Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Japo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu baada kuona ukweli amesema wameshazungumza na Hamas ili wawaachie mateka inaowashikilia. Hata hivyo kwa sasa Hamas hawawezi kukubali hadaa.
Mwanzoni mwa vita mwezi uliopita Israel walikataa masharti mepesi ili kuachiwa kwa mateka hao ambayo waliyapuuza wakiamini katika ukali wa silaha zake. Katikati ya vita nafasi ilitolewa tena kwa kuachiwa idadi fulani na bado wakapuuza.
Ilipofikia sasa si rahisi tena kwa mateka hao kupatikana hai. Hivyo Netanyahu atakuwa amebeba lawama kutoka kila upande wa dunia na kutoka kwa raia zake.
Ugumu wa kupatikana kwa mateka hao kwanza ni kuwa hawakuwekwa sehemu moja kama kambi ya wakimbizi. Waligawanywa vikundi vidogo vidogo kila kikundi na muangalizi wake. Katika hali ya kuwepo vifaru ndani ya Gaza haitakuwa rahisi kuwakusanya kutoka maeneo walipo kwa wepesi.
Kwa upande mwengine baada ya Israel kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu ya Gaza wapiganaji wa Hamas hawatopenda kutoa zawadi kwa Jeshi la Israel kwa kuwakabidhi mateka hao halafu wabaki wao wawindwe ili kuuliwa. Kama ni kuuliwa wao basi wataamua wafe pamoja na mateka wao ili kusitokee sinema nyengine ya kusifu ushujaa wa makomandoo wa IDF ambao tayari ukamandoo huo umeshaingia dosari.
Hali ikimalizika kwa namna hiyo ni wazi itakuwa Israel haikutimiza malengo yao yoyote. Fikra ya kuimega Gaza haitofanikiwa kwa namna kadhaa. Pamoja na kupingwa kwa fikra hiyo kutoka kwa washirika wa Israel baada ya kuona ukweli. Waungaji mkono wa Palestina watakuwa wakipata nguvu siku baada ya siku watakapoona shida zitakazowapata wapalestina milioni 2.3 kuminywa kwenye eneo dogo ambapo tayari watu wameanza kulalamika kuwa hawapati nafasi ya hata kulala vizuri kwenye migongo yao kutokana na msongamano kwenye maeneo waliyopelekwa.