Nguruvi3,
Shukran sana,ama kwa hakika mimi naona hapo hujanifanyia rationalization,kwan nakuona waz waz unakiri ya kwamba BAKWATA ilianzishwa na nyerere kwa madhumuni ya kujilinda na mfumo ambao yeye alikuwa anahis unaweza kumuondoa madarakan,si ndiyo??shukran sana kwa kunifanyia CALCULUS iliyokwenda shule,,
Sasa hapo tunakuja moja kwa moja kuzungumza chanzo cha haya yote,unaposema ya kwamba nyerere alikianzisha chombo hiki kwa madhumuni ya kuwadhibiti wachache na kwa bahati mbaya wahanga kama sisi hatuwez kukosekana unafaham maana yake???yan maaana yake ni kwamba yeye julius kwa kutumia jeuri ya madaraka anayo nafas ya kufanya lolote na kufanya maamuz yoyote bila kujali katiba na kuwaundia chombo waislam ambacho kitaratibu mambo yao ili kuufanya utawala wake yy uwe salama,haki hiyo aliitoa wapi kikatiba??
Hii ni inchi ambayo haina dini,na alilweka hilo mwanzo kabisa wa muundo wa katiba wa nchi hii,,haya sasa iweje kuja tena na kuanza kuisakam dini fulani na waumin wa dini fulani kwa kuwaundia chombo cha kuwaratibu bila ridhaa yao na bila kuwashirkisha waislam kwa ujumla wao??
Nyerere kama alikuwa anajua anahujumiwa na baadhi ya waislam na alikuwa anataka kuanzisha chombo huru na cha haki cha kuwaunganisha waislam,kwanin aunde bakwata kimya kimya tena kwa usiri wa hali ya juu bila kuwataarifu waislam kwamba kuna jambo hili,kama hiyo haitoshi kwann hakuwaambia ya kwamba waislam hii EAWMS haifahai kwa sababu moja,mbili na kadhalika,kwahiyo nawaomba muunde chombo kingine huru na chenye nia njema kwa maana hiki tunakivunja??kwanin asiwaambie waislam walifanye hilo wenyew,kuna nin hadi serikali yake ifanye usiri na kutia mkono kwenye affairs za waislam??tena kwa kucopy na kupaste katiba ya TANU ili iwe mwongozo wa jumuiya hiyo,wewe unajua namna ambavyo uislam unaendeshwa??yan Qur an na Sunnah zije kuwa chini ya KATIBA YA TANU kimwongozo??julius ulipotoka sana wewe haki ya mungu,
Nguruvi3,shukran sana kwa kukiri kwako julius ni mwanzishi wa BAKWATA hii japo unakuja na hoja zingine kwamba hakuwa na nia mbaya,non sense..!!,hakuwa na nia mbaya usiri ulikiuwa wa nin??kwanin hakufanya uwe mchakato wa wazi,kwanin hakuwapa fursa hiyo waislam wenyewe kuianzisha bakwata??au ndiyo kusema popote pale alipohisi kuwapo kwa muislam utawala wake ungekuwa matatani??
Narudia tena kukwambia ya kwamba Suala la kikwete na mwinyi kuwa marais ambao ni waumin wa dini ya kiislam na kwanin wao wameikumbatia BAKWATA nilishakujibu,kikwete hakuja pale magogoni,wala hakuapa kuja kuupigania uislam,yeye aliapa kuja kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,na amepigiwa kura kuwapo pale alipo na waislam na wasio waislam,tumuulize nyerere swali hili kwanin alikiuka katiba kwa uchu na chuki ya kuudhuru na kuunyanyasa uislam??yuko wapi leo??uislam aliukuta,ameondoka na ameuacha,je alidhan kama angeupoteza moja kwa moja kwenye mgonngo na ardhi ya tanganyika??
Miaka 10 ya mwinyi na 8 ya kikwete si ya kuja kuutetea uislam,ni ya kuja kutekeleza ilani za chama chao cha mapinduzi,
KWA MANTIKI HIYO BASI KAMA UWEPO WA BAKWATA UNAFANYA UTAWALA WAO HAO KUPATA UTUVU NA WEPESI KATIKA KUTEKELEZA ILANI ZA CHAMA UNADHANI BAKWATA KWAO ITAKUWA NA KERO GANI??HILI NALO NI LA KUWEKA MJADALA BAINA YANGU NA WEWE??HULION HILI??MBONA LIPO WAZI SANA??
Umeniuliza swali ya kwamba tatizo ni bakwata kama chombo au zaid??
Nakujibu,
Tatizo ni bakwata kama chombo,
namna ya kuanzishwa kwake,
lengo la kuanzishwa kwake,
mfumo wa uendeshaji wake,
nia na madhumuni yake kwa miaka ya baadae inayokuja ndan ya taifa hili ambazo kwa sasa matunda yake yameshaanza kuonekana,na hayo ni haya malumbano ya hoja baina yetu sisi na mihemko ya kitaharuki inayotukumba kwa sasa,
KWA MAANA HIYO BASI NGURUVI3,UKAE UKITAMBUA KUWA JAMBO HILI NI NYETI SANA,NA LIMEGHARIM MFUMO WA MAISHA YA WENGI SANA,HASA LINAPOKUJA SUALA LA UMOJA WA KITAIFA,TAMBUA KWAMBA KWA UWEPO WA BAKWATA AMBAYO IMEASISIWA NA JULIUS KAMA ULIVYOKIRI HAPO JUU NI SABABU TOSHA YA KUKUTHIBITISHIA KUWA JULIUS PINDI WALE WAZEE WANAMPA IMAN NA KUMWEKA YEYE MBELE,KUMBE YEYE ALIKUWA KAMA NI CHUI ALIEVAA NGOZ YA KONDOO,LAKIN KIKO WAPI??YUKO WAPI??ALIDHAN ANGEISH MILELE??UKWELI WOTE SASA UKO WAZI NA HAKUNA MAREFU YASIYO KUWA NA NCHA NA HAKUNA SIRI NDAN YA DUNIA HII,MUNGU AMLAZE MAHALA PANAPO STAHILI JULIUS