Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ni hivi kwa miaka mingi Mohamed Said amewaaminisha watu wa Ulaya na Marekani kuwa mwanzilishi wa AA ni K.Sykes. Si kweli ni mwalimu Cecil Matola.
Amewaaminisha watu kuwa Nyerere aliingia siasa baada ya kukutana na Abdul Sykes, si kweli na imethibitishwa.
Ameanisha watu kuwa hakuwahi kukutana na wajumbe wa AA kabla ya kukutana na Sykes mwaka 1952. SI kweli, alikutana na Dosa mwaka 1948.
Ameaminisha watu kuwa Sheikh Amir alinyimwa fursa katika serikali ya Nyerere baada ya kuongoza harakati za uhuru. Si kweli alipewa nafasi ya uwaziri akaikataa.
Mifano ni mingi sana ambayo Mohamed amekubali kuwa ni matatizo ya uandishi. Kilichopelekea yote kujulikana ni kutokana na Watanganyika wenyewe kuelewa undani na kushindwa kuunganisha dot.
Watu walijiuliza hivi inawezekana mwanzilishi wa chama akawa katibu mkuu bila kuwa na rais au mwenyekiti.
Ndipo waungwana wakasema no way baada ya kufukua wakaona Cecil Matola ndiye mwanzilishi wa wazo.
Kibaya zaidi hata akina Ramadhani Ally hawakuelezewa kwasababu tu wangefunika taswira ya mkusudiwa.
Leo tunajua AA ilikuwa na makamu wa rais.
Kuhusu wazungu nashukuru umekiri kuwa wana uwezo mkubwa na ni kwa uwezo huo kumwalika Mohamed ni sehemu ya kutaka kujua mengine nje ya historia. Utashangaa siku yanapotoka maandishi kuhusu 'extremist' wa East Africa au kuhusu udini Tanzania n.k. kwahiyo usifanye conclusion kuwa wanataka kujua sana kuhusu mzee Kiyate, wana zaidi ya hapo.
Nguruvi,
Usiniwekee maneno yako katika mdomo wangu.
Sijapatapo kusema ''matatizo ya uandishi'' katika mjadala wangu na wewe.
Ikiwa unacho kipande hicho kilete tukijadili.
Tuanze na Cecil Matola.
Ukitaka kujua ushawishi wa Cecil Matola katika siasa za Dar es Salaam ya 1920s
inakubidi kwanza ujue nani walikuwa wakitawala mji.
Kwa hakika si Cecil Matola na taarifa zake ni chache sana katika yale yaliyokuwa
yakitendeka Dar es Salaam.
Huyu Matola hakukaa sana katika uongozi wa AA kwa kuwa alikufa 1933.
Kleist alikuwa na ushawishi mkubwa katika mambo ya Dar es Salaam na ndiyo maana
katika vyama viwili vikubwa vya mjini yeye alikuwa kila siku akichaguliwa kuwa katibu
hata katika chama cha wafanyakazi wa reli alikokuwa akifanya kazi - Tanganyika
Railways.
Kleist alikuwa katiba muanzilishi wa AA (1929) na katibu muanzilishi wa Al Jamiatul Islamiyya
fi Tanganyika (1933). Vilevile katibu kamati ya kujenga shule ya Al Jamiatul Islamiyya Muslim
School.
Lakini kubwa ukimfananisha na wenzake wote Kleist alikuwa akifanya biashara na akatajirika
akiwa na umri mdogo sana...miaka 25.
Hela za Kleist zilisukuma sana harakati mbele na ndiyo kisa cha wanae kuja kutawala siasa za
Dar es Salaam baada ya kifo cha baba yao mwaka 1949.
Hilo wazo la kuanzisha AA alilitoa Dr Aggrey kwa Kleist mwaka 1924.
Taarifa hizi zipo katika mswada alioandika Kleist kabla hajafa na ukitaka zaidi soma maisha ya
Kleist katika Modern Tanzanians kitabu alichohariri John Iliffe na aloandika habari za Kleist ni mjukuu
wake Daisy Aisha Abdulwahid Sykes mwanafunzi wa Ilifee University of Dar Salaam 1968.
Bwana Nguruvi wewe hodari wa kutaja majina lakini tatizo lao kubwa huna taarifa za hao watu
unaowaleta hapa jamvini.
Mimi sijapata kukutana na jina la Ramadhani Ali na mara kadhaa nimekuomba utuwekee hapa
yale alofanya katika siasa za Dar es Salaam lakini hadi leo wewe umekazania kutaja jina lake
tu.
Angalia.
Mabingwa wa AA wanajulikana na taarifa zao wala si siri.
Kuna Erika Fiah ambae akichuana sana na Kleist katika kugombea uongozi wa AA.
Yupo Mzee bin Sudi.
Wapo Hassan Taufik Suleiman, Ali Juma Ponda, Edward Mwangosi na wengineo wengi.
Ramadhani Ali sijapata kumuona si katika majalada ya Sykes wala Tanzania National
Archives (TNA).
Lakini hili si kubwa huenda kanipita pembeni na itakuwa kheri kubwa kwa ukumbi huu
kupata taarifa mpya za mtu huyu.
Ila jua moja.
Hata bingwa wa historia ya Tanganyika John Iliffe hajamtaja Ramadhani Ali popote pale
Mwisho nikuulize Bwana Nguruvi.
Kwa wazee wangu kuondolewa katika historia ya uhuru kulisukumwa na udini hata
unisusulike mimi na udini kwa kuandika kitabu kilichosahihisha historia hiyo?
Mimi ''extremist'' na ndiyo maana napata mialiko...
Mdomo haumkatai bwana wake.
Napata mialiko kwa kuwa yale ninayoandika yana maana.
Tumalize na Nyerere.
Kama una taarifa za Nyerere kufanya makubwa katika siasa za Tanganyika kabla ya
kuja Dar es Salaam na kukutana na Abdulwahid Sykes hebu tupe.
Hiyo kudanadana na Nyerere na siasa za kufikirika haisaidii katika mjadala.
Nyerere ahkuna liyekuwa anamjua katika ulingo wa siasa hadi alipoletwa kwa Abdu na
Joseph Kasella Bantu.
Najua unakereka kusikia habari za baba yangu.
Baba yangu kafahamiana na Nyerere pale nyumbani kwa Abdu Sykes.
Na si yeye tu.
Watu wengi wa Dar es Salaam wamemjulia pale nyumbani kwa Abdu Mtaa wa Aggrey
na kwa Dossa Mtaa wa Mbaruku na wengine pale ofisini kwa Abdu Soko la Kariakoo.
Na katika watu waliomjua kwa karibu sana Nyerere pale Kariakoo Market ni Mzee Abdalla na
Shariff Abdallah Attas.
Kwa watu hawa nimepata mengi sana ya siasa za 1950 nyumbani kwa Abdu na hata pale ofisini
kwake Kariakoo Market.
Hii ndiyo historia ya wazee wangu na Nyerere na hii ndiyo historia ya mji wangu wa Dar es Salaam
nilozaliwa.
Hakuna wa kuja kunifundisha historia hii.
Mimi nimeishi ndani ya historia hii.