Mtu Mzima nadhani tumeeleza huko nyuma ya kuwa katika harakati za kupigania uhuru HUWEZI KUTENGANISHA IMANI ZA WALE WALIO HUSIKA! IWE NI WAKRISTO AU WAISLAMU! NA HUO UPIGANIAJI UHURU! Vipi utataja mikutano iliyofanyika kisiri ndani ya miskitini na makanisani bila kutaja uislamu na ukristo??
sasa basi hapa lengo sio kuonyesha kuwa waislamu ni mahodari kuliko wengine au ni wao tu walioshiriki ktk sakata lile LA HASHA!
Lengo kuu la uzi huu NI KUWEZA KUWATAMBUA NA KUWAENZI WAHUSIKA WOTE BILA KUBAGUA HATTA MMOJA!
Hapa utajiuliza kwa nini waislamu wanayasema haya!
Sababu kuu japo kuwa wengi wanaipinga na kuifungia macho ni namna Historia ya kweli ya nchi hii ilvyochakachuliwa na kitu kinachoitwa MFUMO KRISTO!.
Hii
Mtu Mzima kubali au kataa ni kitu kinacho ligawa taifa letu kila siku!
Katika historia ya nchi hii mara nyingi utakuta ili Cream of the crop inayotajwa basi 90% inahusishwa na UKRISTO! na hili limekuwa jambo la kawaida kabisa!
Mpaka kuingia ktk ofisi za serikali ukakuta picha ya Anaedaiwa kuwa mungu wa wakristo ukutani.
Ukisema vipi mtu aweke vitu kama hivyo wakati serikali yetu inasema haina dini unaitwa mara gaidi mara mtafuta shari!
Lkn kwenye upande mwingine ofisi ya serikali aliyemo muislamu kukiwa na dalili za uislamu mwingi basi utaskia kashfa na majungu!
Hakuna mtu anataka kulipwa hapa au kutukuzwa bali kama Nyerere anatajwa mpaka leo kuwa ni baba wa taifa! Basi kuna walio mfikaisha hapo kwenye huo ubaba wake wa taifa na Hao LAZIMA WATAMBULIWE NA WATOTO WETU MASHULENI WAFUNDISHWE KUWA KUNA MASHUJAA WENGINE ZAIDI YA NYERERE!
HII NDIO HASSA HOJA ILIOKO HAPA.
Waislamu wa Tanzania wanapo toa hoja zao na malalamiko yao hakuna anaetaka kusikiliza. zaidi utaskia viongizo wengi wakisema "hao ni wafanya fujo" sasa kumbuka hao wafanyafujo wana haki ya kusikilizwa vilevile na kama watu wataendelea kuziba maskio! Nchi yetu itaelekea kubaya mno!
Mungu ibariki nchi yangu Tanzania.
Amin.
Nashukuru kwa ufafanuzi ambao kiasi umeniongezea ufahamu wa jambo lenyewe.
Nimejaribu kusoma kwa makini nimegundua kuna mambo ambayo ni ya msingi katika hoja hii.
Napenda kukubaliana na wewe kwa mambo yafuatayo katika hoja zako.
1.
Alama za kidini/udini
Ni kinyume cha katiba ya nchi kuendesha maswala ya dini au kuweka alama za kidini katika ofisi
za serikali. Kama kuna mtumishi yeyote atatenda hilo anatakiwa kuchukuliwa kwanza kuelimishwa
ili aache na atoe alama hizo. Akikaidi ni wajibu wetu sote kuchukua hatua za kisheria au za
kumuumbua kwa jamii mfano kuufahamisha umma nini kinaendelea katika ofisi husika. Hili linaweza
kufanyika bila kujali imani ya mtu.
Itakuwa si busara kuzuia kosa kwa kutenda kosa. Hivyo basi iwapo imebainika mtumishi
wa umma anafanya mambo yanayoashiria udini achukuliwe hatua stahiki, siyo kuhamasisha
wengine nao wafanye kosa hilo. Kufanya hivyo ni kulikosea heshima taifa lako na pia
kuwakosea heshima wazee wetu wote waliojitolea kulijenga taifa katika mazingira magumu.
2.
Nyerere peke yake asingeweza kufika alipofika bila watu wengine wengi tu wa
imani mbalimbali ambao walijitolea kumuunga mkono na pia kushiriki moja kwa moja katika
shughuli za kudai uhuru. Watu wote waliojitolea hali na mali wanastahili heshima.
