jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,404
- 4,973
Ukweli siku zote utabaki kuwa hivyo. Historia ya nchi hii hata kama itakuwa distorted kiasi gani kuna siku ukweli utadhihiri. Maoni yangu ni kuwa bw. mohamed anachotanabahisha ni ukweli wa historia ya mapambano ya kudai uhuru wa tanganyika umepindishwa na anatoa ushahidi wa kuthibitisha asemayo.
Kwa wale walizaliwa miaka ya 50 wakirudisha kumbukumbu zao nyuma watakumbuka kwani lile vuguvugu la mapambano ya uhuru wa tz kwa wa wanadar [wa enzi hizo] ilikuwa siyo mchezo kwani ninakumbuka kuna mama mmoja muuza pombe hapa mjini alitoa ka akiba chake chote kusaidia safari ya nyerere un.
Hivyo basi hao ambao bw mohamed amewataja ni kweli kabisa walishiriki sana katika vita ya kudai uhuru wa nchi hii
Hakuna mtu anakataa kwamba walishiriki watu wengi katika kudai Uhuru. Hata SA walishiriki wengi zaidi ya Mandela. Lakini iko wazi kuwa walishiriki wakiwa kama watanganyika na si waislamu. Hizi habari za uislamu na uhuru zinatoka wapi? Harakati za kudai uhuru hazikufanywa na chama chochote cha kiislamu, bali TANU ya watu wote. Wao wenyewe ingawa ni waislamu hawakuliweka hilo mbele cha kushangaza leo hii watu wanaanza kuleta uislamu! Sasa kama dini ya wanaharakati wa uhuru ilikuwa ni uislamu what's the point? so what?