Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Sheikh Mohamed Said.
Assalamu alaikum warahmatullah!
Huyu mtu maskini hajui asemalo! Hilo jina usingempa basi angekesha kutafuta ni nani huyo ALHAJ MALIK ALSHABAZ a.k.a MALCOM X!
Nakushkuru kumsaidia! Lkn wsws wangu ni kuwa sikio la kufa hili!
Ahsant.
Kahtaan,
Uzee dawa.
Mimi nilipokusoma nilijua umemwekea ulimbo anase.
Lakini nikasema mimi hapa jamvini ndiyo mzee wao na hawa vijana wangu
wapo katika mnakasha.
Nikajisemea katika nafsi yangu kuwa huyu mwenzake huenda akatatizwa na
jina hili nikaona bora nimwopoe ikiwa kwa hakika hana taarifa za Malik Al
Shabaz.
Nikasema hata kama nitamuudhi Kahtaan sasa nifanyeje maana nisipoingia kati
hawa vijana watakuwa katika ''stalemate'' ya bure.
Lakini zaidi nimesikitika kuwa hajui kama Malclom X alisoma dictionary.
Hili jambo ni moja ya maajabu yake na ni kitu mashuhuri katika historia yake.
Ndiyo katika hima yangu ya kumsaidia awe mwerevu nikampa hizo rejea hizo
asome ili atoke huko alikukokuwa.
Malcolm was a brilliant orator.
Tafuta hotuba yake ya Oxford Union 1965 mwenyekiti wakati ule akiwa Tariq
Ali.
Ipo katika Youtube.
Na kwa kweli mtu huwezi kuwa unajua kila kitu.
Na hapa JF ni ulingo wa Watu Wenye Fikra Pevu - Great Thinkers sasa
lazima tusaidiane katika kusomeshana.
Niwie radhi sheikh wangu ikiwa nimemrusha ndege wako.