7spirits
JF-Expert Member
- Dec 1, 2015
- 612
- 514
Unaongelea umesoma theology au siyo??? Tufuate nini, theolojia na hisia au uhalisia wa neno la Mungu??? Na suala hapa so kufurahia umwagikaji damu. Ni uhalisia wa mini kimesemwa kati ya tabaka hizi mbili na Mungu. Yesu alisema akiwaambia Israel; "...kwa kuwa Siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako"Mimi nilichopinga ni kuwa hakuna sababu ya kuvunja Msikiti ili Israel iwe Israel. Kwani kama Mungu alikuwa hawataki hao waliujenga huo msikiti, wakati wakiujenga kwani alikuwa wapi? Wokovu wetu upo Rohoni na Katika sadaka ya Yesu Kristo. Hayo mengine ya Kuvunja misikiti, kuuwa wengine kama mbwa unayajua wewe. Naijua bibilia kuliko unavyodhani. Nimeenda Shule ya Bibilia, Nimefundisha na Kuhubiri miaka zaidinya 20. Na nimeandika Vitabu 2 vya Kikristo. Najua na Kuamini Israel kama taifa lolote linahitaji kujilinda. Nisichokubali ni kuwa ati Israel imepewa mamlaka na Mungu ya kuuwa na kumwaga damu bila hatia.
Kama unajifanya mjuaji wa Biblia Imeandikwa Wazinzi wapigwe mawe, Je tufanye hivyo leo? Kama hilo halifai, kwanini kupigania ardhi na kuuana ni sawa! Na kwanini Yesu "alivunja" amri kwa kukataa kupiga mawe? Kama kuna upumbavu ulionikuta nao mimi ni hilo la kukataa kupiga mawe, kumwaga damu za wengine kwa Kisingizio cha dini. Upumbavu huo basi Nautaka.
Any one who think that his humanity has more value than that of others, based on his religion, ethnicity, wealth, education or any social grouping, such a person is dangerous and a curse among humanity.
Lk 19:41-44
Sasa swali kwako; HUO WAKATI MUNGU ATAKUWA WAPI???
Lakini pia, ukisoma ufunuo kwa habari ya wale watakatifu ambao idadi yao itatokana na kukatwa vichwa kutokana na mateso ya kuitetea Injili, kwa nini Mungu Aache hivyo??
Na nikukumbushe tu kwamba wanaopigana hapo Mashariki ya Kati sio watu; ni 'MUNGU' na 'mungu' wa watu hao na habari ya Yesu naamini kwa wao wote ni mambo wasiyoyaamini ila pia MUNGU hajaondoa jicho lake juu ya Israeli hata sasa japo walimkataa Yesu . TUMIA VIZURI ELIMU YAKO YA DINI (MAANA ELIMU YA BIBLIA SIYO ROHO MTAKATIFU) NA USITAKE KUPOTOSHA WATU LAKINI PIA KUANDIKA VITABU SIYO LEGALITY YA KUTUPOTOSHA.