ilikuwa kupiga marufuku hati za Kiarabu.
Kingine kilichofuata ni kuwaritadisha akina
Martin Kayamba.
Kayamba akawa Mzungu hata kumshinda Mwingereza mwenyewe.
Mwisho napenda kukufahamisha kuwa
Kleist Abdallah Sykes alizaliwa Muislam na kazikwa Kisutu Makaburi
ya Waislam.
Nitakuongezea kuhusu
Chief Kidaha.
Aliyeritadi kuingia Ukristo si yeye peke yake.
Mdogo wake
Hussein vilevile aliritadi.
Na hawa wote mimi nimeowaona.
Hussein alikuwa rafiki wa mmoja wa baba zangu.
Chief Kidaha aliritadi mwaka 1945.
Ukitaka kisa hiki sema nitakiweka hapa jamvini.
Nakunja jamvi kwa bashraf hii hapo chini.
Kama mwenye chuki na
Martin Kayamba si mimi bali ni John Iliffe aliyemwita Kibaraka.
Mwenye chuki ni
Erika Fiah aliyemwita kibaraka wa Waingereza tena kwenye taazia na kusema kuwa
kazi kubwa aliyoimudu
Martin Kayamba ni kufuga kuku Muheza baada ya kustaafu kazi.
[1] Iliffe, Tanzania Under British Rule in B.A. Ogot and J. Kieran (Eds)
Zamani:
A Survey of East African History, East African Publishing House, 1968 p. 22 quoted in
African Studies Working Paper No. 8, April, 1979, by G.W. Reeves.
[1] See Iliffe, The Spokesman: Martin Kayamba in Iliffe (Ed),
Modern Tanzanians,
op. cit. pp. 66-94.
[2]
Kwetu, 29 June, 1940.