3.Katika harakati za kudai uhuru mikutano ilifanyika sehem mbalimbali
ikiwemo misikiti,
kwa kuongezea ilifanyika pia kwenye vilabu vya pombe, kwenye misiba, kwenye sherehe n.k
Sikubaliani na wewe katika mambo yafuatayo.
1.
Swala la mfumo kristo.
Swala la mfumo kristo lilikuwepo kabla ya uhuru kwa sababu ambazo zinaeleweka
hata shule za enzi hizo zilipendelea wakristo zaidi kwa sababu ya migongano ya kiimani
lakini vile vile kama njia ya kuwagawa watanganyika kukidhi matakwa ya kikoloni.
Baada ya uhuru shule za kidini zilichukuliwa na serikali ili kuondoa tatizo hilo.
Lakini pamoja na juhudi hizo za serikali bado haikuwa rahisi kuwavuta waislamu wengi
kujiunga na shule hizo pengine kwa sababu mbalimbali. Wale wachache waliowahi kutumia fursa hizo
waliweza kupata elimu bila matatizo.
Pia ili kupambana na ubaguzi wa kidini na kuepusha taifa kugawanyika kwa makundi ya kidini
maswala ya kidini yaliondolewa kutoka miongoni mwa majukumu ya kusimamiwa na serikali ili
kuweka fursa sawa na kuondoa uwezekano wa watu kuhudumiwa na serikali kwa kuzingatia imani
yao badala ya utaifa wao.
Kwa sasa swala la mfumo kristo limebaki kama hisia tu na linatumiwa zaidi na watu wanaoshindwa
kujenga hoja hasa vyama vya siasa vinavyotumia nyumba za ibada kuendesha siasa-dini.
2.
Harakati za kudai uhuru kufanyika misikitini kama kigezo cha kutambuliwa kama waislam.
Kama nilivyoeleza hapo juu, nakubaliana nawe kwamba mikutano hiyo ilifanyika pia katika nyumba za
ibada. Lakini sikubaliani na wewe kutumia hilo kama kigezo cha kutaka watambuliwe kama waislam
Nakubaliana nawe kwamba ni sahihi watu wote waliochangia upatikanaji wa uhuru waenziwe kwa njia
kwa njia mbalimbali. Lakini sikubaliani nawe kwamba watu hao waenziwe kwa sifa ya imani zao
kidini. Mfano kwenye historia iandikwe Mzee Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza
wa Jamhuri ya Tanganyika na ''alikuwa Muislam'. Mwalimu Julius alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania
na ''alikuwa mkristo''.
Hili siliungi mkono na sababu kubwa ni kwamba siungi mkono udini.
3.
90% ya cream inayotajwa inahusishwa na ukristo.
Hapa sijaelewa ni kigezo gani ulichotumia kuja na hii namba.
Labda kama una-wahusisha akina Mangi Mandara, Mkwawa, Milambo, Mangungo na wengine wa enzi
hizo. Wote hawa wanaotajwa si wakristo na wala hawakuwa waislam.
Katika watu wote waliotajwa katika historia na vitabu mbalimbali vinavyohusu historia ya kuanzia
mwaka 1950 wengi wanaotajwa ni waislam. Pemgine utanishawishi kubadili mawazo utakapo weka
takwimu halisi ili niridhike. Si lazima takwim zako zifike 90% weka japo zifike 75%.
Hitimisho.
Tuepuke kujenga hoja kwa hisia.
Iwapo malalamiko yanatolewa na hayasikilizwi, pengine ni vema kutafakari iwapo njia inayotumika
kutoa malalamiko ni sahihi.
Mfano iwapo tunalalamika kuna watu muhimu katika historia ya nchi wamesahaulika katika kumbukumbu
za Taifa kwa manufaa ya vizazi vijavyo basi tuyatoe malalamiko hayo bila kuchanganya na mambo mengine kama dini ambayo yanaweza kupunguza nguvu ya hoja.
Tujaribu kutenganisha dini katika hili. Kwa sababu historia ya nchi inapoandikwa ni kwa ajili ya
nchi si kwa ajili ya kikundi cha dini moja au mbili.
Iwapo mafanikio yakipatikana wakawa kwenye historia kama watu wengi ambavyo wangependa iwe, bado haitafuta dini yao wawe ni wakristo, waislamu au wasio wa dini hizo kama kina Kinjekitile.
Mtu Mzima.